Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tatu ( 33 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tatu ( 33 )

Written By Bigie on Saturday, March 17, 2018 | 1:50:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

Gafla tukastukia akiichomoa bastola yake na kutonyooshe sisi na Rahma na kwastory nilizo wahi kuzisikia mtaani kweni ni kwamba huyu mzee anatabia ya kutembea na wasichana wadogo japo sikuwahi kumshuhudia na kwa story nyingine nilizo zipata mtaani ni kwamba alimuua mke wake kwa kumpiga rasasi baada ya kufumaniwa akiwa na binti mdogo

ENDELEA
Mlio wa bastola ya mzee Ngoda ukanifanya nifumbe macho huku nikisikilizia ni wapi risasi yake ilipo tu,Swali nililo nalo kichwani kwangu ni kwamba ni wapi risasi ilipo tua kwa maana mwilini mwangu sikusikia maumivu ya aina yoyote na kama imempiga Rahma wangu mbona sijasikia sauti yoyote ya yeye kutoa maumivu.Kwa haraka ni kafumbu macho na kumtazama Rahma na kumkuta akitetemeka kwa woga
“Angalieni nyuma yenu”
Tukageuka na kukuta nyoka mkubwa akining’inia kwenye tawi la mti huku kichwa cheke kikiwa kimetawanywa na risasi aliyo pigwa na Mzee Ngoda
 
“Mwanajeshi anatakiwa kuwa na hisia za kitu chochote cha Atari kitakacho kuwa karibu yake ila nakushangaa Eddy wewe nyoka yupo nyuma yako wala hustuki kwa kitu cha ina yoyote”
Kutokana na mstuko wala sikujua nimjibu kitu gani mzee ngoda,Rahma akanishika mkono na kunikumbatia huku akiendelea kutetemeka.Mzee Ngoda akapanda kwenye gari na kutuomba na sisi tupande,taratibu nikamshika Rahma mkono na tukapanda kwenye gari na safari ikaendelea ambayo tayari nilisha anza kuitilia mashaka na sikujua ni wapi tunapoelekea.Tukafika kwenye moja ya jumba kubwa lililo jegwa vizuri na Mzee Ngoda akasimamisha gari nje ya jumba hili na akatuomba tushuke kwenye gari
 
“Karibuni sana wanangu hapa ni nyumbani kwangu”
Mzee Ngoda alizungumza huku akitoa funguo nyingi na kufungua geti la chuma lililopo kwenye jumba hili,kisha akafungua na mlango mwengine na tukaingia ndani japo kuna giza kuba.Akawasha swichi na taa za ndani zikawaka
“Hapa ni kwangu huwa nikiwa na mawazo sana huwa ninakuja huku kupumzika kama wiki kisha ninarudi tena mjini”
“Unakuja kupumzika peke yako?”
“Ndio ninakuja peke yangu na niwatu wengi hawaijui hii nyumba yangu kwa maana ipo porini sana”
“Ni kubwaa”
 
“Yaa ina eneo kubwa kwa huko nyuma kuna bustani za maua ya kutosha sema sasa hivi ni usiku sana….Hii nyumba niliinunua kwa rafiki yangu alikuwa ni mwanajeshi wa kijerumani kipindi cha miaka ya semanini”
“Ahaa sawa”
Mzee Ngoda akatuonyesha chumba cha kulala ambacho ni kikubwa sana na kina vitu vichache vya dhamani pamoja na kitanda kikubwa cha duara ambacho tangu nizaliwe sikuwahi kulala,nikakichunguza chumba kizima  na kuridhika na mazingira yaliyopo humu ndani.Nikavua nguo zangu na kupanda kitandani na Rahma akafanya kama nilivyo fanya mimi na ikawa ni siku nyingine ya furaha katika mahusiano yetu baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha.Baada ya kupeana haki ianyo stahili kila mmoja akapitiwa na usingizi mzito
 
Jua kali kiasi linalopita kwenye dirisha na kutupata kitandani ndilo lililofanya niamke na kushuka kitandani na kumuacha Rahma aendelee kulala,Nikaoga na kutoka na kuvaa nguo zangu na kutoka nje na kumkuta Mzee Noda akifanya mazoezi
“Shikamoo mzee”
“Marahaba ila Eddy hilo jina la mzee nilisha kukataza”
“Ahaa samahani baba yangu
Mzee Ngoda akamaliza kufanya mazoezi na akaanza kunitembeza kwenye kila sehemu ya jumba lake la kifahari na kusema kweli wajenzi wa hili jumba waliweza sana kulijenga kwa maana lina vyumba hadi ardhini na maeneo makubwa ya michezo pamoja na sehemu ya kuhifadhia magari ya kutembelea
 
“Hizi ni Ford za mwaka gani?”
“Aaaa hizo gari ni za mwaka 1932 mimi jamaa alikuwa akizitumia zamani sana ndio kaniachia mbili za ukumbusho”
Tukaendelea kutembea tembea kwenye bustani zenye maua mazuri ya kuvutia
“Haya matunda yote unayo yaona hayana mlaji mengi yanaiva na kuanguka chini”
“Ina maana huku hakuna watu wanaofika kwenye hii nyumba?”
“Hakuna kwa maana hapa ni katikati ya msitu isitoshe kuna ukuta kubwa umezunguka hili jumba upo mbali sana na hapa hadi kuufikia kwa kutumia miguu ni mwendo wa masaa matatu na nusu hadi mane”
“Ehee kumbu ni kukubwa hivyoo?”
“Ahh wee acha tuu wezetu zamani walikuwa na akili sana na hata hii miti yote unayo iona asilimia 90 ameipanda yeye mingine ni miti ya asili kama ulisha wahi kusoma kuwa kuna misitu ya kutengenezwa huu ni mmoja wapo”
“Ahaa kweli alijitahidi ndio maana nikawa ninashangaa ni kwanini hii miti imepandwa kwa mistari ila nikashindwa kukuuliza tuu”
 
“Ni yeye jamana alikuwa anaitwa Muller Shostaiger Manzuchuk”
“Ehee kweli hilo jina ni la kijerumani”
“Yaaa”
Tukaendelea kuzunguka maeno ya karibu na jumba lake na baada ya kumaliza tukarudi nyumbani na kumkuta Rahma akiandaa kifungau kinywaa.Kutokana na upendo nilio kuwa nao juu yake nikamsaidia kupika piaka anacho kipika,tukaandaa chakula mezani na sote tukajumuika kwa kula.
“Jamani mimi leo nitarudi mjini sasa nyinyi sijui mutakaa kwa kipindi gani huku?”
“Kama wiki hivi?”
“Eddy wiki…….baba yangu sisi tutakaa zaidi ya wiki sitamani kurudi mjini kwa maana ninajua ni lazima baba atakuwa ananitafuta”
“Sasa Sheila tutakaa kwa kipondi gani huku?”
“Kwa muda wowote hadi nichoke mwenyewe ndio nitarudi mjini?”
“Na shule jee?”
“Shule ya kazi gani?”
“Lakini Eddy wewe si mwalimu…..? Utakuwa unamfundisha huku huku mke wako”
“Ahaa jamani haya hapo sina ubishi mumeshinda nyinyi”
“Yeaa kila ninacho kifanya lazima nikishindee”
 
Raham alizungumza huku akinyanyuka na kuelekea jikoni
“Mmmm mwangu huyo mkwe wangu anavutia sana kwa maana mmmm hongera sana”
“Asante”
“Ila kitu ambacho ninapenda kukuambia usije ukaja kumuacha huyu msicha ua kumsaliyi kwa maana utakuja kupata matatizo makubwa sana utakayo yajutia kwenye maisha yako”
“Mmmm matatizo gani?”
“Hapa hakuna cha kuuliza ni matatizo gani ni wewe tuu kuwa makini na kumlindia penzi lake….Kindi ninamuoa mke wangu nilikuwa ninampenda sana tena sana ila hadi ikafikia hatua ya mimi kumuua ilinilazima kufanya hivyo ili kuondoa dukuduku nauchungu ulio kuwa moyoni mwangu”
“Alikufanyaje?”
“Ni historia ndefu tena sana”
Rahma akarudi na kukaa kwenye kiti alicho kuwa amekikalia na Mzee Ngoda akamtazama sana Rahma kisha akatabasamu na kumalizia na kicheko
“Baba mbona unacheka?”
 
“Ninacheka kutokana mke wangu alikuwa ni muarabu kama huyu mkwe wangu hapa na tabia za waarabu ninazijua vuzuri kwa maana wazazi wake nao hawakupenda sana mimi nimuoe na kipindi kile ndio ninatoka zangu depo bado kijana mbichi mbichi ninavutia ahaa basi mtoto alidata sana sema wazazi wake baada ya kugundua mimi ni mwanajeshi walipiga sana kelele nikaamua nimtoroshe kinguvu na kuja kumuweka huku msituni hadi alipo pata ujauzito na alipo karibia kuzaa ndio nikamrudisha mjini na akajifungua yule mwanangu wa kwanza na wapekee…..”
“Basi kadri miaka ilivyo zidi kukatika ndivyo jinsi nilivyozidi kumpenda mke wangu ila kuna kipindi nilichukuliwa na serikali nikapelekwa Cyuba nakumbuka ilikuwani mwaka 1999 na kule nilikaa miaka mitano mbali na yumbani kwangu.Ila nilipo rudi nikamkuta kijana mmoja ambaye alidai kuwa ni mhuhudumu wa ng’ombe…..aaah kuntokana sikuwa na mud asana sikuweza kumfwatilia sana mke wangu ila tabia yake ilianza kubadilika”
“Alibadilikaje?”
“Jamani mimi mwezenu wala sijui hta munazungumzia kitu gani?”
 
“Subiri nitakuaadisia wakati wa kulala”
“Mmmm jamani mbona munanitenga au mimi sistahili kuielewa story yenu”
“Lakini mpenzi wangu mbona unakatisha utamu hembu tulia kwanza baba amalizie”
“Mwaya mweke ni kwamba story ninayoizungumzia ni kuhusiana na mke wangu ambaye kaburi lake lipo nyuma yah ii nyumba”
“Ina maana baba wewe huna mke?”
“Ndio sina mke kwani alisha kufa siku nyingi sana”
“Ahaa masikini pole baba yangu”
“Asante”
“Alikuf a na nini?”
“Rahma unakatisha utamu wa story hembu nyamaza bwan”
“Kwani nimekuambia wewe Eddy.......hembu litazame lile komo leke”
“Ndilo ulilo nipendea”
Sote tukajikuta tukicheka kwa furaha
“Kwa ufupi mke wangu nilimuua kwa kumpiga risasi”
“Haaaa....!!”
“Dawa ya meno hiyo si ulikuwa unataka kujua sasa unashangaa nini.....mwaya baba endelea na story”
“Kwa makelele yenu mumenifanya pia nimesahau ni wapi nilipo ishia?”
 
“Umeishia pale uliposeme tabia yake ilianza kubadilika”
“Eheee basi kila nilipokuwa nikimuomba chakula cha usiku basi akawa ananinyima kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi lakini kipindi cha nyuma yeye ndio alikuwa anakiomba tena kwamachozi pale nilipo kuwa nimechoka alikuwa akilia kama mtoto”
“Mmmm chakula cha usiku ndio nini baba?”
“Rahmaa ahaa utaniboa sasa”
“Mkwe wangu chakula cha usiku hata wewe jana ninaimani umekila”
“Rahma usijifanye hujui wakati kila kitu unakijua.....watu wamefunga bwana usiropoke mambo mengine si yakuyazungumza”
“Wewe umefunga wakati jikoni ulikuwa ukidokoa dokoa soseji”
 
Ikanilazimu nimzibe Rahma mdomo kwa kiganja ili mzee Ngoda aendelee na Stori ya ma ishayake
“Basi ile tabia mimi ikaanza kunipa mashaka na mbaya zaidi mwanangu alikuwa bord kwa maana nilimpeleka tangu akiwa chekeche”
“Eddy nikizaa mwangu swala la bord sitaki kulisikia”
“Haya nimekusikia nyamaza”
“Kuna siku nilimuaga mke wangu kuwa ninakwenda Congo kikazi na haikuwa hivyo nikachukua chumba hotelini na kukaa siku mbili bila kutoka njee na siku ya tatu usiku wa manane nikaelekea nyumbani kwangu nikaruka ukuta na kuingia......Sikuingia ndani kabisa ila nikazunguka kwenye chumba cha dirisha ninalo lala.....katika siku nilizo umia moyoni mwangu ni siku ile kwa maana nilimshuhudia mke wangu akishuhulikiwa na yule mtunza ng’ombe tena nilikuta kipindi anapigwa makofi ya makalio na yule mchunga ng’ombe huku akiamrishwa anitukane tusi ambalo hadi kesho naingia kaburini siwezi kulisahau ni lile alililokuwa anaalizungumza kwa sauti ya kejeli.....MUME WANGU NI FALA HAWEZI CHOCHOTE....iliniuma sana”
 
Rahama akaanza kucheka kichini chini na akashindwa kuvumilia na kuaanza kucheka kwa nguvu na kunifanya na mimi nijikaze kucheka huku nikimuliza Rahma
“Kinacho kuchekesha ni nini sasa....”
Nikajikuta na mimi nikicheka sana hadi nikahisi Mzee Ngoda anaweza akachukia ikanibidi nijikaze japo sura yangu imejaa tabasamu la kucheka
“Wee acha tuu niliitwa Fala mimi na kuambiwa siwezi kabisa....hilo ni tusi dogo kuna mengine makubwa sana alinitukaa tungekuwa sisi wawili ningekuambia sema huyo mkwe wangu hapo ninalinda heshima yangu”
Rahma akainama chini ya meza kwani kila anapomuangalia Mzee Ngoda anashindwa kukizuia kicheko chake hadi machozi yanamwagika
“Niliondoka zungu huku nikiwa mnyonge sana ila nikaataka kumfanyia kitu kibaya mke wangu ila nikaona nimsamehe na kesho yake asubuhi nikarudi na kumuambia safari imehairishwa......kutokana ninampenda mke wangu niliamua kumuambia tabia yake ila alikataa kata kata”
 
“Aaaah kweli hata kama ni mimi ningekuwa mwanaume huyo mwanamke ningemua kwa njia yoyote ile”
“Basi nilifunga kamera za ulinzi za siri siri nyumbani kwangu pasipo kumjulisha mke wangu cha kushangaza sasa wakawa wanaendelea kufanya vitu vyao kama kawaida.....nikaamua na mimi nianze kwenda nje ya ndoa na nikaanza kumfanyia kubuhu nikawa sirudi home nalala siku mbila tatu nje ya nyumba...kumbe na yeye akawa ananifwatilia na kunakitu nilimfanya yule mkata majani hadi kesho huko alipo kama yupo hai nahisi anajutia”
“Ulimfanya nini?”
“Nilimchoma sindano yenye dawa ambayo itamfaya mika yake yote hadi anakufa mashine yake isisimame hata kama anatumia dawa za namna gani haiwezi kusimama”
“Duuu”
“Tena ngoja nikawaonyeshe kaburi lamke wangu muda kidogo umekwenda”
Tukasimama na tukatoka nje na kuzunguka upande wa pili wa nyumba na gafla nikaanza kumuona Rahma akianza kubadilika sura yake baada ya kuiona picha iliyo wekwa juu ya kaburi la mke wa Mzee Ngoda

 ITAENDELEA


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts