Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Saba ( 37 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Saba ( 37 )

Written By Bigie on Thursday, March 22, 2018 | 2:59:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Nilizungumza kwa sauti ya kujiminya kwani mfuniko ulituzidi nguvu,Mzee ngoda akajiingiza katikati yetu na kutusaidia kuufungua mfuniko na kwa pamoja tukafanikiwa kuufungua.Gafla tukastukia kumuona Mzee Ngoda akirushuwa juu kama kifaranga kilicho nyakukiliwa na Mwewe mwenye njaa kali na kitendo cha kutua chini hakuwa na kichwa na damu nyingi zikawa zinaruka kila sehemu na kumfanya Rahma kupiga ukulele mkali

ENDELEA
Nikabaki nikiutazama mwili wa mzee Ngoda jinsi unavyo rusha rusha miguu,Sauti kali nikaisikia kwenye masikio yangu ikiniambia
“Mmoja wenu ni lazima afee”
Nikayakumbuka yalikuwa ni maneno ya bibi,kwa haraka nikamuwahi kumziba mdomo Rahma.
“Shiii nyamaza”
Nikaendelea kumziba mdomo Rahma kwa nguvu kwa kutumia kiganja cha mkono.Tukayashuhudia majini yakitoka na kulizunguka eneo tulilopo sisi huku wakiwa wanaelea elea angani.Nikakitoa kifimbo mfukoni na kuwanyooshea majini yaliyojaribu kwenda mbali,
 
“RUDINI HAPA”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali na majini hayo yakatii,hadi na mimi nikaanza kushangaa.Rahma akanikumbatia kwa nyuma,mwili mzima ukiwa unamtetemeka mithili kama amepigwa shoti ya umeme.Eneoa la anga zima katika eneo tulilopo limefunikwa na majini haya ambayo ni mengi sana na yana sura za kila aina
“Tunakushukuru sana kwa kututoa”
Niliisikia sauti kwenye masikio yangu ambayo ni tofauti sana usikiaji wake kama tulivyo sisi wanadamu,Kwani sauti niliisikia ndani ya masikio yangu na si kama ile inayo ingia kwenye masikia yangu.Nikawatazama kwa umakini na kuwashuhudia wakiwa akatika makindi tofauti tofauti,Wazee sana,wazee kiasi,vijna na watoto
“Munataka nini?”
“Tulikuwa tunauhitaji uhuru,tumeupata kutoka kwako asante sana,tupo tayari kukusikiliza wewe kwa kila kitu”
Hata jini ambaye ananijibu simjui ni yupi kati ya kundi kubwa ambalo limetuzingira mimi na Rahma
 
“Kwa leo tunakuomba tutoke tukatafute japo kitu cha kula,kisha saa kumi na mbili tutakuwa tumerudi”
“Eddy ukiwaruhusu hawa huko kwengine mambo yatakuwa si mazuri”
Rahma aliniambia
“Kumbe hata wewe unawasikia?”
“Ndio”
“Sasa munaniahidi nini nikiwaruhusu kwenda kuchukua chakula?”
“Amani itakuwa juu yetu”
“Hamuto wadhuru wanadamu wengine kama huyu?”
“Hatuwezi fanya hivyo,tunakuahidi”
Nafsi moja inaniambia niwaruhusu na nyingine inaniambia nisiwaruhusu.Nikamtazama Rahma akatingisha kichwa nisiwaruhusu.
“Acha wakatafute kitu cha kula,unadhani hapa wakikaa watakula nini?”
“Haya kama umeoamua hivyo”
“Haya nendeni ila saa kumi na mbili jioni nawahitaji hapa”
“Turuhusu tuanze na mwili huu.”
“Khaaa”
 
Nikautazama mwili wa mzee Ngoda kisha nikawatazama Majini,sura zao baadhi zimejaa upole na masikitiko makubwa,wengine wapo kwenye rah asana.
“Kwanza ni nani aliye fanya hivi?”
Akajitokeza jini wa kiume mwenye mwili wa kawaida tuu na kushuka chini kitendo cha kukanyaga ardhi mwili wake ukakamilika kama wa binadamu wa kawaida,kwani wote anao elea elea angani miili yao imekaa kama donge kubwa la maji.Akapiga magati mbele yangu na kuinama
“Nisamehe mkuu haikuwa dhamira yangu ufanya hivi ila nilimuona kama adui yetu ndio maana nikamdhuru”
“Sawa nimekusamehe”
Akanyanyuka kwa furaha na kurudi juu na mwili wake ukafanana sawa sawa na wezake.Nikawaruhusu na ndani ya dakika mwili wa Mzee ngoda haukuwepo mbele ya macho yetu,walisha utafuna.Wakaondoka kwa furaha huku wakishangilia na kutuacha mimi na Rahma
 
“Eddy nahisi kama nipo kitandani,naota vile?”
“Mmmm upo kwenye maisha halisi mke wangu”
“Eddy wewe umewezaje kuwaamrisha hawa viumbe kwa maana hawaeleweki”
“Wee acha tuu mke wangu”
Tukaanza kushuka kwenye ngazi zilizopo kwenye handaki tulilo lifungua,Tukakuta mafuvu mengi ya vichwa vya watu pamoja na mifupa ikiwa imesambaa chini,Mwanga wa bluu uliopo ndani ya handaki ukatusaidia sana kuyaona mazingira yaliopo humu ndani
“Baby huu mwanga unatoka wapi?”
Rahma aliniuliza kwa sauti ya kuninon’oneza
“Hata mimi sijui unatokea wapi?”
Tukaendelea kutembea kwenye eneo la handaki,lililo na eneo kubwa sana.Tukaingia kwenye moja ya ukumbi na kukuta kila kitu kilichomo ndani ya ukumbi huu kimetengenezwa kwa dhahabu,kuanzia viti,meza ukuta sakafu  vipo kwenye namna hiyo.Nikataka kuokota kikombe cha dhahabu ila Rahma akanizuia
 
“Ona kule”
Rahma akanionyesha mzee aliye keti kwenye kiti cha dhahabu akiwa ameshika fimbo ndefu ya dhahabu huku mikononi mwake akiwa amevalia pete nyingi.Nikashika kifimbo changu vizuri na kuanza kuoiga hatua za taratibu huku Rahma akiwa nyuma yangu akinifwata.Tukafika eneo alilopo mzee huyu ambaye ni wamakamo sana,hata macho yake yanafumbuka kwa shida.
“Nikipindi kirefu sana nilikuwa ninakusubiria wewe,na leo nimekuona”
Mzee alizungumza kwa sauti ya kukwaruza kwaruza
“Nani....Mimi?”
Nilijiuliza swali na kujijibu mwenyewe na kumfanya mzee kutingisha kichwa chake
“Ndio,Imepita karne na karne nikiwa namtazamia atakaye shika falme yangu ya kuwaongoza hawa majini.Tangu ulip kuwa tumboni mwa mama yako niliweza kukulinda hadi ukafika hapa.”
 
“Samahani mzee wangu wewe ni nani?”
“Mimi ni mfalme wa wafalme”
Nikakaa kimya kwani jibu alilo nipa sikujua kama ndio jina lake alisi au ni mbwembwe tuu,Akasimama akisaidiwa na fimbo yake,vazi zima alilo livaa nimepabwa na dhahabu.
“Sogea karibu,Usiniogope”
Rahma akanishika mkono,nikamtazama na kumkazia macho hadi akaniachia mkono.Nikamsogelea mzee na akaninyooshea mkono wake ulio valia pete na bangili nyingi zilizo tengenezwa kwa madini ya kila aina.Nikampa mkono wangu na kitu kama shoti kikautetemesha mwili wangui kwa sekunde kadhaa na kikaachia
“Wewe ndio mridhi wangu,Utaifanya dunia kuwa katika uwezo wako,waongoze wanadamu katika njia ya kumtafuta MUNGU.Ila unakazi kubwa sana ambayo mimi niliishindwa na kujifungia humu ndani kwa siri”
 
“Kazi....kazi gani hiyo?”
“Nitakuambia,Jina langu ni Suleima Mfalme wa wafalme,Nilipewa uwezo mkubwa na MUNGU katika  kuvitawala viumbe vyake,vya baharini na nchi kavu.Watu wengi wanatambua kuwa sasa hivi nimefariki,ndiovyo maandishi yalivyo katika vitabu vitakatifu vya MUNGU.Ila nimepewa nafasi hii ya kuonana na wewe ili roho yangu ikalale mahali salama,nikiwa nimekuachia kazi yangu ya kuendeleza mapambano dhidi ya majini 72 yalio niasi”
“Ehee nitawezaje?”
“Vizuri,Uwezo wako ni mkubwa kuliko mimi.Unasauti kubwa katika viumbe hivi kuliko mimi.”
“Mungu alinipa uwezo mkubwa sana wa kuwatawala ila hao 72 waliniasi na niliwafungia kwenye Gudulia la Shaba na kuwadumbukiza mtoni,Baada ya mimi kufa katika enzi zile wakaja kufunguliwa na watu wa Babilon ambao walikuwa wakitafuta mali na kusababisha majini hayo kuwa huru na kuleta tabu kama unayo iona katika dunia ya sasa”
 
“Baada ya BARBATOS na wezake kurudi katika mamlaka yao,Ndipo nami MUNGU alipo niruhusu nirudi duniani na kuwa katika handaki hili lenye udongo ulio jaa Baraka za Mungu nikisubiria wewe kuzaliwa na kuja kuwa mridhi wangu na laiti nisinge rudi basi Dunia ingezidi kuangamia”
Nikashusha pumzi na kubaki nikimtazama Mfalme Suleiman,ambaye kwa kipindi chote nilimsoma kwenye histori za vitabu tuu.
“Majina hao ni BARBATOS ambaye ni mkuu wao au Mungu wao,BAAL anamiliki mashariki mwa duni,BUER anawapa umashuhuri watu,AGARES huyu husababisha mitetemeko ya ardhi,ni mzee anatumia mamba katika kusafiria,AMON ananguvu nyingi na anamwili wa mbwa mwitu ila anakichwa cha joka lenye ndimi zinazo tema moto ila anabadilika na kuwa kama binadamu anatumika katika upatanishi wa marafiki”
“Sasa hao wote wapo wapi?”
“Duniani”
“Hao walio salia ni wafuasi tu,Kikubwa ni kupambana nao kwa kutumia hekima ambayo umepewa”
 
Mfalme Suleima kwa ishara akaniamrisha nipige goti moja chini wa mguu wa kushoto huku mguu mwengine wa kulia nikiunyanyua kidogo na kuuwekea kisuku cha mkono wa kulia na ngumi ya mkoni wikiwa imegusana na paji la uso na kuangalia chini.Akanishika kichwa na kuanza kuomba kwa lugha ambayo sikuitambua,akatumia dakika zaidi ya kumi katika kufanya maombi yake.Akavua pete mbili kidoleni mwake na kunivalisha,kwenye vidole vyangu vya mkono wa kulia,kisha akaniinua na kunivisha joho lake.
“Nimekukabidhi mamlaka yangi juu ya majini wote wema ambao nilikuwa nao humu ndani,Ila hakikisha hawatekwi na majini waliomo dunia.”
“Nitalihakikisha hilo hakuna linalo tokea”
“Kazi unayopaswa kuanza nayo ni juu ya wale wote wanaotumia nguvu za giza,kuwateka watu wa Mungu katika majengo yao waliyo yaanzisha duniani kote”
“Sawa”
Mfalme Suleiman akamuita Rahma kwa ishana,akaja na kusimama kando yangu.Akachukua pete yake nyingine na kumvisha Rahma kwenye mkono wake wa kushoto
“Pete hii inanguvu ya ushawishi na ikusaidia kumtuliza jazba pale mume wako atakapofanya maamuzi yaliyo kinyume palipo na ukweli”
 
“Sawa” Rahma alishukuru kwa sauti ya unyenyekevu
Mfalme Suleiman akatukumbatia kwa pamoja huku akinipiga piga mgongoni,akasogea nyuma kidogo,
“Utajiri wangu upo juu yako”
Gafla mwanga mkali ulio ambatana na radi ukjatawala ndani ya ukumbi na kusababisha tetemeko kubwa la ardhi.Mfalme Suleiman akanyoosha mikono,wau wawili wenye mavazi meupe pee na madawa mawili mgongoni mwao wakasimama pembeni yake na kumnyayua kwenda juu hana kupotea naye na mwanga ukarudi kama kawaida.
Kila kitu kinacho endelea kwenye maisha yangu ninaona kama mkanda wa kuigiza,Tukatoka nje ya handaki na sote tukaelekea ndani.Mida ya saa tisa jioni tukasikia vishindo nje ya nyumba ikatulazimu tutoke nje kuangalia ni nini kinacho endelea.Nikakutana ana kundi la majini ninao waongoza wakikatiza katiza nje wengine wakiwa wanaelea angani.
 
“Kuna nini?”
Nilimuuliza mmoja wa majini ambaye alisimama mbele yangu
“Mkuu kuna hali mbaya imetoke?”
“Hali gani?”
“Wezetu wapatao 250 wametekwa”
“Wametekwa....!!? Na nani?”
“Tunakuomba utupe ruhusa tukawakomboe”
“Wapi?”
“Sehemu ambayo wapo ni kwenye kisiwa kimoja kipo karibu na bandari ya Tanga”
“Ngoja unaweza kuniambia ni nini kimetokea?”
“Mkuu twende ukajionee”
“Eddy unataka kwenda wapi?”
“Ngoja nikaone mke wangu”
Jini la kiume ambalo ninaongea naye akaniishika mikono na gafla kufumba na kufumbua nikajikuta nikiwa katika anga na sikuamini macho yangu baada ya kuukuta mji mzima wa Tanga ukiwa umetawaliwa na damu nyingi lizilizo tapakaa maeneo mbalimbali ikiashiria watu wengi wametafunwa na majini yangu.

 ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts