Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Nane ( 18 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Nane ( 18 )

Written By Bigie on Thursday, March 1, 2018 | 5:30:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

      Nikakata simu na kuendelea na safari yangu na kwa mbali kutoka nilipo hadi ilipo nyumba ya bibi nikaona nje kumefungwa turubai huku watu walio valia kanzu wakiwa wamekaa kwenye majamvi huku ukimya ukiwa umetawala katika endeo hilo.Nikazidi kuongeza mwendo huku akilini wazo la bibi kuwa amefariki dunia likaanza kunitesa,Kabla sijafika karibu na sehemu ilipo nyumba ya bibi nikastuka mtu akinishika mkonno kwa nyuma huku akinivuta kwa nguvu

ENDELEA
     Nikageuka na kukutana na sura yam zee wa makamo akiwa amavalia kanzu nyeupe na barakashea huku mkononi mwake akiwa ameshika mkongojo wa kumsiadia katika kutembelea
“Shikamoo mzee”
“Shikamoo yako haina msaada wowote kwangu”
Mzee alizungumza kwa hasira huku akiachia msunyo mkali hadi nikabaki ninamshangaa huku nikijiuliza nilicho mkosea ni nini
“Wewe kijana ni mbaya sana…..Kijana huna adabu shiii nkumi,kijana huna busara.Yaani umeona haitoshi umeamua kutuma majini yako kuja kumdhuru mke wangu”
“Mzee mbona sikuelewe umechanganyikiwa nini?”
“Mimi nimechanganyikiwa.PUMBAVU SANA WEWE”
Mzee akanichapa bakora moja na kunifanya nimponyoke mkononi mwake na kusimama pembeni nikiwa ninamshanga huku watu wengine walio karibu yetu wakitushangaa kwa tukio alilo lifanyia babu
 
“Vijana wa siku hizi hamuuna adabu sana unaniambia nimechanganyikiwa mimi?”
“Oya brother Eddy huyo mzee ni kichaa asikupotezee muda wako wewe achana naye”
   Alipita jamaa mmoja na kuniambia kuhusiana na huyo mzee ambaye kwenye macho yangu sikuwahi kumuona siku hata moja katika mtaa nilio kuwa nimekaa.Nikaamini mzee hana akili vizuri baada ya kuanza kumkimbiza kijana aliye niambia kuwa mzee huyo ni kichaa.Nikajiweka vizuri shati langu na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya bibi iliyo jaa watu nje wenye kanzu nyeupe.Bibi akaniona na kuja kunifwata na kunikaribisha na kunionyesha stuli isiyo kaliwa na mtunkisha nikaichukua na tukasogea kidogo na kukaa pembeni na walipo watu wenye kanzu nyeupe huku bibi akikaa juu ya gogo la muembe ulio katwa siku nyingi
“Bibihapa kuna nini?”
“Ni maulidi ya mwanangu mmoja wa kike anayafanya kwa mtoto wake alieye zaliwa miezi kadhaa ya nyuma”
 
“Ahaaa mbona kumetulia sana?”
“Ahha ndio wanamalizia malizia…”
“Inamaana watu tayari wameshamaliza kula ubwabwa?”
“Ubwabwa wamekula tangua amchana hapa wanasubiri kufunga maulidi”
“Bibi bwana mimi nimekuja nina tatizo tena sio dogo nitatizo kubwa kiasi kwamba ninajikuta nimechoka kwenye tatizo lenyewe”
Bibi akaanza kucheka na kwajinsi ya meno yake kuwa pungufu mdomoni mwake na kuweka mapengo makubwa ikanilazimu na mimi kuanza kumcheka
“Eddy mjukuu wangu ile jana ulivyo kuwa unahama unakumbuka nilikupa nini?”
“Ulinipa maji kwenye kichupa?”
“Uliyatumia?”
“Bibi nisikudanganye nilisahau?”
“Hapo ndipo ulipo kosea na yule msichana uliye hama naye ndio aliye kusababishia matatizo hayo”
“Amenisababishia matatizo hayo kivipi?”
“Ngoja nikuambie kitu usicho kijua kuhusu yule msichana”
Nikajiweka vizuri kwanye stuli niliyo ikalia huku nikimtazama bibi kwa umakini 
 
“Yule binti anaitwa Hilda si ndio?”
“Ndio”
“Hilda yule binti amefunga ndoa na jini moja linaitwa Seifh na jini hilo lipo katika kifungo baada ya kukiuka sheria zao za ujini.Na binti yule Alisha zoea kufanya mapenzi na jini ambeye tayari  amevishwa pete ya uchumba na mangasuti?”
“Ngoja bibi….Mangasuti ndio nini?”
“Mangasuti ni kitambaa Fulani hivi hutumiwa na watu wenye asili ya India katika swala zima la ndoa”
“Ahaa apo nimekuelewa…Sasa imekuaje kuaje Hilda akafunga ndoa na jinni?”
“Amefunga ndoa na jini bila yeye kujua na ndoa yao siku inafanyika ilifanyikia chini ya bahari…..Na baada ya jini aliye muoa kuwekwa kizuizini basi imekuwa ni ngumu kwake yeye kuweza kukaa bila mwanaume kwani hamu zote zilikuwa zinamalizwa na huyo jinni”
“Walipo kuwa wanafanya mapezni alikuwa anamuona jinni huyo?”
 
“Ndio alikuwa akimjia kwenye njozi kiasi kwamba anajibadilisa badilisha kwenye sura za tofauti tofauti leo anaweza akajiweka sura ya mtu maarufu duniani…..Yaani humjia katika naamna yeye atakavyo”
“Mmmm sasa bibi yule msichana ameniganda kiasi kwamba hataki kutoka nyumbani kwangu”
“Nilazima akugande kwani amepata ladha ya mwanadamu mwenzake tofauti na majini ambao ladha zao ni tofuati sana na mwanadamu na wengi wao ladha zao huwa si nzuri kwa yule anae fanya naye”
Nikajikuta nikichoka baada ya kuyasikia maneno aliyo niambia bibi na kujikuta nikianza kumpangia mbaya Hilda
“Tuje sasa katika tatizo lako linalo kupelekesha na lisipo tatuliwa mapema litakuondoa duniani”
Moyo ukanipasuka kiasi kwamba nikajikuta nimemtumbulia mimacho bibi hadi mwenyewe akaanza kuogopa
“Babu weeee unanitisha na hiyo mijicho yako…Umesikia kuondoka duniani ndio unashangaa kiasi hicho”
 
“Bibi acha tu nishangae katika hilo”
“Maana yangu ya kuondoka duniani sio kufa”
“Una maana gani?”
“Unaondoka duniani na kuhamishiwa katika ulimwengu mwengine ambao utaishi kama Mzimu?”
“Mzimuuu!!?”
‘Makelele ya nini sasa”
“Ahaaa bibi sasa huko ni kwengine kabisa”
“Ndio ukweli wenyewe siwezi kukuficha kwani maisha yako sasa hivi yapo hatarini”
“Sasa bibi kwanini ni mimi kila siku?”
“Eddy kunakitu sikuwahi kukueleza mwazoni nikijua  kwa wakati ule halikuwa na maana sana kuweza kukuambia”
“Jambo gani?”
“Eddy katika watu wenye nyota kubwa duniani wewe ni mmoja wapo.Na nyota yako hiyo inawindwa na watu wengi ili kuweza kuichukua……Ndio maana unaweza kuona jinsi unavyokubalika katika sehemu nyingi na watu wa kila aina.Wewe unaweza kuona ni kitu cha kawaida ila si hivyo una kitu kinacho kufanya uwe hivyo”
 
“Sasa bibi kama ni hiyo nyota basi waichukue mimi waniache niishi kwa amani kwani saa hivi kuna mwanamke ananitokea toke asana na kunifanyia vituko vya ajabu kiasi kwamba nijikuta ninachoshwa na mambo yake”
“Tena shukuru Mungu huyo msichana amekutokea kwani ni mwema kwako…..Ila angekutokea yule mwenye mke wake ungekuwa umeshakufa na isitoshe huku alipo anaona kila kitu unacho kifanya na mke wake na anamipango mibaya ya kukuangamiza ndio maana ninakuambia kuwa nyota yako inanguvu sana”
“Sasa bibi mbona unazidi kunichanganya inakuwaje yule mwanamke anaye nitokea ni awe mzuri kwangu wakati yeye sio binadamu?”
“Ni mzuri na ndio mwenye jukumu la kuilinda nyota yako la sivyo  utakuwa mzimu kama nilivyo kuammbia”
“Mmmm bibi hakuna hata dawa ya kulamba kidogo nisimuone kwa leo usiku?”
“Eddy mmjukuu wangu dawa ya kulamba wala mimi sina kwani yule sio kiumbe wa kawaidana laiti kama nikimuingilia kwenye mipango yake nilazima na mimi niudhurike”
 
Nikakaa kimya kwa muda huku wazo la kuondoka likanijia kwani hadi hapa nilipo fikia ninaona bibi anataka kunichanganya kiasi kwamba anataka nianze kuamini vitu visivyo aminika
“Bibi ngoja mimi niende wewe baki salama”
“Sawa mjukuu wangu japo umechelewa ningekuandalia hata kitu cha kula”
“Bibi hapa ni kwangu nitakuja kula siku yoyote”
“Sawa mjukuu wangu”
“Hivi hapa kumeshapata mpangaji?”
“Hapana si umehama jana tu”
“Mmmm haya mwaya bibi ninakutakia siku njema na maulidi mema”
“Na wewe pia mjukuu wangu ninakutakia mapumziko mema na Olvia Hitler”
Nikastuka kusikia jina na Olivia ikanibidi nisimame kwa sekunde kadhaa huku nikimtazama bibi
“Mbona unanishangaa?”
“Nashangaa hilo jina umelijuaje?”
“Kwani ni mangapi ninayo kuambia ambayo huyajui ndio sembuse la huyo Olvia”
“Mmm sawa bibi kigiza hichi kinaingia ngoja nikawahi dalala”
“Sawa mjukuu wangu”
 
   Nikapita nyuma ya watu walio kaa kwenye majamvi huku wote wakinishangaa nikajua ni labda nilivyo katiza nyuma yao bila kuwasalimia.Naikaanza kupiga hatua za haraka huku nikidhamiria kummfukuza Hilda aondoke zake pale tu nitakapo fika nyumbani asije akaniletea matatizo ambayo sikutarajia yaweze kunipata kwa wakati huu.Kabla sijafika mbali na nyumbani kwa bibi nikasikia ninaitwa kwa nyuma na sauti ambayo ninaifahamu.Nikageuka na kumkuta ni Mama Fety akija kwa hatua za haraka huku tenge lake alilo livaa likimdondoka dondoka huku akijitahidi kulifunga vizuri
“Mambo vipi?”
“Safi tuu Eddy mzima wewe?”
“Mimi mzima “
“Kuna mtu amenifwata na kunitaarifu kuwa wewe umechanganyikiwa?”
“Nimechanganyikiwa na nini…Au ndio umbea wenu munao anza kuzungumza zungumza kwa watu”
“Eddy hasira ya nini jamani wakati nimekuuliza kwa ustaarabu jamani”
 
“Hakuna cha jamani nyinyi wanawake wa mtaa huu wambea sana”
“Eddy kama nimefanya kosa kukuuliza ninakuomba unisamehe na wala sikuwa na  haja ya kutaka kukuudhi ila ulicho kifanya pale msibani kwa watu sio vizuri”
“Msibani wapi?”
“Si pale kwa bibi Mwanavita”
“Bibi Mwanavita mimi mbona simjui?”
“Ni yule bibi aliyekuwa anaishi jirani yako pale si amefarika dunia asubuhi ya kuamkia leo na wewe umekwenda pale wala hukutaka kusalimia na watu waliopo kwenye msiba na mwenyewe ukatafuta sehemu uakajikalisha na kuanza kuzungumza peke yako”
Moyo ukanipasuka nikahisi mwili unaishiwa na nguvu ikanibidi nikae kwenye kibaraza cha pembeni ya nyumba tuliyo simama nje yake huku mapigo ya moyo yakinienda kasi na kwa mbali kajasho kikaanza kunimwagika huku nikijiuliza yule niliye zungumza naye atakuwa ni nani na mbona nimeogea naye ina maana watu wengine hawakumuona.Maswali yangu yote sikuyapatia majibu ya kuaminika
 
“Wee unataka kusema yule bibi amefariki?’
“Bibi wa watu amefariki na amezikwa leo saa sita mchana kwenye makaburi ya kwa Minchi sasa nakushanga wewe uanye kwenda pale na kuzungumza peke yako unaonekana kama umetumwa”
Maneno ya Mama Fety yakazidi kunichanganya kwani sikulewa kitu kinacho endelea.
“Ina maana yule niliye zungumza naye sio bibi?”
‘Sasa unamuuliza nani aliye muona huyo unaye zungumza naye?”
Nikakosa kitu cha kuzungumza na kujikuta nikinyanyuka taratibu huku nikijihisi vibaya vibaya nikapiga hatua mbili mbele na kizunguzungu kikali kikanipata na kujikuta nikienda chini kwa kasi ya ajabu na kuanguka kama gunia na giza kali likayatawala macho yangu na sikujua ni nini kinacho enedelea

                                                                ***
     Nikaja kuzinduka na kumkuta Mama Fety akiwa pembeni yangu amekaa nikakitizama vizuri chumba nilichomo na kugundua nipo hospitali kwani nilijikuta nimetundikiwa dripu la maji kwenye mkono wangu wa kushoto.Nikakaa kimya huku akili yangu ikinirudisha nyumbani kwa bibi na kuaanza kuyakumbuka maongezi yatu kisha nikayakumbuka maongezi ya mama Fety nikajikua nikipiga kelele na kumfanya mama Fety kutoka kwa haraka uku akiwaita manesi ambaao baada ya muda mfupi wakaingaia ndani ya chumba nilicho kuwepo na kujikuta nikinyamaza kimya na kuwatazama
 
“Huyu mgonja wako usinge muwahisha hii malaria ingempanda kichwani”
Nesi mmoja alizungumza huku akitoa dawa kwenye kichupa kidogo kwa kutumia sindano yenye bomba kisha akanishika mkono wangu wa huku mwezake akinifunga mpira unao vutika kwenye  msuli wangu kisha nesi aliye shika bomba la sindano akanipaka dawa kwenye kiungio cha mkono wangu kisha akanichoma sindano na kuisukuma dawa yote kwa nguvu kisha akaniachia na kusimama pembeni
 
“Nesi atapona kweli?”
“Ndio atapona wala usijali.Kwani huyu ni nani yako?”
“Mume wangu”
“Usijali mwaya mama ataponana tuu”
   Sikuweza kuendelea kuyasikiliza maongezi yao kwani usingizi mzito ukanipitia.Gafla nikamuona Olvia Hitler amesimama kwenye moja ya pembe ya chumba hichi huku akiwa ameachia tabasamu pana usoni mwake na kuufanya uso wake kuwa mmzuri kiasi kwamba ukaanza kunivutia.Olvia amevalia gauni zuri na lililo mbana mwilini mwake huku miguuni akiwa amevalia viatu vyekundu vilivyo kaa vizuri mguuni mwake.Akaninyooshea mkono na kujikuta nikaanza kunyanyuka taratibu kitandani huku nikielea hewani kama nilivyo elea jana usiku alipokuwa amejitokeza kwa mara ya kwanza.Nikazidi kushangaa kwani Mama Fety na wale manesi hawakuona jinsi ninavyo elea angani na wanaedelea na story zao za kawaida.
Olvia akanishika mkono na kunisogeza karibu yake kisha akanikumbatia kwa nguvu na sote tukajikuta tukianza kwenda juu kwa kasi huku bati la hospitalini hapo likiwa limeacha uwazi mkubwa wa tobo ulio turuhusu sisi kupita bila ya wasiwasi
 
“Eddy kuna sehemu nataka twende nikakuonyeshe maajabu ya ulimwenguni”
“Wapii”
“Utapaona”
“Ila leo Olvia umependeza sana”
“Asante”
“Hivyo viatu sijawahi kuviona tangu nizaliwe”
“Nitakupa kama zawadi ukampe Rahma”
“Kweli?”
“Ndio kwani si vitamtosha?”
“Ndio vitamtosha”
Olvia alizungumza huku tukienda kwa mwendo wa kasi angani ambapo kumetawaliwa na mwanga wa nyota kwani giza tayari lilisha tawala angani.Nikajikuta nikishangaa jinsi tunavyokwenda kwa mwendo wa haraka huku tukipita kwa kasi kwenye bahari
“Wewe si mwalimu?”
“Ndio”
“Unaijua hii iliyopo chini yetu ni bahari gani?”
“Hiyo sijui ni bahari gani”
“Hii ni bahari nyekundu”
 
“Kwa nini imeitwa bahari nyekundu?”
“Nenda kasome kwenye vitabu utajua”
  Kadri muda ulivyozidi kwenda nasi ndivyo tulivyo achana na giza na kukutana na mwanga wa jua ikimaanisha tupo katika nchi zinazo pishana masaa na Tanzania
“Hapa ni wapi?”
“Hapa ni bara la Amerika kaskazini”
“Ahaa ndio kuzuri ivi?”
“Ndio”
Tukatua kwenye gorofa refu kiasi kwamba ukitazama chini unaweza kuhisi kizungu zungu cha kuanguka
“Eddy hapa tupo Marekani na hili ni gorofa linaloitwa Twin Tower”
“Ahaa nililisikia sikia kipindi ninasoma kuwa lilipigwa Bomo na Osama Bi Laden mwaka 2002”
“Ndio…..Maana yangu kubwa ya mimi kukuleta huku ni wewe uweze kuwa miongoni mwa watu maarufu duniani?”
“Ina maana mimi na Tanzania ndio basi tena?”
“Hapana Tanzania utarudi  le oleo”
“Ahaaa”
   Nikazidi kuushangaa mji niliopo kwani unamagorofa mengi kiasi kwamba yamekuwa kivutio katika macho yangu na maisha yangu na sikutarajia kama ipo siku nitakuja kuiona Marekani kama ninavyo iona leo
 
“Olvia mimi nipo ndotoni au?”
‘Haupo ndotoni kwani huamini?”
“Ndio siamini”
Gafla Olvia akanisukuma gorofani na kuanza kwenda chini kwa kasi ya ajabu na kunifanya nianze kupiga kelele kali ya kuomba msaada huku mwenzangu akinipungia mkono wa kuniaga
“Eheeee nisaidieni”
Nikastukia nimekaa kitandani na kumfanya Mama Fety kunyanyuka alipo kaa kwa haraka na kuja kitandani nilipo kaa mimi huku nikihema kwa pumzi nyingi kiasi kwamba nikajihisi kupata kiu ya maji
“Eddy mpenzi wangu una tatizo gani?”
“Marekani?”
“Marekani…… Kuna nini?”
“Nimeenda Marekani”
“Dooo kweli mpenzi wangu umechanganyikiwa ni nini kimekupata jamani au ndio hiyo Maleria?”
“Hapana mimi nimekwenda Marekani unanibishia nini wakati nilikuwa kwenye gorofa refu TWIN TOWER”
“Mmmm mwenzio hata hilo Twin tower sijui ni linini?”
“Mshamba wewe”
Nikashuka kitandani na kuichomoa sindano ya dripu na kwenda kusimama kwenye kona ya chumba aliyokuwa amesimama Olvia na kuangalia juu na kukuta kumezibwa na ‘sinboard’ jeupe na hapakuwa na tobo lolote
 
“Ina maana mara moja hii pameziba?”
“Nini hiyo iliyo ziba?”
“Hapa palikuwa na tobo”
Ikambidi mama Fety aanze kucheka hadi machozi yakaanza kumwagika kwa kicheko anacho kicheka
“Eddy mpenzi wangu umechanganyikiwa kwa kweli ahaa kumbe una vituko kiasi hicho”
“Wewe huamini au ndio huo ushamba wako?”
“Sio siamini ila mmm….wewe ni kiboko,Mara hoooo nimekwenda Marekani mara hooo ni hapo kuna tobo”
“Wewe huamini nini….Ndio tatizo la watanzania wengi munakuwa hamuamini kama Tomaso?”
“Tomaso ndio nani?”
“Katazame kanda ya Yesu utamuona”
Mama Fety akazidi kucheka ikambidi afungue mlano na kuchungulia nje huku akiwaita manesi amabao baada ya muda wakaja na kunifanya nistuke baada ya kumuona mmoja wao akiwa amefanana na Olvia
 
“Jamani hiisindano tuliyo mchoma mgonjwa wako ni ya usingizi na mgonjwa akichomwa hulala kwa masaa nane sasa huyu hata masaa mawili bado?”
“Ngoja kwanza nesi….Unajua mimi si mgonjwa kama munavyo dhani nyinyi mimi ninanguvu zangu za kutosha sasa mimi ninaomba muniruhusu niondoke zangu”
“Wewe Eddy si unaumwa?”
“Nani anaumwa bwana hembu niacheni mimi niende zangu kwangu.kwanza ni saa ngapi?”
Nikaushika mkono wa nesi anaye fanana na Olvia na kuisoma saa yake ya mshale na kukuta ni saa Saba na dakika sita usiku
“Kwani saa saba hii nikitembea barabarani kuna kibaka atakaye nikaba?”
“Shosti hembu ngoja tuwasiliane na daktari mkuu kama kuna uwezekano mume wako asubuhi apelekwe Milembe hospitali ya watu wenye ulemavu wa akili basi tujue mapema”
“Alafu wewe nesi umevurugwa ehee nani amekuambia mimi sina akili.Mimi ni ticha wa Biology na Physics isitoshe Mathematics na Chemistry vyote ninafundisha.Sasa ninakusangaa unavyosema kuwa mimi sio mzima wa akili”
“Hii malaria itakuwa ni mbaya au amepata homa ya DENGUE?”
 
Nesi anaye fanana na Olvia alizungumza na kujikuta nikimtazama kwa hicho kali huku nikimchunguza kuanzai juu hadi chini na kukuta akiwa amevalia viatu vyekundu kama alivyokua maevaa Olvia kipindi amekuja kunichukua na tukaelekea Marekani
“Naomba basi hivyo viatu nikampelekee Rahma”
Nilizungumza huku nikimuangalia nesi anaye fanana na Olvia na wote wakashusha sura zao kuangalia viatu alivyo vivaa mwenzao kisha wakanitazama na mimi
“Wewe Eddy hivyo viatu unataka kuvipeleka wapi?”
“Nikampe Rahma huyu alisema atanipatia kipindi ninakwenda naye Marekani”
“Shosti mume wako sisi tumesha mshindwa yameshakuwa ya Marekani tena?”
“Wewe nesi mimi sijao na sina mke na safari ya Marekani muulize huyo mwenzako atakuambia”
“Mmmm jaman ihuyu mwanaume wangu sijui amapatwa na nini?”
 
“Hembu tunyamazeni jamani nataka kuwauliza maswali nyinyi manesi?”
Wote wakakaa kimya na kunitazama kwa umakini kisha nikakohoa kidogo na kuiweka suruali yangu isiyo na mkanda sijui waliuweka wapi mkanda wangu wa suruali
“Munaujua ugonjwa wa Dengue umemetokana na nini?”
“Si umetokana na Mbu anayeng’ata kuanzia asubuhi hadi jioni”
“Je dawa yake mumesha ipata au ndio munaacha watu wafe wafe kidogo ndio museme dawa imepatikana?”
Manesi wote wakaa kimya na kutazamana huku wakionekana hawana jibu la uhakika la kuweza kunipa
“Mwaka 1988 ugonjwa wa dengue ulijulikana katika nchi za Thailanda,Bamako,Veitinam na kwengineko katika bara la Asia.Ambapo ugojwa huo ulitokana na mazalio mengi ya mbu walio sababishwa na uwekaji mbovu wa mazingira hususani vita vya wenyewe kwa wenyewe”
 
“Ngoja kwanza kaka.Wewe umeyajuaje haya yote?”
“Ndio maana nikakuambia kuwa mimi ni mwalimu na ninaijua kazi yangu.Na nimesoma sana juu ya magojwa haya tuendelee…..Ungojwa wa dengue umekuja Tanzania kutokana na vimelea au mayai ya mbu hawa kuja kwa wingi kwa kutumia maji yanayo tiririka kupitia mto Naili unao ingiza maji yake katika ziwa Victori.Na baada ya Mafuriko yaliyo tokea juzi juzi Dar,Morogoro na kwengineko kumesababisha mayai ya mbu hawa kukua na kujitotolesha na kukapatikana hawa mbu ambao dawa yake ni moja tu inayoweza kuuzuia huu ungonjwa na sidhani kama munaijua?”
“Dawa gani?”
      
ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts