Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Moja ( 31 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Moja ( 31 )

Written By Bigie on Thursday, March 15, 2018 | 4:34:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Wakaanza kupigana na ikamlazimu mwenye kipande cha bangi mdomoni kukitema pembeni huku kikiendelea kuwaka na kikaangukia kwenye mafuta ya pretroli yanayotoka kwenye tanki lililo pasuka la gari aina ya Scani ambayo yamesambakaa barabarani na ndani ya dakika mlipuko mkubwa ukatokea na kusababisha idadi kubwa ya watu wanao gombania viroba vya unga na vindoo vya mafuta kurushwa mbali na wengine kupoteza maisha

ENDELEA
Moshi mwangi na harufu kali ya moshi wa mafuta aina ya Petrol ikatawala katika eneo zima la eneo rulilopo huku vilio vikianza kutwala kwa wale walio wapoteza ndugu zao kwenye ajali ya moto.Ikanilazimu kumsogeza madam Zena pembeni zaidi ili kuepuka kuunguo kwa moto unaosambaa kwenye hili eneo kwa kupitia upepo mkali.Gari za Polisi mbili zikafika katika eneo la tukio na sikujua ni nani aliye wataarifu na baada ya muda gari za zima moto na gai ya wagonjwa ikafika katika sehemu ya tukio na kuanza kupakiza baadhi ya wagojwa mahututi ikiwemo madam Zena na wakawahishwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga iitwayo Bombo.

 Msongamano wa magari mengi yaliyo simama kutokana na ajali ikazidi kuongezeka na kusababisha msongamano mkubwa wa magari mengi yanayotoka mkoani na yanayokwenda mkoani.Maiti za wanakijiji walio ungua katika mlipuko zikaanza kukusanywa eneo moja na nikajikuta nikitafuta sehemu nikisimama kutokana na kushindwa kuiangalia miili ya watu wengine kwa maana imeharibika kiasi kwamba inatisha.Hadi inafika saa tatu usiku magari yakaanza kuruhusiwa kuendelea na safari baada ya magari yaliyo pata ajali kusogezwa barabarani.
 
Nikarudi kijijini na kukuta nyumba nyingi zikiwa zimetawaliwa na vilio kiasi kwamba hata raha ya viroba vya unga na vindoo vya mafuta ya kupikia ikawa imetoweka miongoni mwa wanakijiji wengi,Kutokana sikuwa mwenyeji kwenye kijiji hichi mojo kwa moja nikafikizia kwa bibi aliye nihudumia kipindi nikiwa nimeokotwa porini,akanipatia chakula nikala na kwenda kuoga kasha nikarudi ndani na kumkuta akichanganya changanya dawa zake kama kawaida
 
“Unajisikiaje sasa mjukuu wangu?”
“Kdogo afadhali bibi yangu”
“Mshukuru Mungu kwa yale yote yaliyo tokea na ameweza kukuokoa hadi ukafikia kuwa na hali kama hiyo”
“Ni kweli bibi na vipi mbona hauendi kwenye misiba?”
“Mbona hiyo sio misiba mjukuu wangu”
“Sio misiba kivipi bibi?”
“Mjukuu wangu kwenye ulimwengu huu kuna mambo mengi sana ambayo wanadamu huwa tunayapitia na kuyafanya,Yakiwemo mazuri na mabaya”
“Ni kweli bibi ila sijakuelewa ni kwanini umesema kuwa sio misiba?”
“Watu hao hawajafa kilicho tokea kwenye hiyo ajali ni kiini macho tu ila watu wanao sadikika kufa kwenye hiyo ajali wote wapo hai”
Nikajihisi kama mwili ukiwa umesizi kidogo huku nikifikiria cha kumuuliza bibi kwa maana ninacho kisikia hapa ni kama vile nipo ndotoni vile na ikanilazimu kuamini ninacho ambiwa hapa ni kweli na wala sio ndoto
 
“Kwa nini bibi?”
“Kwa malezo zaidi nitakufwata usiku nikakuonyesha hao watu sehemu walipo”
“Usiku kivipi?”
Bibi akanyanyuka na kuingia ndani kwake na kuniacha na alama ya kuuliza huku mapigo ya moyo yakiaanza kunienda mbio hata hamu ya kulala ikaanza kunitoweka.Nikatoka nje kwa kunyata na nikafanikiwa na kukuta bado wenye misiba wakiendelea kupiga makalee ya kuomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.Nikaanza kutembea kuelekea barabarani na kukuta  na watu wengine wakiendelea kusafisha safisha barabara huku gari aina ya Rosa iliyo pata ajali ilinyanyuliwa na gari maalumu lenye winchi na kuwekwa barabarani
“Kaka hili gai lenu munalipeleka wapi?”
Nilimuuliza mmoja wa wafanyakazi walio kuwa wakijishuhulisha na jinsi ya kuinyanyua gari hii ya abiria
“Tanga mjini”
“Samahani kaka sijui ninaweza kupata japo kanafasi ka kujishikiza na hadi huku munapo elekea?”
“Kwani wewe unakwenda wapi?”
“Mimi ninakwenda Tanga mjini?”
“Sasa huku ilikuwaje ukaja?”
 
“Niliacha na basi niliingia porini kuchimba dawa kurudi ninakuta basi nililo lipanda likiwa halipo”
“Powa ngoja nizungumze na suka”
Sikuwa na ujanja ilinibidi kudaganya kwa maana pasipo kufanya hivyo ingekula kwangu na jamaa niliye zungumza naye akazungumza na dereva wake kasha akaniita na sote tukaingia kwenye gari lao kubwa na safari ikaanza huku ililivuta gari la abaria lililo pata ajali.Japo bibi amenisadia ila kusema kweli alivyo niambia atakuja usiku kunichukua nikapoteza amani kabisa ya kukaa nyumbani kwake.Ndani ya lisaa na nusu tukafika Tanga mjini na mimi wakanishusha maeneo ya Reilway na nikawashukuru na jamaa wakaelekea barabara ya sita anapoishi mmiliki wa gari hiyo.Nikakodi bodaboda japo mfukoni sina hata senti moja ikanipeleka hadi nyumbani kwangu.Sikuwa na woga kutokana ninahisi kuwa baba Rahma anaamini kwa wakati huu nitakuwa ni maiti.Nikalikuta geti la nyumbani kwangu likiwa limerudishiwa na moja kwa moja nikaingia ndani kwangu huku nyumba yangu nikiwa nimeichungaza vya kutosha
 
Nikaaza kutafuta kikadi changu cha benki na kwa bahati nzuri nikiwa ninakagua kwenye mifuko yangu ya suruali nikakuta noti mbili za elfu tano tano kwenye suruali yangu ya jinzi,nikatoka nje na kumlipa boda boda na kufunga geti langu na kurudi ndani na moja kwa moja nikajitupa kitandani na kutokana na uchovu mwingi usingizi mwingi ukanipitia.
Nikaanza kuhisi hali ngumu kila nilipojaibu kuvuta pumzi nikajikuta nikishindwa kiasi kwamba nikaanza kutumia nguvu nyingi katika kupambana na kitu kilicho nikaba kooni ambacho sikioni na kadri muda ulivyo zidi kwenda nikajikuta ninazidi kukabwa,Gafla bibi akasimama pembani ya kitanda changu huku akiwa amevalia kaniaki nyeusi huku mkononi mwake akiwa ameshika unyonya wa simba pamoja na kijikibuyu kidogo
 
“Eddy mbona ulinikimbia pasipo kuniaga?”
Nikashindwa kumjibu na kila nilipo mtazama sauti yangu haikuweza kunitoka kaisa nikabaki nikiwa nimemtazama
“Basi nimekuja kuitimiza ahadi yangu ya kuja kukuchukua”
Mwili mzima ukaanza kumwagikwa na jasho na katika siku amazo nimepatikana hii kwangu leo nimepatikana tena kwa asilimia kubwa na sikuona dhamani yoyote ya pete niliyo ivaa kunisadia,Akaunyosha mkono wake mmoja na kujikuta nikinyanyuka kitandani na pasipo kupenda.Akaniamrisha kuzunguka kwa kutumia kidole chake kimoja cha mkono wa kulia na kujikuta nikizunguka zaidi ya mara saba kisha akanishika mkono na tukapiga hatua hadi kwenye kona ya chumba changu na kujistukia tukipita bila wasiwasi na tulipo tokea si nje kwangu bali kuliwa makaburini na nikakuta kuna chungu kikubwa kilicho zungukwa na watu walio uchi wakiwemo wakubwa na wazee,wanawake na wanaume.Bibi akanipaka unga kwenye uso wangu na kuniambia kuwa watu hao itakuwa ni ngumu wao kuniona
 
Tukapita kati kati yao huku nikijitahidi kuchungulia kwenye chungu kikubwa walicho kizungukana sikuona ni kitu gani wanacho kichemsha,Tukasimama pembeni kwenye kaburi lililopo kwenye eneo ilo kisha tukaanza kushuhudia wale watu walio fariki kwenye ajali wakipita mmoja baada ya mwengine huku wakiwa wamepanga mstari mmoja kama wanajeshi walio tekwa huku mikono yao wakiwa wameinyoosha juu na moja kwa moja wakaenda mpaka kwenye moja ya kaburi lililo wazi na wakaanza kusukumwa na Yule mzee ambaya jamaa aliniambia kuwa ni mchawi kikongwe na karibia watu thelathini na saba wakadumbukia ndani ya shimo moja kisha wale wachawi wali zunguka chungu wakasimama na kuanza kucheza ngoma iliyo tibua vumbi jingi kiasi kwama hata sikuweza kuwaona vizuri
“Bibi pale wanafanyaje?”
“Mjukuu wangu pale wanasherekea kuwa wamewapata vibarua wapya”
“Vibarua vipya kivipi?”
 
“Ni wafanyakazi wapya wa kuwalimia kwenye mashamba yao na kuwafanyia kazi nyingine za utapeli kama kukopera”
“Kukopera ndio nini?”
“Kukopera ni ile hali kwamba mtu anakuja na kiasi kidogo cha pesa ila anapo kupa pesa yake na ukazichanganya na pesa zako kwa mfano dukani basi kuna misukule yao huwa wanaituma na kuja kuzichukua pesa karibia zote ikiwemo na ile pesa ambayo wamekupatia na huwa wakati wanazichukua huwaoni”
Nikabaki kimya nikiwa ninashangaa jinsi wanavyo tolewa mmoja mmoja kwenye shimo na kunyweshwa kitu kilicho kuwa kikichemshwa kwenye chungu a kila aliaye nywesha alionekana kupata shida sana japo sauti zao zilitoka mara moja tuu
“Ndio wananyweshwa nini pale?”
“Ile ni dawa inayo wakata kauli”
“Inayo wakata kauli kivipi?”
“Inayo wafanya washindwe kuzungumza kabisa na hata wakikutana na watu wana wajua hawawezi kuzungumza kitu cha aina yoyote”
“Bibi mimi nilisikia kwamba wanakatwaga ulimi?”
“Ndio walikuwa wakikatwa ulimi ila mambo yanabadilika kwani kwenye ulimwengu wa kawaida kuna mfumo wa kidigital basi hata katika ulimwengu wa wachawi kuna udigital kama wenu”
 
Nikatamani kucheka ila nikajikuta nikiwa nimeuziba mdomo wangu kwa kutumia kijanja changu,Shuhuli ikaendelea na bibi akaniomba kunirudisha nyumbani kwangu na kutokana kumekaribia kupambazaku.Tukafika nyumbani kwangu na bibi akatoa kichupa kidogo kwenye kiuno chake na kunikabidhi
“Humo ndani kuna mafuta ambayo ukijipaka usoni mara tatu hata ukitembea mtu hawezi kukuona”
“Nikijipaka kwa mtindo gani?”
“Jipake vidoti vitatu kwenye paji la uso kidoti kimoja kwenye kila shavu utajipaka mara moja moja”
“Sawa bibi nimekuelewa”
Kama tulivyo toka mara ya kwanza ndivyo bibi alivyo toka kwenye chumba changu na kutokana na uchovu mwingi nikajitupa kitandani na kulala.Mida ya saa tano asubuhi nikaamka huku mwili ukiwa umechoka sana kiasi kwamba nikabaki nikiwa ninajifikiria jinsi ya kuamka kitandani,nikakitazama kichupa alicho nip bibi jana usiku na kujikuta nikiachia tabasamu kubwa sana huku nikijifariji moyoni mwangu
 
“Kitanisaidia kumrudisha Rahma kwenye himaya yangu”
Nikanyanyuka kwa furaha huku nikicheka cheka na nikaingia afuni kwangu nikaoga na kurudi tena kitandani kwangu na kujifuta maji vizuri na kuvaa pensi kisha nikaingia jikoni kwangu na kukuta ile hali ya maunga niliyo jimwagia siku nikiwatoroka wazazi wa Rahma ikiwa vile vile.Nikaanza kufanya usafi na ndani ya dakika kumi na tano mazingia ya ndani kwangu yakawa yamekaa safi.Nikajipikia uji na kunywa ili kuuweka mwili wangu vizuri kisha nikarudi chumbani na kuchukua kichupa changu chenye dawa na nikajipaka kama alivyo niambia bibi na nikatoka nyumbani kwangu na kuanza kutembea barabarani kwa majaribia
 
Kusema kweli hapa ndipo nikaanza kuamini kuwa uchawi upo na unafanya kazi kwani kila nilipokuwa ninapapita ikawa ni ngumu sana kwa watu kuniona na hata baadhi ya watu ninao wajua nilipo pita karibu yao hawakuweza kustuka wala kuniona.Nikapata wazo na nikalifanyia kazi mara moja na sikutaka kulilazia damu.Moja kwa moja nikachapusha miguu yangu hadi kwenye jumba la kina Rahma na kukuta geti lao liliwa wazi na kuna gari moja imesimama katikati ya geti ikijiandaa kutoka,Dereva wa gari hii sikumjua kwani ni kijana mdogo wa kiarabu na anazungumza na mwanamke mwengine ambaye analifwata gari lilipo akitokea ndani
 
Nikapishana nao na kuzidi kushangaa kwani hawakuweza kuniona,Nikafiaka mlangoni na kutizama huku na kule na sikuona mtu na kwa tahadhari kubwa nikashika kitasa cha mlango na  kuufungua kisha nikaingia sebleni na kukakuta kazee kale kaliko kuja sehemu niliyo tekwa kakiwa kameshika tama huku mkononi akiwa na picha kubwa iliyo tengenezwa kwenye jifremu kubwaa na ikionyesha sura ya yule mzee mwenzake aliye zikwa akiwa hai,Nikasimama karibu yake na hakuweza kuniona na kila nilipo mpitishia kiganja mbele yake wala hakuweza kustuka.Mlango ukafunguliwa na akaingia baba Rahma akiwa ameongozana na daktari wa kiarabu na wakasalimiana na babu aliye shika piacha
 
”Mumefika wapi juu ya mdogo wangu aliye potea?”
“Bado tunaendelea kumtafuta ila tutampata”
“Bada usiniambie kwamba utampata nakupa siku yaleo nataka kumuona mdogo wagu”
“Lakini baba unavyo niambia mimi hivyo ni kana kwamba mimi ndio niliye mpoteza”
“Haswaaaa wewe ndio umempoteza mdogo wangu ingekuwa sio hilo jiroho lako baya wala haya matatizo yasinge fikia huku kwa maana mimi nilisema muacheni mtoto wa watu nyinyi mukaniona mimi mjinga umeona sasa hayo yote yamehamia kwa mwanao hapo alipo lala hajielewi wala kujitambua”
“Lakini baba hayo yote yametokea wapi?”
“Sitaki ujinga nasema namtaka mdogo wangu hapa leo la sivyo nitakuachia laana na wewe ukawehuke kama weu wezako”
 
Mzee alizungumza kwa uchungu huku machozi yakimwagika kiasi kwamba nikabaki nikiwa ninamuonea huruma na laity angejua kuwa mdogo wake amezikwa kikatili kiasi kile nahisi angejaza machozi sehemu nzima aliyo kaa.Baba Rahma akaanza kupandisha ngazi za gorofani huku akiwa yupo na daktari na mimi nikaanza kuwafwata kwa nyuma na sote tukafika kwenye moja ya chumba na baba Rahma akaufungua mlango na akaanza kuingia ndani  na ikanibidi nimpige kikumbo daktari na nikawa wa pili kuingia
“Vipi dokta mbona unayumba?”
“Ahaa nimejikwaa hapa”
“Pole sana”
Nikamkuta Rahma akiwa amelala kwenye kitanda kikubwa cha sita kwa sita huku pembeni kukiwa na mashine za kupumulia pamoja na mtungi mkubwa wa gesi,Macho yake bado hayakuwa na nguvu ya kufumbuka na wala hakuweza kujitingisha na yupo sawa na mfu aliye hai kwani kuhema kwake kwa mbali kuliidhihirisha kuwa hali yake sio mzuri kabisaa.Daktari akaanza kumtazama tazama na kumpima pima kisha akamgeukia baba Rahma
 
“Hali yake kusema kweli bado ni mbaya”
“Sasa tutafanya nini dokta?”
“Kama nilivyo kushauri ni vyema ukampelea katika hospitali kubwa ili akapatiwe matibabu zaidi ya haya tunato mpa hapa nyumbani”
“Sawa dokta hilo nimekuelewa ila woga wangu unakuja hapa endapo madaktari watataka kujua kuwa ni nini kilicho mpa je itakuwaje?”
“Hilo ni swala la kuwahonga wao wasihitaji udhibitisho kutoka polisi wewe unapesa hembu tumi hizo pesa zako katika kuyaokoa maisha ya mwanao na usipo angali utampoteza kiurahisi”
“Sawa nimekuelewa ila…….Mmmmm”
“Mbona unaguna?”
“Nina mtihani kama ulivyo kuwa ukimsikia baba pale akifoka foka akimuhitaji mdogo wake”
“Kwani huyo mdogo wake ni mtoto?”
“Ni mtoto wapi wakati ni mtu mzima kabisa na mimi ninamuita baba kabisa anakaribia miaka 60”
“Duu sasa atapoteaje…..?”
Kabla hakazungumza chochote akaingia shangazi wa Rahma ambaye anajifanya ni mganaga na wote tukamgeukia kisha mimi nikapiga hatua za haraka hadi nyuma ya mlango na kujibanza,
“Vipi mbona unahema juu juu kuna nini?”
“Ngojeni kwanza”
 
Akaanza kunusa nusa ndani ya chumba huku akizunguka zunguka na akaipiga hatua hadi sehemu niliyo simama na akaiangalia sehemu niliyopo kwa muda huku macho yake akiwa ameyatoa kiasi kwamba nikahisi ananiona ila nikaendelea kujikausha kimya na nikawa nipo tayari kwa lolote na kama ataniletea shida ya aina yoyote nitamtandika ngumi kali itakayo mpotezea hata uwezo wa kunusa nusa.Nikajianda kuivuta ngumi na kabla sijaiachia akawageukia baba Rahma na daktari
“Kaka kuna askari wamekuja na wapo sebleni na huyo baba usipo angalia ataanza kuzungumza hata mambo yasiyo husiana na atakacho ulizwa”
“Wee wapo wangapi?”
“Wapo wanne  wewe nenda kazungumze nao”
“Ohhh Mungu wangu”
Baba Rahma akaanza kubabaika kiasi kwama nikaanza kumuona akitetemeka akatoka huku akiwafwatiwa na shangazi wa Rahma na wakamuacha daktari akiwa anamtazama tazama Rahma,Simu ya daktari ikaanza kuita  na kumfanya afungue mlango na kutoka ndani ya chumba na kwenda kuzungumza na simu nje.Kwa haraka nikapiga hatua hadi kitandani mwa Rahma na kumshika kifuani na kuyasikilizia mapigo yake ya moyo jinsi yanavyo na nikaanza kumuita
 
“Rahma……Rahma……Rahma”
Nilimuita huku mdomo wangu ukiwa upo karibu sana na sikio lake ila hakuweza kunisikia,Nikaelekea hadi mlangoni na kufungu mlango na kumuona daktari akishuka kwenye ngazi na nikachungulia kwa chini walipo kaa askari na wazazi wa Rahma na kuwaona wapo kimya huku wakisubiria swali la  askari mmoja kujibiwa,Nikarudi ndani na nikahisi  Rahma hanisikii kutokana na dawa niliyo jipaka,nikaingia kwenye bafu lililopo ndani ya hichi chumba na kunawa uso kisha nikarudi kitandani kwake na kuanza kumuita karibu na lilipo sikio lake na nikarudia mara kadhaa na kumuona akiiunyanyua mkono wake mmoja wa kushoto huku akiyafumbua fumbua macho yake na nikazisikia sauti za watu wakija karibia na mlango na kunifanya nikimbilie bafuni na nikajifuta maji usoni na kukitoa kichupa cha dawa na kujipaka usoni na kusubiri kwa muda
 
Nikamuona Hilda akiingia bafuni na kwa haraka akaanza kuzishusha nguo zake na kujisaidia haja ndogo na akageuka sehemu niliyo mimi na akaupitisha mkono wake katikati ya miguu yangu na kuchana kipande kaidogo cha toilet paper na kujifuta sehemu zake za siri kisha akajiweka sawa na kutoka na nikaamini hajaniona.Nikapiga hatua hadi chumbani na kumkuta Rahma akifumbua fumba mdomo wake huku akiliita jina langu na kumfanya Hilda na msichana mwengine niluye muona wakibaki wakishangaa huku sura zao zikiwa zimejaa tabasamu.Hilda akanyanyuka kwa haraka akaungua mlango na kusikia sauti akimuita baba Rahma na baada ya muda wakaingia wazazi wa Rahma wakiwa na polisi na Rahma alipo muona baba yake akaanza kuatokwa na machozi
 
Watu wote ndani ya chumba hawakuweza kuniona kiasi kwamba nikazidi kujiamini uendelea kukaa ndani ya hichi chumba
“Baba”
Rahma aliita kwa sauti ya upole na yaunyenyekevu
“Naam wamwanangu”
“Yupo wapi Eddy wangu?”
Swali la Rahma likawafanya watu wote kutazamana na kukaa kimya pasipo kujibu kitu cha aina yoyote
“Huyo Eddy ni nani?”
Askari mmoja aliiuliza huku akionekana ni mkubwa kwa cheo hii ni kutokana na mavazi yake aliyo yavaa kutawaliwa na vyeo vingi vya kijeshi na kuwafanya ndugu wa Rahma pamoja na wazazi wake kutazamana tazama pasipo kuwa jibu.Gafla nikastukia shangazi wa Rahma akinishika mkono huku akinikonyeza akiashiria nijikaushe kama nilivyo na akatoa simu yake mfukoni na kuandika baadhi ya maneno na kuiweka mbele yangu na nikayasoma
 
{NIMEKUONA MIMI PEKE YANGU JIKAUSHE HILI SWALA LIPITE NDIO TUTAJUA MIMI NA WEWE}
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbioa kiasi kwamba nikahisi nimeingia tena mikononi mwa familia hii makatili
“Wee mama hembu hiyo simu yako”
Askari mmoja akaichukua simu ya shangazi wa Rahma na kuusoma ujumbe kwa sauti ya kichini chini.
“Huyo uliye muona ni nina?”
Watu wote wakamgeukia shangazi wa Rahama na akaniachia mkono kwa haraka na kutingisha kichwa akimaanisha kuwa hukuna kitu
“ILA BABA KWANINI UMUUE EDDY WANGU?”
Swali la Rahma likawafanya watu wote kumtazama na nikaanza kuziona sura za askari zikianza kubadilika na kuweka mikunjo askari wawili wakaziweka bunduki zao sawa kuzielekeza kwa baba Rahma  huku mkuu wao akipiga hatua hadi kitandani na kumuuliza Rahma swali
“Unasema kuwa Eddy ameuliwa na baba yako?”
‘NDIO”
 
 ITAENDELEA
Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts