Get the latest updates from us for free

Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tisa ( 39 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tisa ( 39 )

Written By Bigie on Saturday, March 24, 2018 | 3:35:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Olvia alizungumza huku akiwa amemshika mtoto mchanga ambaye sikuweza kumuona vizuri sura yake.Olvia Hitler akanyoosha mkono wake kwenye  moja ya lango kubwa,ukafunguka na yakatoka majitu mawili yakutisha yakiwa na vishoka vikubwa na kuwafanya watu waliopo hapa kuanza kushangilia

ENDELEA
Nikabaki nikiwa nikiyatazama majamaa yanayo kuja kwa mwendo wa taratibu ulio jaa vishindo.Nikatazama vishoka walivyo vishika na kujikuta mwili mzima ukiingiwa na hufu
 
“NIMERUDI”
Nikaisikia sauti ambayo mara kwa mara huwa inanielekeza nini cha kufanya,
“Muda wote ulikuwa wapi hadi umeniacha nimekuja huku chini?”
“NILIKUWA NINAMANA YANGU”
“Maana gani?”
“MANAA KUU NI KWAMBA UJE KUICHUKUA DAMU YAKO KABLA HAWAJAKUDHURU ZAIDI”
“Sasa nitamchukuaje?”
“USIJALI KWA HILO”
Sauti ninayo zungumza nayo kidogo ikanipa matumaini ya kuweza huku kizimu nilipo.Nikastukia  kuona watu watu wapatao sita,walio valia mavazi meupe wakiwa wamenizunguka.Mwanga mkali mweupe ukaanza kumulika katika eneo zima lililo kaa watu wanaoshangulia.Mwanga ukasababisha miili ya watu hao kuanza kupasuka vipande vipande.Majiu yaliyokuwa yakinifwata nayo yakaanza kupasuka vipande vipande.Olvia Hitler akabaki akiwa amenitazama kwa macho makali.Sikuweza kujua ni kwanini mwanga haukuweza kumdhuru,
“Mbona yule msichana audhuriki na huu mwanga”
“TUNAUA KWANZA WATU WAKE”
Watu walio nizunguka,wakaanza kazi ya kukimbia huku wakinizunguka kwa kasi kubwa,Nikajashangaa nikianza kupanda kwenda juu hadi nikafika sehemu alopo Olvia Hitler,
“USIMUOGOPE MSOGELEE”
 
Nikaanza kupiga hata za taratibu huku nikiwa ninajiamini sana,Olvia Hitler akabaki akinitazama kwa macho makila
“MCHUKUE HUYO MTOTO,HAWEZI KUKUZUIA TUMEMFUNGA MWILI WAKE”
Nikaupeleka mkono wangu wa kulia alipo mtoto,Olvia hakuweza kunifanya kitu chohote zaidi ya kubaki akinishanga,Nikamchukua mtoto wangu,Jambo ambalo linaniogopesha juu ya huyu mtoto ni jinsi alivyo.Sura yake haijaendana kabisa na mimi hata mwili wake si wakawaida kama watoto wengine
“Hivi huyu ni mwanangu kweli?”
“WEWE MCHUKUE HUYO MTOTO TUONDOKE”
Sikuwa na lakuuliza zaidi ya kumchukua mtoto,Nikajistukia nikivutwa nyuma,watu walio nizingira kwakanishika na kuanza kwenda juu.Tukiwa katikati kuna sehemu nikaiona ikiwa na moto mwingi sana
“Pale ni wapi?”
“NI KWENYE ZIWA LA MOTO,WALE WOTE AMBAO WANAFANYA MAOVU WANAPELEKWA KULE.NA SIKU YA MWISHO WA DUNIA MOTO UTAONGEZEKA MARA DUFU”
“Mmmmm naweza kwenda kupaona?”
 
“UNA MOYO WA KUVUMILIA?”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“KUNA HALI YA KUTISHA JE UTAWEZA KUVUMILIA?”
“Ndio”
“NITAKUZUNGUSHA KWA DAKIKA KUMI NA TANO TUU”
“Sawa”
Wakanichukua na kunipelea sehemu yanye giza kuwba,Galfa nikasikia kelele za ajabu ambazo siwezi kuzifananisha na kiumbe cha aina yoyote duniani.Kila tunavyozidi kwenda mbele ndivyo jinsi kelele zilivyo zidi kuongezeka.Gafla nikamuona mnyama mkubwa sana mwenye pembe kumi na vichwa saba na mfano wake kidogo anaendana na chui na mdomo ya vichwa vyake vimefanana na Simba.Mwili kigogo ukaanza kunitetemeka,Pembeni ya mnyama huyu nikaliona jijoka likubwa lenye vichwa kumi na mbili.Unene wa mwili wake sikuweza kuupatia mfano.Mkiwa wake unaendana na mkia wa Tai
“HILI JOKA NDILO LINALO TAWALA HUKU KUZIMU NA LINA MAMLAKA KUBWA SANA NA NDIO SHETANI MWENYEWE”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikatamani kuwaambia kuwa tuondoke
“Akituona itakuwaje?”
“HATUONI KWA MWAANA SISI NI TOFAUTI SANA NA WAO,ILA ITAFIKIA KIPINDI WATATUONA”
“Leo?”
 
“HAPANA”
“Na lile jinyama?”
“Na lile jinyama?”
“LILE NDIO MKE WA LILE JIJOKA NA PALE HUWA ANAPEWA MAMLAKA NA LILE JOKA”
Tukaipota sehemu na kutokea sehemu ambayo kuna eneo kubwa lenye moto mwingi.Watu wengi wakiwa wamo kwenye bwawa la moto.Miili yao inatobolewa na funza wakubwa walio nenepa sana na wana midomo inayo fanana na nng’e,Nikabaki nikijaribu kutazama  kama nitaweza kujaa baadhi ya watu ila sikuweza kuzitambua sura zao kutokana ni nyeusi sana,Vilio vilitawala katika kila sehemu ya bwawa la moyo
“Hawa nao wamefanya nini?”
“HAWA NI WALE WOTE WANAO ENDENDA KINYUME NA TARATIBU ZA HUKU KUZIMU”
“Kivipi?”
“KUNA WATU AMBAO WANAMUABUDU SHETANI,SIKU AMBAYO WANAVUNJA MASARTI YA SHETANI BASI HULETWA HUKU,NA HUWA WANAKUFA KWA SIKU ZAO WAO WENYEWE ILA SI ZILE ALIZO ZIPANGA MUNGU”
“Mmmmm,sasa ikifika siku zao za kufa inakuwaje?”
“WANATOLEWA HUMU NA KUPELEKWA KATIKA SEHEMU AMBAYO YUTAIENDELEA”
Kila sehemu ya ziwa la moto kunamiminika uji uji wa moto kutoka juu sana,sehemu ambayo ukiitazama huoni mwisho wake.Uji unafanana sana na uji wa volcano inayo toka kwa wingi.
 
“UNAWAONA WELE”
Mmoja wa watu wangu walio nizunguka aliunyoosha mkono kwenye upande wa kushoto wa sehemu tuliyopo.Nikaona kundi kubwa watu wakiwa wanalia kwa vilio vya ajabu sana na miili yao ikidonolewa na mandege makubwa mawili,yenye sura za kutisha sana.Midomo yao ikiwa ni mirefu sana na inafanana na misumeno mikubwa ya kukatia mbao
“WALE NI WATUMISHI WAONGO,KAMA WALE AMBAO UMETOKA KUWAKAMATA.NA WALE WANAPATA ADHABU TOFAUTI SANA NA WEZAO”
Hali ya mandege makubwa ikawa na kazi kunyofoa nyofoa nyama za miili ya watumishi hao,kiasi kwamba kila ninapowatazama nikajijihisi ndio mwili wangu ndio unavyo nyofolewa,Tukaendelea kwenda mbele hapo ndipo nilipokutana na mavitu ya kutisha yenye mingurumo mizoto kiasi kwamba nikabaki nikiwa nimeyatazama,
“Ni manini haya?”
“HAO NI MAJESHI WA HUKU KUZIMU,ENDAPO SIKU KUTATOKEA VITA KATI YA MALAIKA WA MUNGU GABRIEL AKIWA NA MAJESHI YAKE BASI UJUE ANAPAMBANA NA HAYA MADUDE.HAPA YAMELALA ILA YAKIPEWA NGUVU NA LILE JOKA NDIO UTAONA JINSI YANAVYO FANYA KAZI”
 
“Mmmmm.....!!”
“USIGUNE NDIO HALI ALISI”
“Na vita hivyo husababishwa na nini?”
“UTAJUA,DAKIKA ZETU ZIMEKWASHA TUNARUDI DUNIANI”
Tukaondoka zetu na kuanza kwenda juu kwa mwendo wa kasi,Tukatokea sehemu ya bahari ambapo tuliingilia mara ya kwanza.Wakanikabizi fimbo yangu ya dhahabu,wakanirudisha hadi nyumbani huku mkono mmoja nikiwa nimembebe mwanangu.Rahma akanishangaa baada ya kuniona nikiwa nikitokea kwenye msit ulipo karubu na nyuma yetu
“Eddy ulikuwa wapi?”
“Kuna sehmeu nilikwenda mara mara moja”
“Huyo mtoto umemtoa wapi?’
“Nimemuokota huku porini”
“Mmmmm mtoto mwenyewe mbona wa maajabu ajabu hivyo?”
“Hata mimi mwenye ninashangaa,Ndio maana niliamua kuja naye”
“Eddy,hembu wape hao viumbe vyako kumla huyo mtoto”
“Ili iweje?”
 
“Eddy ninamashaka kabisa na huyo mtoto.Nafsi yangu hainipi jibu kabisa juu ya huyo mtoto”
Nikataka kumjibu Rahma kwamba huyu ndio kiumbe wake aliye tolewa tumboni mwake Olvia Hitler kwa madai ya kumsaidia katika kumlea
“USIDHUBUTU KUNYANYUA KINYWA CHAKO KUMWAMBIA KWAMBA HUYO NI MWANAE”
Sauti ilinionya,Nikampita Rahma na kungia zangu ndani.Nikamlaza mtoto kitandani japo nimeambiwa kuwa ni mwanangu ila hata mimi mwenyewe nikaanza kupata mashaka juu ya mtoto.
“Eddy,yaani huyu mwanao ndio umeamua kumlaza kwenye kitanda ambacho tunalala mimi na wewe?”
“Si mtoto jamani”
“Ahaaa hembu mtafutie sehemu umuweke.kumbuka kuwa mimi ndio mshauri wako mkubwa na hii pete nilivalishwa kwa kazi hiyo.Hembu naomba unisikilize mume wangu fanya hivyo”
Nikamnyanyua mwanangu na kumpeleka chumba cha pili na kumlaza kitandani,Nikamtazama kwa muda,kichwani kwachangu sikupata jibu la kueleweka.
“Labda ni kutokana na jinsi alivyo kaa tumboni mwa jini”
Nilijisemea mwenye kimoyo moyo.Nikaufunga mlango na kutoka nje.
“NI MUDA WA KUWAHUKUMU HAWA WOTE,AKGIZA WAPELEKWE KULE KWENYE LILE ZIWA LAMOTO.ILA HAWA WATAPATA MATESO MAKALI KULIKO WENGINE KWA MAANA WANAKWENDA KULE WAKIWA HAI”
“Wote”
“WOTE NDIO”
“Hawa viumbe vyangu watarudi kweli?”
 
“NDIO NITAKUWA PAMOJA NAO”
“Nahitaji siku na wewe nikuone,kwa maana tunazungumza pasipo mimi kukujua”
“UTANIONA”
Nikafanya kama suti ambayo inanishauri muda wote akilini mwangu,Nikawaagiza majini kuwachukua watumishi wote.Ndani ya dakika moja watumishi wote wakapotea mbele ya macho yangu.
“Eddy wanakwenda wapi wale?”
“Kutoswa baharini.”
“Eddy mbona unafanya kazi nyingine pasipo kunishirikisha?”
“Ahaa wacha wakafe”
“Sawa,twende ukashuhudie hicho kiumbe chako huko ndani”
“Si amelala?”
“Wewe twende ukajionee”
“Ngoja nitakuja”
Rahma akaondoka akiwa amenuna.Majini walio salia nikawaamuru kuingi kwenye handaki ambalo walikuwa wakiishi na sikuufunga mlango.Nikiwa ninarudi kwenda ndani nikastukia kumuona bibi aliye nitibu akiwa amesimama mbele yangu
“Bibi nini tena?”
“Kuna tatizo?”
“Tatizo gani?”
“Umewatoa sadaka viumbe vyako.Pili unaongozwa na roho potofu na huyo unaye zungumza naye ni yule mwanaume jini uliye tembea na mke wake?”
“Nani?”
 
“Hilda,Si unamkumbuka vizuri?”
Mapigo ya moyo yakanienda mbio kiasi kwamba nikawa sijui nifanye nini.Bibi akabaki akiwa ananitazama
“Bibi mbona sikuelewi?”
“Utanielewa,Kumbuka nilikupa kifimbo ambacho kingekutambulisha kwa kila ambaye unazunguumza naye kama ni mbaya kwako au si mbaya kwako,ila umekiweka na kutumia hiyo fimbo kubwa japo ina uwezo ila si wautambuzi kama ilivyo kile kifimbo changu kidogo”
Nikashusha pumnzi nyingi.Gafla nikamuona Rahma akitoka ndani kasi huku akipiga kelele.Ikanibidi kukimbia na kwenda kumshika
“Nini wewe?”
“Nenda kajionee jitoto lako”
Nikakimbilia ndani na kwenda moja kwa moja nikaingia chumba alipo mtoto,Sikuyaamini macho yangu kwani nilimkuta amekuwa mkubwa na kufikia ukubwa babu mtu mzima mwenye mandevu mengi na anatisha kupita maelezo,akanitazama kwa jicho lake kililo kubwa kama gololi za kuchezea pooltable
“NATAKA DAMU YAKO”

ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts