Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Tisa ( 19 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Tisa ( 19 )

Written By Bigie on Saturday, March 3, 2018 | 9:40:00 AM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

“Ndio maana nikakuambia kuwa mimi ni mwalimu na ninaijua kazi yangu.Na nimesoma sana juu ya magojwa haya tuendelee…..Ungojwa wa dengue umekuja Tanzania kutokana na vimelea au mayai ya mbu hawa kuja kwa wingi kwa kutumia maji yanayo tiririka kupitia mto Naili unao ingiza maji yake katika ziwa Victori.Na baada ya Mafuriko yaliyo tokea juzi juzi Dar,Morogoro na kwengineko kumesababisha mayai ya mbu hawa kukua na kujitotolesha na kukapatikana hawa mbu ambao dawa yake ni moja tu inayoweza kuuzuia huu ungonjwa na sidhani kama munaijua?”
“Dawa gani?”

ENDELEA
“Wewe kama wewe unahisi ni dawa gani?”
“Tukuulize wewe ambaye umesema unaijua dawa ya Dengue”
“Hivi kweli wewe umesoma masomo ya Sayansi au huo unesi umeupata baada ya kufeli form four”
Swali langu likawafanya manesi kukaa kimya huku wakinitazama wasijue cha kunijibu
“Kwa akili za kawaida mtu akiwaona nyinyi manesi wawili atajua kabisa mumeishia kidato cha nne na hamkuwa mukiyasoma masomo ya Sayansi……Na mumefeli mukaamua kuja kusomea unesi.Uongo au kweli?”
Manesi wote wakakaa kimya huku wakinitazama kwa macho ya aibu aibu
 
“Kabla sijaendelea na na mada yangu hivi munamjua mtu anaye paswa kwenda Mirembe munapo sema?”
“Eddy baby wewe itakuwa ni malaria imekuchanganya mpenzi wangu”
“Na wewe koma malaria haiwezi kunichanganya……Hawa manesi wenu wamenidhalilisha wakiniambia mimi sina akili vizuri na hata kama ni Malaria sijawahi siku hata moja sijawahi kupatwa na ugonjwa wa kupungukiwa na akili………Musinitumbulie mimacho yenu kama mumebwana na mlango”
“Shosti kuna mgonjwa wodi ya watoto ngoja nikamuangalie”
Nesi anayefanana na Olivia Hitler alizungumza na akaanza kupiga hatua za kuuelekea mlangoni,nikamuwahi na kumshikamkono
 
“Hembu rudi pale kwa mwenzako huna cha mgonjwa wala cha nini kaa unisikilize”
Nesi akarudi na wote watatu wakakaa kitandani wakinisikiliza huku nesi niliye mrudisha akionekana kutetemeka kwa woga
“Atakayetoka kabla sijamaliza somo langu nitampiga boooonge la kofi mtapisho”
“Shosti unaona shunguli ya mume wako anavyo tufanyia?”
“Masikini Eddy wangu sijui amepatwa na nini?
“Nyamazeni……Dengue kama dengue dawa yake ni rahisi sana….Kwanza mtu ambaye hajapatwa na ugonjwa huu inabidi aanze kumrudia Mungu wake mapema kwa maana asisubirie ameupata ndio anakumbuka kumuomba Mungu.Pili munatakiwa kuua mazalio yote ya Mbu kama madimbwi kufyeka nyasi ndefu zilizopo karibu na makazi ya watu au kufunika vitu vyote ambavyo munajua vinaweza kuweka maji yakasimama kwa muda mrefu kama vile vifuu na kadhaliaka”
 
“Mmmmm kubwa hayo hadi vifuu vipo kwenye somo”
Mama Fety alazingumza huku akinitazama kisha akawageukia wezake ambao wapo kimya wakionekana kunifwatiliwa kwa umakini somo langu
“Ujinga wako ndio utakufanya ufe na dengue ninakuambia muvichome vifuu vyenu wewe unaropoka ropoka maswala ya ajabu…….Sasa tuje kwenye dawa halisi ya kutibu ugonjwa huu…..Unapaswa kunywa maji mengi ambayo yataweza kuchuja sumu iliyo jaa mwilini mwako ikiwemo bacteria wa ugonjwa huu wanao itwa ARBOVIRUS ambao watatoka kwa njia ya haja ndogo au kutokwa na jasho mwilini”
“Mwalimu nina swali?”
“Uliza”
“Hao bacteria wanaingia ingia vipi mwlinini mwa binadamu?”
“Ndio maana nikasema nyinyi manesi munaonekana hamjasoma kabisa masomo ya sayansi.Hapa si tunazungumzia huyu mbu anaye itwa AEDES ndio msambazaji wa hawa bacteria wanaosababisha Dengue sasa usicho kielewa wewe ni nini?”
 
“Huu ugonjwa ni mpya kwetu  ndio maana nikakuuliza hivyo ila samahani kama nimekuudhi ticha wetu”
“Umesoma chuo gani cha unesi?”
“Mmmm wewe endelea tu mwaya huyu achana naye”
“Muna kipimo cha  PCR?”
“Ndio tunacho”
“Nionyesheni”
Manesi wakasimama kutoka kitandani na tukatoka nje ya chumba tulicho kuwepo na tukamuacha mama Fety akitusubiria.Tukaingia kwenye maabara ya hospitali hiyo.
“Nahitaji damu za kila mmoja wenu nizipime?”
“Kupimana tena?”
“Kama hamtaki semeni?”
“Hicho kifaa ni kipya sisi wala hatujafundishwa kukitumia”
“Nyinyi jitoboneni na munipe damu zenu niwapime……Na wewe ndenda kamuite mwenzenu kule”
 
Nesi mmoja akatoka na kumuacha mwenzake akijichoma sindano ya ndogo ya kutolea damu kisha akaipaka kwenye kiio maalumu ambacho hutumika kupakia damu zinazo tolewa kwenye vidole mara nyini hutumika  kwa wagonjwa wanao pima ugonjwa wa Malaria.Akanipa na kukiweka kwenye kipimo hicho na kuanza kusikilizia majibu.
“Huna bakteri”
Mama Fety akaingia akiwa ameongozana na nesi aliye kwenda kumuita,wakatoa damu zao na nikaanza kuzipima moja baada ya nyingine na kujikuta nikimtazama nesi anayefanana na Olvia kisha nikahamisha macho yangu kwa mama Fety
“Kati yanu mmoja anavirusi vya Dengue”
Mama Fety na nesi wakabaki wakinitazama huku wakiwa na wasiwasi kiasi kwamba kila mmoja wao akaanza kumwagikwa na jasho
“Si useme sasa ni nani mwenye Dengue?”
Mama Fety alizungumza huku akijifuta jasho kwa kutumia tenge lake huku kwa mbali machozi yakimlenga lenga.
 
“Jamani wapendwa zangu kupatwa na Dengue sio mwisho wa maisha unaweza ukanywa Parasetam na ukapona”
“Sasa Eddy zungumza basi ni nani mwenye dengue”
Mama Fety akazidi kunihimmiza huku machozi yakianza kumwagika na kumfanya nesi anaye fanana na Olvia kuanza kulia
“Sasa nyinyi kiancho waliza ni nini?”
“Eddy sema basii nani mwenye dengue?”
“Hembu totokeni huku nje”
Tukatoka kwenye chumba cha maabara na wakakaa kwenye moja ya benchi lililopo njee ya chumba hicho na huku wakinisubiria nizungumze.Nitakazama mlango wa kutokea nje na kuukuta upo wazi.
“Sasa nisikilizeni kwa umakini…….Poleni sana kwa kulia kwani nimoja ya maisha ila ukweli ni kwamba HAKUNA MWENYE DENGUE”
Nikachomoka kwa kasi kuelekea nje huku nikiwaacha Mama Fety na wezake wakinipormoshea matusi ya nguoni.Nikaendelea kukimbia hadi kwenye moja ya kituo cha taksi na kukuta gari mbili za za kukodi,nikaingia kwenye moja huku nikihema kwa kuchoka hadi dereva taksi akaanza kunishangaa
“Kaka nipeleke Raskazoni”
“Sawa elfu thelathini na tano”
“Powa hata ukitaka hamsini nitakupa”
“Ila ni Raskazoni sehemu gani kwa maana huu ni usiku mwingi kaka”
 
“Kule karibu na kwenye nyumba ya mkuuwa wilaya”
“Basi utafanya hiyo elfu hamsini”
“Powa kaka”
Safari ikaanza huku miguuni nikiwa peku na kila safari ikiendelea nikamuona dereva taksi akinitazama kwa macho ya kunichunguza  kuanzi chini hadi juu
“Kaka mbona unaniangalia sana?”
“Hapana kaka”
“Au unashangaa mimi kuwa peku?”
“Ndio sijui umekumbwa na majanga gani?”
“Wee acha tu ndugu yangu”
Tukafika getini kwangu nikashuka na kumuomba dereva taksi anisubirie kwa dakika kadhaa nikamchukulie pesa ndani.Nikagonga geti kwa muda kisha Hilda akafungua huku akionekana kutoka usingizini
“Eddy saa hizi unatoka wapi?”
“Hembu niache na wewe”
Nikapimga Hilda kikumbo getini alipo simama na kuingia ndani nikapitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwangu nikafungua kabati la nguo na kutoa kiasi cha pesa anacho kihitaji dereva na kutoka nje nikapishana na Hilda kwenye mlango wa kuingilia ndani ikamlazimu kunishika mkono
“Eddy mbona sikuelewi?”
“Hunielewi nini?”
“Umerudi upo shakala baghala viatu huna,nguo zimejikunja kunja?”
 
“Hembu niachie kwanza nimlipe jamaa wa watu kisha ndio tuzungumze”
Nikatoka nje ya geti na kumlipa dereva taksi kisha nikarudi ndani na kumkuta Halda akiwa amesimama sebeleni akionekana kuwa na hasira
“Haya niambie kilicho kupata huko utokapo ni nini na kurudi saa hizi usiku?”
“Hembu niandalie chakula kwanza nile nipate nguvu ya kuzungumza “
“Sawa chakula kipo pale mezani ila nahitaji kujua ni kwanini unarudi saa hizi?”
“Uaniuliza hivyo wewe kama nani kwa maana sikuelewi?”
“Sio unielewi nina haki ya kukuuliza mimi kama mpenzi wako na shemeji yako”
Halda alizungumza kwa hasira huku akinijishika kiuno na kama wanavyofanaya wanawake wengine wanapokuwa na hasira akaazna kunipandisha na kunishuka
“Wewe mwanamke wewee usitake nifanye kitu amabacho sijatarajia kukifanya kwa wakati huu”
“Nipige uone”
“Halda nitakuvuruga”
“Utanivuriga……..Jaribuuu.Umetoka kulala kwa Malaya zako huko unanirudia usiku kumbe wewe ni Malaya kiasi hicho”
“HILDA HEMBU NIACHE SITAKI MATATIZO NA WEWE”
“Utanieleza umetoka kulala kwa nani?”
“Kulala na mbu wa dengue”
“Eddy usiniletee dharau wewe mwanaume unajua nitamwambia kila kitu Rahma unacho kifanya”
“Ole waku siku ufungue domo lako utanijua kuwa mimi ni nani”
 
“NITASEMA”
“SEMA UONE NITAKACHO KIFANYA”
“Nyoo umetoka kufumaniwa huko hata viatu umeviacha utakuja kufa wewe mwanaume maradhi mengi”
“Nikifa si mimi wewe inakuhusu nini?”
“Liangalie lile bichwa lake kama bomu la nyuklia”
Sikutaka kuendelea kumsikilaza Halda maneno yake kwani nikiendelea kuyasikiliaza yatazidi kunichefua roho yangu na siku nzima imekuwa mbaya kwangu tangu asubuhi.Nikavuta kiti cha meza ya kukaa nikakaa na kuanza kula chakula alicho nipikia Hilda ambacho kusema kweli ni kitamu tofauti na vyakula nilivyo wahi kula kwenye maisha yangu
“Chalula chako kitamu”
“Nyooo kamwambie huyo Malaya wako uliyetoka kufumaniwa naye ndio akupikie chakula kitamu”
“Hilda mbona umekuwa jeuri siku hizi jua kuwa penzi lako kwangu ni lamkataba muda wowote  linaweza kusitishwa kama mkataba wa David Moyes”
“WEWE NILETEE USENG* WAKO”
“Unasemaje wewe mwanamke?”
“Habari ndio hiyo wewe mseng* kama waseng* wengine”
   Nikanyanyuka kwenye kiti kwa hasira na nikapiga hatua za haraka kumfwata Hilda sehemu aliyo simama  na akaanza kukimbia kuelekea ndani kwangu huku na mimi nikimkimbiza kwa nyuma na kabla hajashika kitasa cha mlango wa kuingilia chumbani kwangu akakanyaga maji yaliyopo juu tarzi na gafla akateleza na kuanguka kwa kwa nyuma na kichwa chake kikapiga chini kwa nyuma na damu zikaanza kusambambaa taratibu kutoka sehemu kilipo angukia kichwa cha Hilda na kuufanya mwili wangu kuanza kutetemeka kwa woga

 ITAENDELEA


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts