Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Tisa ( 29 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Tisa ( 29 )

Written By Bigie on Tuesday, March 13, 2018 | 3:37:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

Na taratibu Amina mfanyakazi wa madam Zena akashika panga alilo kabidhiwa na Olvia Hitler na taratibu akaanza kupiga hatua za taratibu na kisimama nyuma ya Madam Zena na kulinyanyua panga lake juu na kabla hajalishusha mwilini mwa Madama Zena nakiajikuta nikimrukia Madam Zena na sote tukaanguka chini ya kitanda na kumfanya madam Zena kutoa ukelele mmoja wa maumivu makali na akakaa kimya  na watu wote nilio waona ndani ya chumba sikuweza kuwaona tena na kujikuta nikianza kuchangajikiwa baada ya kumuona madama Zena akitokwa na damu za puani na mdomoni

ENDELEA
Nikamnyanyua Madam Zena na kumuweka kitandani huku nikihema kisha nikachukua kanga iliyoning’inizwa nyuma ya mlango kisha nikaanza kumfuta Madam Zena damu zinazo mtoka,Nikikiweka kiganja changu kwenye kifua chake na kukuta mapigo yake ya moyo yakienda kama kawaida na kujikuta nikipata matumaini na wasi wasi ukanipungua kwa kiasi kikubwa.Nikakaa pembeni ya Madam Zena na ndani ya dakika 45 madam Zena akapiga chafya kisha akaanza kufumbua macho na tabasamu likaanza kutawala usoni mwangu baada ya madam Zena kufumbua macho yake na kukaa kitako kitandani
 
“Unajisikiaje mpenzi?”
“Kidogo afadhali”
“Samahani sana kwa kitendo kilicho tokea”
“Kwani Eddy wewe una tatizo gani?”
“Ahaaa ukiwa sawa nitakuambia tatizo langu ila kwa sasa ninakuomba utulie”
“Nitatulia vipi wakati unaonekana kama mtu mwenye mapepo?”
“Sio hivyo ila ukiwa salama nitakuambia”
Nikaanza kujihisi tofauti kwenye viganja vya vidole vyangu vya mkono wa kushoto hii ni baada ya kuto kuiona pete niliyo vishwa na Yudia.Nikasimama huku nikiwa wasiwasi huku nikijitazama kwenye vidole vyangu na nisione kitu cha aina yoyote,
“Unatafuta nini?”
“Kuna pete nilikuwa nayo kidoleni siiioni?”
“Ni pete ya nini?”
“Hiyo pete inanisaidia sana kwenye mambo yangu”
“Ahaa nilikuvua pete hiyo asubuhi wakati ulipo kuwa umelala.....Nilitokea kuipenda sana pete yako”
 
“Ohooo ipo wapi?”
“Niliweka ndani ya droo ya dreasing table”
Madam Zena akanyanyuka na kufungua droo ya dreasing table akaanza kuitafuta taratibu jambo lililo anza kunipa wasiwasi kwani kipindi nilipo kuwa nayo sikuweza kupata tatizo la aina yoyote ila baada ya kuvuliwa na Madam Zena vitu vya ajabu ajabu vinaanza kujitokeza.Nikanyanyuka kitandani na kwenda alipo madamZena na tukasaidiana kuitafuta
“Kwani wewe uliiweka wapi?”
“Niliiweka humu ndani tuu kwenye hii droo”
“Aaahh sasa atakuwa ameichukua nani?”
“Saijajua.....kwani ina umuhimu sana”
“Tena umuhimu wake ni zaidi ya sana”
Tukaendelea kuitafuta pasipo kuiona kiasi kwamba  nikaanza kuchanganyikiwa japo madam Zena analichukulia ni jambo la kawaida sana katika pete hiyo.
 
“Baby tutaitauta baadaye?”
“Zena Zena umenitafutia matatizo?”
“Matatizo gani mpenzi wangu?”
“Ile pete inanilinda mimi na watu wabaya na hapa tulipo kuwa humu ndani kwako kuna watu walinitokea ndio maana ukaona nimekukukumba?”
“Eddy mbona unanitisha?”
“Sio ninakutisha huo ndio ukweli wenyewe”
“Mmmmm sasa inakuwaje?”
“Mimi mwenyewe sijui hata itakuwaje”
Tukabaki kimyahuku kila mmoja akibaki akimtazama mwenzake.Madam Zena akanipa tenge nikajifunga kwani kwa wakati wote nilikuwa kama nilivyo zaliwa kisha tukatoka chumbani huku yeye akiwa ametangulia mbele,Nikakutana na Amina akiwa amebeba sahani za dongo alizotoka kuziosha.Macho yangu yakatua kwenye vidole vyake na kuiona pete yangu.
 
“Wee weee hembu mara moja”
Nikamsimamisha na kumfanya madam Zena kunishangaa na nilicho kifanya ni kumvua Amini pete iliyopo kidpleni mwake
“Haya wewe Amina umeingia saa ngapi ndani kwangu na kuchukua pete ya shemeji yako?”
Amina akabaki kimya akikosa kitu cha kuzungumza na tukio la yeye kutaka kumkata Madam Zena kwa panga ikanijia kichwani kwangu na kujikuta nikimtazama Amini kwa mach makali
“Si ninakuuliza wewe......huo mtindo wa kuchukua vitu vya watu imeanza lini?”
“Niliingia chumbani kufanya usafi?”
“Usafi wakati shemeji yako yupo umeshaa anza tabia mbaya ehee?”
“Nisamehe dada Zena sinto rudia tena”
“Amina utarudi kwenu ohooo maswla ya ajabu ajabu mimi sipendi......wewe unajua kabisa kuwa leo nina mgeni chambani kwangu na wewe asubihi asubuhi unaingia na kuchukua vitu vya watu wewe unajua ina kazi gani hiyo pete?”
 
“Lakini dada katika swala la kuwa na mgeni mimi sikulijua kwa maana jana alivyo kuja mimi sikumuona”
“Hembu nenda kaendelee na kazi zako majini yangu yasije yakanipanda ninaimani unanijua vizuri sana”
Amina akaondoka na kutuacha sisi tukikaa sebleni na nikaichunguza pete yangu na sikuona mabadiliko ya aina yoyote na kujikuta nikijiuliza maswali yasiyo na  majibu
“Hvi imekuwaje na Amina amekuwepo kwenye mkumbo wa kina Olvia......? Na kama pete iliwekwa kwenye droo huyu Amina ameionaje............ ? Kuna kitu hapa kinach endelea itanibidi nikijue”
Nilijisemea huku Madam Zena akiwa anabadilisha badilisha chanel za kwenye Tv na baada ya muda tukapata kifungua kinywa  na kabla hatujamaliza kunywa simu ya madam Zena ikaaita
“Mama anaumwa?”
“Mumepeleke hospitali”
“Kwahiyo yupo Teule eheee?”
“Haya ninakuja kumuona”
 
Madam Zena akakata simu na kunyanyuka na kuekekea chumbani kwake na mimi ikanibidi nimwfwate kwa nyuma na kumkuta akianza kuvua nguo moja baada ya nyingine huku akitafuta nguo ya kuvaa kwenye kabati lake
“Eddy mama yangu anaumwa sana”
“Yupo wapi?”
“Muheza hapa inanilazimu kwenda Muheza kumuona”
“Na mimi ninaweza kwenda?”
“Hapana ngoja tu mimi niende nitarudi kesho kama hali yake ikiwa mbaya nitakujulisha”
“Mimi sijaja na simu yangu huku kwako?”
“Ipo wapi?”
“Ipo nyumbani kwangu?”
“Basi nitawasiliana na Amina na nitamueleza kila kitakacho tokea”
“Sawa.....ila roho yangu inasita kabisa kukaa humu ndani kwako”
“Unamuogopa nani?”
“Simuogopi mtu ila kukaa humu kwako mimi sina imani nako kabisa na kama unavyo jua kwamba huko uraiani nina soo”
“Tungeenda wote ila nguo zako ndio kwanza zinafuliwa”
“Ahaaa sasa daaaa haya mwayasafari njema”
Madam Zena akamaliza kuvaa nguo zake kisha tukatoka chumbani na Madam Zena akamuaga Amina
“Unaondoka na gari lako?”
“Hapana sijalifanyai servise nitaoanda Costa.....Amina na shemeji yako umueshimu nisije nikarudi hapa nikakuta hali ya tofauti na nilivy kuacha utajuta”
 
“Dada siwezi kufanya chochote kibaya?”
“Na iwe hivyo kwa maana unanijua vizuri”
“Sawa dada safari njema”
“Ila si kila kitu kipo kwenye friji?”
“Ndio ila ni soseji ndio zimebaki chache”
“Kwenye droo yangu ile ya upande wa kushoto kuna kwenye kitanda kuna elfu hamsini utanunua vile ambavyo utaona vimepungua ila kesho au kesho kutwa ndio ninaweza kurudi ila ninakuomba uwe makini sana”
“SAWA”
Madam Zena akanibusu mdomoni kisha akaondoka zake na sisi tukarudi ndani na kujikuta furaha yangu ikiisha kabisa kwa maana Amini aliiapia kabisa kuwa nitaona.Nikapitiliza hadi ndani pasipo kumuongelesha Amina kitu chochote kisha nikafunga mlango kwa funguo na kujitupa kitandani nikianza kuutafuta usingizi ila sikuupata kabisa.Nikasikia mlango ukigongwa huku amina akaniomba nifungue kwani tayari chakula cha mchana kipo tayari.
 
“Ninakuja”
Nikajinyanyua kitandani na kujifunga tenge langu vizuri na kwenda sebleni na kukukita chakula juu ya meza.
“Amina nguo zangu zipo wapi?”
“Zimesha kauka nataka nizipige pasi”
“Basi ninaomba unifanyie mpango huo”
“Sawa”
Nikala haraka haraka na kuingia bafuni na kuoga kisha nikatoka na kuzikuta nguo zangu zipo tayari nikazivaa kidogo nikapata amani kwani hata lolote litakalo tokea ninawza kuondoka zangu
“Shem unaondoka?”
“Ndio nataka kwenda kwangu mara moja”
“Sawa ila shem ninakitu ninaomba kukuuliza?”
“Niulize”
“Wewe na dada mapenzi mumeanza lini?”
“Kwa nini?”
“Nataka kujua tu mapenzi yenu mumeanza lini?”
“Mmmm hilo swali ni gumu na nijepesi ila yameanza siku nyingi tuu”
 
“Kweli?”
“Mbona unamaswali mengi?”
“Kwa maana dada anamume wake ambaye yeye ni mwanajeshi na siku si nyingi anaweza akarudi ikawa ni balaa kwako na jinsi shemeji yangu yule alivyo na roho mbaya inaweza ikawa ni hatari kwako”
Maneno ya Amina yakapita moyoni mwangu na kujihisi kama nimekatwa na kisu kikali na maumivu yake yameendana na mshangao mkubwa kwa maana sikutarajia kama madam Zena anaweza kuwa na mwanaume kwani kwa jinsi alivyo nifanyia vutu vyote ni sawa na mtu asiye na mwanaume kwani kila kitu amekifanya kwa kujiamini.
“Poa ninashukuru kwa taarifa yako”
“Ila usije ukamwambi dada kwa maana ninaweza kupoteza kibarua changu na kwetu mimi ndio ninaye tegemewa”
“Sawa sinto mwambia.....Ila na wewe asubuhi ilikuwaje hadi ukawa unanilazimisha kufanya mapenzi?”
“Nilivyo ivaa hiyo pete yako sikuwa ninajielewa nikawa ninahisi kuwa na hamu ya kufanya mapenzi na wewe ila nakuoma unisamehe kwa hilo pia”
 
“Sawa”
Nikaondoka na moja kwa moja nikaenda hadi nyumbani kwangu na nikasimama kwa mbali kidogo kuangalia kamwa kuna ishu yoyote inayo endelea nyumbani kwangu ila sikuweza kumuona mtu wa aina yoyo akiwa nyumbani kwangu.Nikapiga hatu za umakini hadi getini kwangu na kukuta geti langu limerudishiwa,nikachunguliwa kwa ndani na sikumuona mtu wa aina yotote.Nikasukuma geti taratibu na kuingia ndani huku nikizidi kuwa makini kwani endepo kutakuwa na mtu wa aina yoyote asiweze kuniona,nikaingia sebleni na kukuta kukiwa kama nikivyo kuacha nikapitiliza hadi ndani kwangu na kuikuta hali ni ile ile ya jana,Nifungua kabati langu na kuanza kuchukua nguo moja baada ya nyingine na kuziingiza kwenye begi langu kubwa la mgongoni.Nikaanza kuitafuta simu yangu na kuikuta ipo chini ya uvungu wa kitanda kwa umbali kidogo na ikanilazimu kuinama na kuanza kuunyosha mkono wangu ili kuutona na nikafanikiwa na kabla sijanyanyuka nikahisi kutu kigumu kikinigusa kichwani kwangu
“Simama hivyo hivyo la sivyo niakuchangua kichwa chako”
Nikasikia sauti nzinto ikizungumza nyuma yangu na kujikuta nikianza kutetemeka na kujutia ni kwanini nimekuja nyumbani kwangu
 
“Simama”
Nikasimama na kuwasikia watu wawili watatu wakiwa wanajadiliana kitu cha kunifanya
“Ila bosi amesema tumpeleke akiwa hai kwa maana anataka kumuua kwa mkono wake yeye mwenyewe”
“Huyu bila kumpiga hatuto weza kumpekeka kwewe unamuonaje mtu mwenyewe?”
Nikageuza shingo yangu nyuma na kwakutumia pembe ya jicho langu la kulia nikawaona watu watatu wakiwa wamevalia vinyago vilivyo yaacha macho yao kuwa wazi ila sehemu nyingine za uso zao zikiwa zimezibwa na mmoja akiwa ameshika bastola.Nikageuka gafla kabla sijachukua maamuzi ya kumpiga aliye shika bastola yake nistukia kitako cha bastola kikitua kichwani kwangu na kunifanya niangukie kitandani na kupoteza fahamu

Nikastuka nikiwa nimening’inizwa kichwa chini miguu yangu ikiwa juu na imefungwa na kamba ngumu ambayo sio rahisi kwa mimi kuweza kuanguka kirahisi,Mikono yangu ikiwa imefungwakwa nyuma na kamba pia na sikuweza kuona ni sehemu gani ambayo mimi nipo kwani nip ndani ya chumba chenye sakafu iliyo chakaa huku kwa juu kukiwa na kijikidirisha kimoja kidogo kinacho ingiza mwanga hafifu wa jua na kadri muda unavyo zidi kukatika ndivyo jinsi giza lilivyo tawala ndani ya chumba hichi hadi mwisho wa siku sikuona kitu cha aina yoyote kutokana na giza nene
 
Baada ya masaa mawili mbeleni kikahisi mngurumo wa gari ukisimama nje ya kibanda na baada ya muda gari lilazima,Nikastukia taa ya mshumaa kiawaka ndani ya chumba kisha mlango ukafunguliwa na akaingia jaa mmoja mweusi sana kiasi kwamba nikaanza kuogopa kwani mwili wake ulivyo tanuka ninaweza kuwafananisha na wale wanao cheza michezo ya myereka nchini Marekani.Wakafwatia wazee watatu wa kiarau wakiwa wamevalia kanzu nyeupe na mmoja nikamfahamu kwa haraka kwani ndio baba yeke Rahma ambaye jana nilimpiga kikumbo getini
 
Wakaanza kunong’onezana vitu ambavyo sikuweza kuisikia kisha kwa ishara akamuamrisha jamaa mweusi na nistukia ngumi nzito ikitua tumboni mwangu na kuifanya kamba kuzunguruka na mimi mwenyewe nikazunguka ngumi mvululizo kutuka kwa jijamaa hili ambalo linaonekeana kuwa na haruma hata kidogo zikazidi kutua mwalini mwangu na unaweza ukasema ni Mayke Tysona anavyochuka mazoezi ya kulipiga ‘Panch beg’ la mazoezi.Mwili wangu wote ukazidi kutawaliwa na maumivu makali huku nikitoa makelele ya kuomba msaada
 
“Wewe huwezi kumtia mimba mwanangu.....sitaki azae na watu weusi”
Baba Rahma alizungumza na kumfanya jamaa kuzidi kunipiga ngumi zilizo zidi kuulainisha mwili wangu na maumivu yakazidi kunitawala na damu za puani zikaanza kunimwagika
“NAOMBA UNISAMEHE MZEE WANGU”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika na kumfanya baba Rahma kumuamrisha jamaa kuacha kunipiga kisha akamuomba anivue shati langu na jamaa akalivuta na likachanika vipande vipande.Baba Rahma akatoa kisu cha kukunja kwenye kanzu yake na kukiminya sehemu kikafyatuka kisha akanisogelea na kukogoa kuhozi kubwa na kunitemea usoni,Akaniguza na kumuachia mgongo na akaanza kinichana chana kwa kutumia kisu chake na kujikuta nikipiga kelele za kumba msaada ila sauti yangu haikupata msaada wa mtu wa aina yoyote.Akanigeuza na kauendelea kunichana chana na kisu chake kwenye kifua changu na nikaizidi kulia huku maumivu makali yakendelea kuutesa mwiki wangu.
 
Kazee kamja ka kiarabu kakamzuia baba Rahma kuendelea kunichana kwani mwili wagu mzima ulilowana damu zilizo uchafua uso wangu hii ni kutokana na kiwa kichwa chini miguu juu.Mzee aliye mzuia baba Rahama akaishika bakora yake na kuanza kunichara mikwaju mingi isiyo naidadi kiasi kwamba nikajikuta nikilia hadi nikaanza kucheka kwa uchungu.Mzee anaye nichapa akazungumza maneno ya kufoka kwa kiarabu kisha akaitupa fimbo yake chini na kunishika masikia yangu na kuaza kuyavuta huku akinitingisha tingisha kichwa changu
 
Akaniamchia na wakazungumza na kutoka ndani ya chumba na kuniacha nikiwa ninalia kwa uchungu kiasi kwamba nikamuomba Mungu aweze kunichukua kwa wakati huu niweze kupumzika mahali pema peponi,Taa ikazimwa na nikaendelea kuvuja damu na nikalisikia gari likiwashwa na kuondoka.Ndani ya robo saa nikahisi kufuli la mlango likifunguliwa nikajua wanarudi tena ila nikaona mtu akiingia akiwa amevalia nguo nyeusi kutokana na damu zilizo tanda usoni na giza kali sikuweza kuona ni nani
“Ohhh Eddy mpenzi wangu”
Nikajua ni Rahma baada ya kuisikia sauti yake kisha akanikumatia huku akiwa analia kwa uchungu,
“N....ifungue”
Nilizungumza kwa shida na kumfanya Rahama kuanza kutafuta swichi ya kuwashia ndani ya chumba ila hakuiona,
“Ra...hma unatafuta nini?”
“Semehe waliyo ifunga hii kamba”
Rahma kwa bahati nzuri akaiona sehemu niliyo fungwa na kutokana na ugumu na kukazwa kwa kamba hii ikamlazimu kutoka nje na nikastukia taa ikiwashwa na akaingia huku akiwa ameshika jiwe lenye ncha kali ila baada ya kuniona jinsi nilivyo akabaki akiwa ananishangaa kiasi kwamba akazidi kulia
 
“Rah...ma”
Rahma akastuka na kuanza kupiga hatua za haraka hadi sehemu yenye nondo iliyo kitwa kutani na ndipo kulipo fungwa kamba iliyo kwenda kwa juu na kupita kwenye chuma kingine na kunining’iniza.Rahma akaanza kuipiga piga kamba kwa kutumia nguvu zake hadi kamba ikaanza kukatika taratibu
“Jika...ze....Ba...by”
“Sawa mume wangu”
Rahma akajitahidi kukata hadi kamba ikakatika yote na kunifanya nianguke kama mzogo na nizidi kapata maumivu mengi.Rahma akanifwata na kunikumbatia huku akiwa analia kisha akanza kunifungua kamba za mikononi nilizo fugwa kwa nyuma.Rahma akaninyanyua na kutokana na kipigo kikali nikajikuta ninakosa hata nguvu za kuniwezesha kutembea.Rahma akauchukua mkono wangu mmoja na kuupitisha begani mwangu na kuninyanyua na taratibu tukaanza kutembea taratibu kutoka nje na kuuona msitu mkubwa na kwa mbali tukaziona taa za gari zilija eneo la chumba kilichopo.
 
“Mungu wangu ni gari ya baba.....Eddy jikaze tuondoke”
Rahma akanihimiza na nikajikaza japo mwili wangu umepoteza nguvu na tukaanza kutokomea msituni na mwendo wa dakika kama tano nikakuta gari ambayo Rahma mara nyingi huwa huitumia.Akaniingiza kwenye siti ya mbele kisha na yeye akaingia upande wa dereva na akaiwasha gari na kuotoa kichakani alipo ificha na kwa kasi ya ajabu akaingia barabara ya vumbi iliyopo ndani ya msituu huu na kuendelea kuliendesha gari na sikujua tunaelekea wapi.Galfa nimamuona Rahma akitoa msunyo mkali kiasi kwamba kwa shida nikakinyanyua kichwa changu na kuangalia nyuma na kuona gari ikijakwa kasi huku ikiwa imewasha taa zake zenye mwanga mkali na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kunienda kasi
 
Gari tuliyomo ikaanza kutoa mlio ulio ashiria mafuta ya gari kuisha na kadri tunavyozidi kwenda ndivyo gari lilivyozidi kupungua mwendo na kuliruhusu gari la nyuma yetu kutufikia kwa ukarubu zaidi na mwish wa siku gari ikasimama kabisa na kumuona Rahma akitetemeka mwili mzima na asijue nini anafanya.Gari ya baba Rahma ikasimama kwa nyuma yetu na kumuona baba Rahma akishuka huku mkononi mwake akiwa na bastola,Wakafwatia wazee wawili wa kiarabu pamoja na lile jijamaa jeusi.Nikashika kitasa cha mlano na kukifungua na kudondoka chini kisha kwa tabu nikasimama huku nikiwa nimelishaka gari kwa msaada wa kuto kudondoka
“Eddy nini unafanya?”
“Nipo tayari kufa Rahma siwezi kuishi tena.....Niache nife mbele yako”
Nilizungumza kwa uchungu huku nikiwa nimejishika tumboni kwenye maumivu malali na kumfanya Rahma kushuka kwenye gari kwa haraka na kusimama pembeni yangu huku akilia na kumuomba baba baba yake asifanye kitu anachotaka kukifanya.Baba Rahma akaikoki bastola yake na kunielekezea mimi huku akiwa amesimama umbali kidogo na sehemu tuliyo simama sisis akimsikiliza mwanaye kitu anacho kizungumza
 
“Baba kumbuka kwamba mimi ni mwanao na ninauhuru wa kuchangua na kufanya kila ninachi kihitaji na siwezi kumuacha mwanaume ninaye mpenda katika maisha yangu”
“Nyamaza wewe mshenzi...mwanaharamu siwezi kukuruhusu kuwa na watu kama hao”
“Mzee wangu fanya unacho kifanya nipo tayari kwa lolote utakalo liamua”
Maneno yangu niliyazungumza kwa uchungu huku nikiwa ninatokwa na machozi na nikapiga hatua mbili mbela na kustukia mlio wa bastola na kujikuta nikiwa nimeanguka chini huku taratibu nikimshuhudia Rahma akianguka huku akiwa amejishika tumboni akitoa kilio cha maumivu makali hii ni baada ya Rahma kunivuta mimi pembeni na yeye kupigwa na risasi ambayo baba yake aliifyatua kwa lengo la kunipiga mimi ili kuniua

 ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts