Get the latest updates from us for free

Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Nane ( 38 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Nane ( 38 )

Written By Bigie on Friday, March 23, 2018 | 11:07:00 AM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Jini la kiume ambalo ninaongea naye akaniishika mikono na gafla kufumba na kufumbua nikajikuta nikiwa katika anga na sikuamini macho yangu baada ya kuukuta mji mzima wa Tanga ukiwa umetawaliwa na damu nyingi lizilizo tapakaa maeneo mbalimbali ikiashiria watu wengi wametafunwa na majini yangu.
 
ENDELEA
Nikabaki nikihamaki kwani hali ilizidi kuwa mbaya,watu walikimbizama hovyo kuyaokoa maisha yao.Jini aliye nishika akanishusha juu ya gorofa moja la bandari.Kwa kutumia uwezo wa fimbo nilio nao nikaamaru majini wote kutulia,Wakatutii kwani maamlaka niliyo nayo juu yao yamezidi kuongezeka.Wakalizunguka eneo ambalo mimi nipo wakisubiri nini nifanye.
“Nani aliye waamuru kufanya huu upuuzi wakati niliwaachia kwa roo njema?”
Niliwauliza kwa ukali na majini wote wakaa kimya
“Aliye jijua kuwa amefanya tukio la kumla au kumdhuru binadamu yoyote ambaye ni mwema akae upande wangu wa kushoto”
 
Majini wakajigawa hadi mimi mwenyewe nikashangaa kwa jinsi wanavyo nisikiliza kwa umakini wa hali ya juu.
“Mkuu sisi ni wachache kati ya wale ambao wametekwa na wanadamu wenye nguvu zinazo endana na wewe.”
Jini mmoja alizungumza kwa sauti nzito akiwa katika kundi la majini walio watafuna watu.
“Hiyo sio mada niliyo nayo,nimeuliza ni kwanini mumewala watu wasio na hatia?”
“Mkuu wezetu ambao wametekwa walipandikizwa roho ambazo ni mbaya ndio maana wakawala watu na sisi tulio nusurika tukajua tumeruhusiwa kuwala watu ndio maana hata sisi tukawala”
Nikaangalia chini na kuona jinsi ukimya wa sehemu tuliyopo ulivyo tulia,Magari mengi yaliacha milango wazi huku mengine yakiwa yameangushwa na kuwashwa moto.
“KUMBUKA KUNA WATU WANAHITAJI MAJINI ILI KUYATUMIA KATIKA KAZI ZAO ZA KICHAWI NA WAGANGA,KUWA MAKINI NA HAO WATU.”
 
Sauti ya taratibu ilisikika masikioni mwangu,na ninauhakika hakuna jin lolote aliye weza kuisikia
“Sasa nifanye nini?”
“UNATAKIWA KUWAREJESHA KWANZA HAO 250 KAMA WALIVYO KISHA UANZE LILE AGIZO LA KWANZA ULILO PEWA.”
“Nitawarudisha vipi?”
“CHAGUA WAFUASI KUMI,NANE WAAMRISHE WAENDE KWENYE KILA KONA YA DUNIA WAKIWA WAWILI WAWILI,KISHA WAWILI WABAKI KATIKATI YA MKOA WAKO”
“Sijakuelewa,hao nane waende pende za dunia mzima au kwa huu mkoa tuiopo?”
“KWEENYE DUNIA,WANAKWENDA KUZUIA KUBADILISHWA KWA WEZAO,NA ENDAPO WEZAO WAKIBADILISHWA ZAIDI WATAWEZA KUKUANGAMIZA KWA MAANA WANAJUA SIRI ZAKO ZOTE”
“Sawa ila wewe sijajua ni nani?”
“MIMI UTANIJUA,NI KIONGOZI WAKO NILIYE AGIZWA KUFANYA KAZI HII”
 
“Asante”
Nikawatazama majini na kuona wakiendelea kusubiria kitu cha kuwaambia,Nikaaamrisha jinsi nilivyo ambiwa na nikapata majini kumi vijana wenye nguvu za kutosha na wenye miili mikubwa.Mara moja wakaanza kazi niliyo wapa,wengine nikawaruhusu warudi nyumbani na nikabaki na wawili wa kunilinda.Nikamuagiza jini mmoja kunishusha chini na akafanya hivyo.Nikaanza kukatiza maeneo ya Club Lakasa Chika na kukuta damu nyingi ikiwa imetawala sehemu nyingi za barabara.
“Mkuu,mimi ninaitwa Khadan huwa ukoo wangungu asili yetu kubwa ni ulinzi kwa binadamu wanao tuhitaji”
“Sawa”
Tukazunguka karibu mji mzima kuna maeneo yamesalimika kwa watu kutafunwa.Wakanichukua hadi nyumbani,Na kumkua Rahma akiwa katika hali ya majonzi.Baada ya kuniona akanikumbatia huku akimwaga machozi
 
“Baby una nini?”
Nilimuuliza Rahma kwa wasiwasi huku nikiwa ninamashaka
“Eddy viumbe vyako vimeua ndugu zangu.”
Nikastuka kidogo sikujua ni vipi amezipata hizi habari
“Nani amekuambia?”
“Nimehisi tu mume wangu”
“Utahisi vipi wakati kitu haujakiona?”
Nikamtazama Rahma machoni,nikamvuta karibu na kumpiga busu la mdomoni na kuingia naye ndani.Hadi inafika jioni majini ambao walikuwa wametekwa wakawa wamerudishwa kwenye himaya yangu.Siku mbili zikapita nikiwa ninaendelea kupata kuwatamua majina na kazi zao wanazo zifanya majini ninao waongoza.Siku ya tatu alfajiri na mapema nikaanza kuwaagiza kazi husika ambayo mimi ninahitaji waweze kuifanya
“Agizo la kwanza ninahitaji muwalete hapa viongozi wote wa dini ambao hawamchi MUNGU wanamtukuza BARBATOS na wezake”
 
Majini wapatao hamsini nilio wakabidhi kazi ninayo hitaji wakanisujudia na kuondoka zao.
“Eddy mume wangu hao viongozi watakao letwa utawafanyaje?”
“Nitajua ni nini cha kuwafanya”
“Ila kuwa makini katika maamuzi yako”
“Usijali kwa hilo”
Ndani ya masaa mawili wakaanza kuletwa watumishi mmoja baada ya mwengine na wengine nikabaki nikiwashangaa kwa maana ni maarufu sana nchini na duniani.Idadi yao ikazidi kuongezeka hadi wakafikia watumishi zadi ya elfu moja.Nikamuomba Rahma kwenda ndani aniache niwashuhulikie hawa wapumbavu
“WAKATI WA HUKUMU UMEFIKA” Niliisikia sauti ikiniambia masikioni mwangu
“Niwafanye nini?”
“WAWEKE KATIKA MAKUNDI NA KILA MMOJA ATAPATA ADHABU YAKE KUTOKANA NA UDANYANYIFU ALIO UFANYA KWA WATU”
 
“Sasa makundi hayo yawe vipi?”
“NITAKUWEKEA KILA MWENYE KUSTAHILI ALAMA YA X NAWE UTAWEZA KUCHAGUA NI NINI CHA KUWAFANYA”
Ndani ya muda mchache watumishi wadanganyifu wengi wakawa wamewekewa alama ‘X’ kwenye mapaji ya nyuso zao.Katika kupita pita na kuwachunguza macho yangu yakakuta na baba mchungaji ambaye anashirikiana na Olvia Hitler na nimiongoni mwa waliotaka kuniangamiza,akatabasamu huku akitingisha kwa dharau nikatamani nimzabe kofi ila askari wangu akanishika mkono na kuionya nisifanye hivyo.Hakuweza kuzungumza chochote kwani nimewaamrisha majini wangu kuwafunga kauli,hii ni kuepuka kuomba misamaha isiyo na msingi wa aina yoyote.Nikawatazama kwa umakini wakiwa katika mistari ya kunyooka kama wanajeshi wa Adolf Hitler.
 
Gafla nikaanza kuona madonge makubwa mawili ya moto yakija kwa kasi kubwa kutoka angani,Majini baadhi yanayo nilinda yakapaa angani kwenda kuyazuia ila wakashindwa na kuunguzwa miili yao
“NI WAKATI WAKO KUPAMBANA WEWE KAMA WEWE,HAO WANAO KUJA NI MAJINI WABAYA AMBAO UMEWACHUKULIA WATU WAO” Sauti iliniambia
“Nifanye nini?”
“TUMIA FIMBO KUYAZUIA”
Nikainyoosha fimbo ya dhahabu niliyo powa,Mwanga mkali ukatoka mbela ya fimbo na kusababisha madonge ya moto kujibadilisha na kuwa katika hali upepo unaokwenda  kwa kasi midhili ya kimbunga cha Katrina.Upepe ukaanza kunizunguka kwa kasi na kujikuta nikiaanza kunyanyuliwa kwenda juu
 
“USIOGOPE ENDELEA KUPAMBANA”
“Mbona nakwenda juu sasa?”
Niliiuliza sauti ninayo isikia ila haikunijibu kitu chochote,Nikazidi kwenda juu na jinsi ninavyozidi kwenda juu ndivyo nguvu za mwili wangu zilivyoaanza kuniishia.Kufumba na kufumbua nikajikuta nipo katikati ya usawa wa bahari.Nikaanza kwenda chini kwa kasi kuelekea yalipo maji
Fimbo yangu ikatoweka mkononi mwangu,nikaanza kuchanganyikiwa.Nikashtukia nikigeuwa kichwa chini miguu juu na kuingizwa kwenye maji kwa kasi ya ajabu,Nikaendelea kupelekwa chini hadi nikajikuta nipo katika mji ambao siuelewi na watu waliopo ndani ya mji huu wanasura za kutisha sana.Gafla upepo ukaniachia na ukabadilika na kuwa watu wenye mikono miine mikubwa inayo tisha.Vichwa vyao vikiwa na mapembe yenye ncha kali sana
 
Ikaninyanyua juu na kunidumbukiza kwenye kisima chenye giza totoro,Nikaanza kushuka kwa kasi kwenye kisima hichi pasipo kufika chini.Sikuweza kuona chochote kwenye kisima kutokana na giza kali.Nikastukia nikipigwa kikumbo kikali kilicho nipeleka chini zaidi.Galfa nikaanguka kwenye ukumbi mkubwa ulio jaa watu wasio eleweka na wakaanza kushangilia,Chakushangaza sikuweza kuumia sehemyu yoyote
“KARIBU KUZIMU BWANA EDDY,NIMEFURAHI KUKUONA KWA MARA NYINGINE”
Sauti ya Olvia Hitler ilinifanya nigeuke nyuma yangu na kumkuta akiwa amekalia miili ya majoka mawili makubwa yanayotoa moto midomoni mwao.Akasimama huku akipiga makofi kwa dharau
“EDDY,HUWEZI KUPAMBANA NA MIMI KAMWE.MIMI SASA CHAGUA MOJA KUACHIA WATU WANGU HURU AU MKE WAKO RAHMA NA KIUMBE CHAKO HICHI NIVIANGAMIZE”
Olvia alizungumza huku akiwa amemshika mtoto mchanga ambaye sikuweza kumuona vizuri sura yake.Olvia Hitler akanyoosha mkono wake kwenye  moja ya lango kubwa,ukafunguka na yakatoka majitu mawili yakutisha yakiwa na vishoka vikubwa na kuwafanya watu waliopo hapa kuanza kushangilia

ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts