Get the latest updates from us for free

Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tano ( 35 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tano ( 35 )

Written By Bigie on Tuesday, March 20, 2018 | 11:53:00 AM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA   

Taratibu nikafungua pazia la dirisha la sebleni na nusu nipoteze fahamu ila nikajikaza kuendelea kutazama.Kundi kubwa la watu wenye asili ya kijerumani wamewazunguka Rahma na jamaa mmoja wa kizungu huku Rahma akiwa amevalia shela la harusi huku na jamaa suti ya harusi na Rahma ameishika pete yangu aliyo itupa akitaka kumvalisha jamaa kwenye kidole kama nilicho kuwa nimekivaa mimi na nikazidi kuchanganyikiwa baada ya muongozaji wa harusi hiyo akiwa ni Olvia Hitler

ENDELEA
Taratibu nikalifunga pazia na kukaa kwenye kichi huku nikijiuliza ninacho kiona ni kwelia au ni ndoto,Kelele za ngoma zikanifanya niweze kuamini kama ni kweli kwa ujasiri mkubwa nikasimama na kuufungua mlango na kuwafanya watu wate waliopo kwenye eneo nje kunitazama kwa macho makali ambayo si ya kawaida kama ilivyo kwa sisi binadamu.Macho yao yametawaliwa na rangi ambazo si za kawaida kwa haraka haraka ninaweza kuzifananisha na mwanga wa moto wa gesi.

Rahma akabaki akinishangaa kama mtu asiye jitambua aliye kamatwa na bumbuazi kali,Nikaanza kupiga hatua mbili mbele na kuwafanya vijana wawili wa kijerumani kusimama mbele yangu na kunitazama kwa umakini kisha nao wakaanza kunisogela huku taratibu wakianza kubadilika maumbo yao kwa kutoka manyonya kama ya mbwa.Nikaanza kurudi nyuma kwa haraka na nikausukuma mlango ila kwa bahati mbaya nikaukuta mlango ukiwa umejifunga kwa ndani.
 
Jamaa wakazidi kunifwata na sikuwa na jinsi zaidi ya kaanza kupiga hatua za hakanyaga maua yaliyopo pembezoni mwa ukuta na kuanza kukimbia kuelekea sehemu yenye msitu,Vijana wa kijerumani naa wakanza kunikimbiza na kadri wanavyo kimbia ndivyo  miili yao ikabadilika na kuwa kama mbwa aina ya Bweha(FOX) na kuzidi kunikimbiza.Sikuwa na namna nyingine yoyote zaidi ya kuuparamia mti kwa haraka cha hadi nikakaa juu ya moja ya tawi huku nikihema na jasho jingi lilimwagika.Mwanga wa mbara mwezi ukanisaidia kuwaona jamaa wakiuzunguka mti huku wakinguruma kwa sauti za kutisha sana.Mbwa watu wakaanza kutoa vilioa vya ajabu na kadri mawingu yanavyozidi kuufunika mwezi ndivyo wao wanavyozidi kupata shida katika miili yao na ambayo ikaanza kurudi katika hali kawaida hadi wa kawa binadamu wa kawaida ila hakuna aliye kuwa na nguo miomgoni mwao
 
Kila kitu ambacho kinaendelea sikuwa ninaamini ni kweli na ninayo jionea,nikajilaza kwenye tawi huku nikiendela kuwatazama jamaa na wakabaki chini ya mti wakiwa wananitazama huku wakinisubiria nishuke.Masaa yakazidi kwenda na kidogo nikaanza kushindana na macho yangu kitika swala zima la usingizi na kila nipojaribu kuyafumbua kwa nguvu zagu zote ndivyo jinsi macho yalivyo zidi kunikatali nakujikuta taratibu nikiyafumba na kausingizi kakanipitia.Nikaanza kuisikia sauti kwa mbali ya Rahma ikiniita na kunilazimu kuyafumbua macho na kukuta mwanga ukiwa umetawala kila sehemu na jamaa sikuwaona,Nikashuka kwenye mti taratibu hadi ninakanyaga ardhi na Rahma akawa amefika kwenye sehemu nilipo
“Eddy ulikuwa wapi?”
Nikamtazama Rahma kwa macho makali yaliyo jaa hasira na sikumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuondoka pasipo kumkibu.Nikapitiliza moja kwa moja hadi sehemu walipo kuwa wakicheza ngoma zao usiku na kuyakuta mazingira yakiwa kama jana mchana tulivyo yaacha na hapakuwa na hata jani linalo onyesha kuwa limekanyagwa.
“Eddy mume wangu si nimekuuliza ulikuwa wapi hujanijibu kitu au hujanisikia?”
 
“Pete yanguipo wapi?”
“Ila baby jana si nilikuambia kuwa nimeitupa”
“Nisikikilize wewe mwanamke usitake nikufanyie kitu ambacho sijapanga kukufanyia ninaomba unipe pete yangu kabla sikakuvuruga.”
Nilizungumza kwa hasira huku macho yangu nikiwa nimeyakaza hadi Rahma akaanza kurudi nyuma
“Eddy kwahiyo mimi unanikasirikia?”
“Ninaomba pete yangu”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiwa nimemsogelea kwa karibu Rahma hadi akaanza kutetemeka kwa woga.Nikamuacha na kuingia ndani,kitu cha kushangaza sehemu ambayo jana damu zangu zilimwagika sikuzikuta ila kila kitu tulicho kiacha nikakikuta kama kilivyo ikiwemo dishi la maji na kiwembe.Wasiwasi ukaanza kunijaa na sikujua ni nini kinacho endelea,nikapitiliza moja kwa moja hadi chumbani na kujitupa kitandani na baada ya muda Rahma akarudi akiwa amechoka na kukaa pembeni yangu
“Baby nimeitafuta ila sijaiona”
“Huo ujinga usiniambie ila kikubwa ninaihitaji peta yangu umenielewa?”
“Ila baby kwani swala la pete si tulisha lizungumza jana na likaisha”
 
“Nitakunyonga Rahma au ndio umemvisha yule bwege wako jana usiku?”
“Eddy mbona sikuelewi hayo yote yametokea wapi?”
“Sasa hivi unielewei eehee?”
“Ndio Eddy sikuelewi ninaona unanichukia pasipo kuwa na sababu ya msingi....”
“Nisikilize Rahma mimi sio mjinga na kama unahisi kuwa mimi ni mjinga tambua ya kuwa umekosea na kamwe usitaraji kuwa mutaweza kuniteka akili zangu wewe na hao mashetani wezako sawa?”
“Eddy mimi shetani?”
“Ndio wewe nishatani tena Shetani mwenye mguu mmoja”
Rahma akaanza kulia kwa uchungu huku akinitazama kwa unyonge
“Tena usijilize kinafki kiasi hichi mimi ninadhani nina mwanamke mtu kumbe unakwenda kufunga ndoa na majini watu wala wasio eleweka ili sasa iweje au unavyo ona mwenyewe umenikomoa si ndio?”
Nilizidi kupayuka kwa hasira
“Eddy laiti kama mimi ni jini basi Mungu anilaani sasa hivi na nife ninaapa kwa jina leke mimi siwezi kukufanyia hivyo unavyo fikiria”
 
“Ahaa kwahiyo jana mimi niliota si ndio....hadi mashemeji zako wakaamua kunilaza juu ya mti?”
“Eddy naomba unisikilize mpenzi wangu........mimi jana usiku niliamka na kwenda jikoni kunywa maji ila nilipo rudi huku chumbani sikukuta kutokana na usingizi mwingi nikajua utakuwa upo bafuni mimi nikaamua kujilaza zangu sasa asubuhi ndio nikaanza kukutafuta na kukukuta ukishuka juu ya mti ila unapo nihukumu nakuniita mimi jini la mguu mmoja unakuwa hujanitendea haki mume wangu....Unavyo niambia hivyo unanipa mimi uchungu mwingi inaonekana kuwa mimi si chaguo lako sahihi.”
Rahma akaendelea kuzungu kwa uchungu huku machozi yakimwagika
“Kwa hiyo niliye muona pale nje sio wewe?”
“Nje wapi mume wangu mbona unaninyanyasa kiasi hicho au kukupenda kwangu ndio kosa?”
“Koma sijazungumzia maswala ya kupendana,mimi ninacho taka kukijua ni kwamba ipo wapi pete yangu”
 
“Eddy sijui nimetafuta sehemu nilipo itupa jana ila sikuiona”
“Ahaa powa niache nilale....ila kabla sijalala nahitaji kujua mbona jana ulipo iona picha ya mke wa Mzee Ngoda ulistuka?”
“Eddy yule dada nilimuona siku moja nikiwa sijielewi pale nilipo pigwa risasi na baba,alikuwa akinijia katika mazingira ya kuogopesha sana kiasi kwamba nikawa ninaogopa sema sikuwa na uwezo wa kusema kuwa ninaweza kupambana naye.”
Nikajikuta nikikaa kimya huku nikimuangalia Rahma akizungumza huku machozi yakimtiririka
“Kuna vitu ambavyo alikuwa akinionyesha vya ajabu ajabu na akaniambia kuwa mimi ni mfu na sito weza kuishi tena,ila akaniambia kuwa nisipo weza kukubaliana na sharti lao moja basi sino weza kurudi kuishi tena duniani”
 
Mwili mzima ukazizima huku nikiusikilizia jinsi unavyo nisisimka na kujikuta nikikaa kitako nakumtazama Rahma vizuri na kumsikiliza kwa umakini
“Walikupa Sharti gani?”
“Waliniambia kuwa nifanye juu chini niweze kukuvua pete ambayo ulikuwa umevaa mkononi,na walinipa siku saba za kuishi ndio maana ile siku ya kwanza ulipo kuja nyumbani mimi mwili wangu ulikuwa umesimama nyuma ya mlango na pale kitandani alikuwa amelala Rahma mwengine anaye fanana na mimi na ndio uliye zungumza naye na baada yaw ewe kuondoka mimi mwili wangu ukaingui kwa yule Rahma uliye mkuta kitandani.”
 
Maelezo ya Rahma yakanichanganya kiasi kwamba nikabaki nikiwa kimya nimemtumbulia mimacho huku akilini mwangu nikijiuliza kwa maana huyu niliye kuwa naye ni Rahma mfu au asiye mfu
“Kwa hiyo wewe hapo upo upo vipi?”
“Eddy mimi ndio Rahma wako halisi ila Rahma mwengine yupo anaye fanana na mimi na endapo akiingia mwilini mwangu ninakuwa na hasira kama niliyo ishika jana nilipokuwa ninakulazimisha kuweza kuivua pete yako.”
Nikajikuta nikichoka pasipo kufanya kazi,hali ya mashaka ikaanza kunitawala juu ya Rahma huyu ambaye ninaonge.
“Ila Eddy kwa nini ulinificha?”
“Nilikuficha na nini?”
“Hujui kuwa wewe ndio chanzo cha haya yote”
Nikabaki nikiwa ninamtazama Rahma huku nikikosa la kunzungumza na sikjua nimwambie nini juu ya kitu anacho dai mimi ni chanzo

ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts