Get the latest updates from us for free

Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Mbili ( 32 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Mbili ( 32 )

Written By Bigie on Friday, March 16, 2018 | 1:38:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

“ILA BABA KWANINI UMUUE EDDY WANGU?”
Swali la Rahma likawafanya watu wote kumtazama na nikaanza kuziona sura za askari zikianza kubadilika na kuweka mikunjo askari wawili wakaziweka bunduki zao sawa kuzielekeza kwa baba Rahma  huku mkuu wao akipiga hatua hadi kitandani na kumuuliza Rahma swali
“Unasema kuwa Eddy ameuliwa na baba yako?”
‘NDIO”

ENDELEA
Chumba kizima kikatawaliwa kwa ukimya kiasi kwamba kila mmoja macho yake yakamgeukia baba Rahma
“Huyo Eddy kwako alikuwa ni nani?”
“Ni mpenzi wangu ninaye mpenda sana”
Nikanyata taratibu huku shangazi Rahma akiwa anaendelea kuwaomba askari waweze kuzungumza juu ya swala alilo lizungumza.Nikashuka kwenye ngazi za gorofa lao na nikatoka nje na moa kwa moja nikeelekea nje na safari ya nyumbani kwangu ikaanza.Moyoni mwangu nikaanza kuhisi hizto na wa ushindi mkubwa kwani swala la kuingia nyumbani kwa kina Rahma pasipo wazazi wake kufahamu na nimtu mmoja ndio amelitamvua hilo kidogo likanipa faraja ya kuweza kumtorosha,nikanawa sura yangu na nikarudi katikahali yangu ya kawaida
 
Siku nzima nikajifungia ndani na sikutoka nje huku nikiwa ninapanga mipango ya kumtorosha Rahma katika hali ya kawadi,Picha nyingi nilizo zichora kwenye karatasi nyeupe zikiwa kama ramani ya nyumba ya baa Rahma zinakanitosha zaidi kujua kuwa ninaanzia wapi katika kufanikisha swala la kumtorosha Rahma hadi nikajikuta ninapitiwa na usingizi katika kocho nililo kalia.Asubuhi na mapema nikaelekea nyumba ya pili kwa mzee mmoja ambaye na mstaafu wa jeshi na kipindi cha nyuma aliniomba niweze kumfundisha mwanaye wa kiume masomo ya kumbo yake ya PCM na kwa bahati mbaya sikuweza kupata muda huo kutokana na matatizo
Nikagonga geti lake nalikafunguliwa na mlinzi na akaniruhusu kuingia ndani na kwabahati nzuri nikakutana na mzee Ngoda akifanya mazoezi kwenye moja ya bustani yake na nikamfwata hadi sehemu alipo na kumsalimia
“Vipi Eddy kuna siku nilisikia sikia kelele huko kwako ila kutokana nilikuwa ninawageni muhimu sana nikashindwa kutoka”
“Mzee wee acha tuu kuna mambo mengi yalinikumba hivi vijiwiki kadhaa vya nyuma nikajikuta hata ninashindwa kutimiza ile ahadi ya kumfundisha mwano”
 
“Mambo gani kwa maana nilipo kuja kuchungulia sikukuta mmtu zaidi ya ukimya mwingi?”
Nikaanza kumsimulia mzee Ngoda kuanzia mwanzo hadi mwishio kuhusiana na mkasa wa Rahma hadi ninamaliza akabaki akisikitika huku akishusha pumzi nyingi mara kwa mara
“Duuu sasa wewe unataka nikusaidie nini juu ya hilo swal lako?”
“Mimi ninataka unisaidie juu ya mipango na mbinu za kijeshi ili niweze kwenda kumtorosha yule binti”
“Hjui hilo ni kosa la jinai na kama ukikamatwa hapo unachukuliwa kuwa kama gaidi na kifungo chake nina imani unakijua”
“Ndio ninakutambua mzee wangu ila naomba tuu unisaidie”
“Wee koma wenyewe wanasema uzee mwisho msata kila mtu mjini ni baby”
Nikajikuta nikangua kicheko kwani sikutegemea kama mzee ataweza kuniropokea maneno ya namna hii ukilinganisha na umri wake.
 
“Eddy mimi kama mimi kwenye hilo sinto weza kukusaidia labda kuna jengine useme nitakusaidia kwa maana nitakuwa nimevunja sheria na kanuni za jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na sheria za jeshi.”
Mzee Ngoda akanikatalia kata kata na sikuwa na kingine cha kuzungumza zaidi ya kuondoka zangu na kurudi nyumbani kwangu.Nikajipikia kifungua kinywa na baada ya kumaliza kupata chai nikaelekea kwenye maduka ya wachaga yaliyopo barabara za namba na kazi yangu ikawa ni kutafuta ni nguo gani ninaweza kuzinunua na kuzivaa na zikabadilisha muonekano wangu kabisa.Hadi mwisho wa mizunguko yangu nikajikuta nikinunua overol jeusi pamoja na kofia kubwa na kurudi nyumani kwangu mida ya saa kumi na moja jioni.Nikapanda kitandani na kulala huku saa yangu ya mkononi niiitega muito wa kunistua saa nne usiku.
 
Kama nilivyo itega saa yangu ndivyo ilivyo niamsha nikanyanyuka kitandani na kuingia bafuni na kunawa uso ili kutoa uchovu kisha nikarudi  ndani na kuvaa overoli langu na pamoja na kofia,Nikatafuta mabuti yangu ya mvua kisha nikavaa,nikazichukua karatasi nilizo chora ramani ya nyumba ya kina Rahma na kuanza kuipitia moja baada ya nyingine.Nikachukua beki langu dogo na lenye vijimikanda vyembaba na kulivaa mgongoni huku likiwa ni vifaa kama koleo,bisibisi na nyundo
Kabla sijafungua geti langu nikasikia likigongwa taratibu na kunifanya nistuke,likarudiwa kugongwa na taratibu nikapiga hatua za taratibu huku nikiwa na tahadhari kubwa na nikacjungulia nikaona gari aina ya ‘geap’ lililo kibanda wazi na ni kama magari ya jeshi likiwa limesimama nje ya geti langu.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio ila nikapata ujasiri wa kufungua geti na kumkuta mzee ngoda akiwa amevalia nguo za jeshi huku mkononi mwake akiwa ameshika begi la wastani
 
“Eddy ndio umevaa nini hivyo?”
“Ehee ndio mavazi ninayokwenda kumuokoa mpenzi wangu”
“Kijana hembu acha uzembe tuingie ndani”
Tukarudi ndani na geti tukalifunga kisha tukaingia sebleni na akalifungua begi lake na akatoa nguo za jeshi na kunirushia
“Kamata hizo uangalie kama zinaweza kukutosha”
Nikaanza kuzitazama moja baada ya nyingine na nikalivua overoli langu na kuva nguo alizo nipa mzee ngoda na kwabahati nzuri zikawa zinanitosha vizuri kuanzi suruali hadi shati la juu.Pia akanikabidhi viata vya jeshi japo vinanibada kidogo ila vimekaa vizuri mguuni mwangu,akanikabidhi begi nilibebe na nikaona kamba pamoja vifaa vingine ambavyo sikujua matumizi yeke ni nini
“Unaweza kutumia bunduki ya aina yoyote au ulisha zoea manati za uwindaji wa ndege huko kwenu Morogoro?”
“Ahaaaa sijawahi mzee wangu”
“Eddy hilo jina lako la mzee silipendi”
 
“Hhaaaa haya baba”
“Hapo kidogo sawa na mtu unapokuwa umevaa hizo nguo niite kamanda”
“Ndio kamanda”
“Ahaa hapa kuna hiizi bastola tatu nimekuja nazo moja inatumia risasi baridi na hizi mbili zinatumia risasi moto….Hii ya risasi baridi itakulazimu ukae nayo wewe na hizi nyingine nitakaa nazo mimi sawa”
“Sawa kamanda..je nikitaka kufyayua risasi ninafaje?”
“Unashika hapa na unaparudisha nyuma na unakuwa risasi umeipandisha kwenye chemba na ukiminya hapa unairuhusu kuchomoka kuelekea kule ulipo iagiza kwenda”
“Sawa nimekuelewa kamanda”
“Vaa kofia yako na ninaomba hizo karatasi unazosema umechora ramani ya hiyo nyumba”
Nikamkabidhi karatasi zote na akaanza kuzipitia moja baada ya nyingine hadi akazimaliza zote
“Kumbe wewe ni mtaalamu mzuri wa kuchora ramani?”
“Ehee kidogo kidogo  ninajaribu”
“Ina bidi nikupeleke kambini wakakuajiri kwa kazi hii kwa maana wa taalamu kama nyinyi ni wachache sana”
“Ukiachilia kuchora ramani hata kuchora watu au vitu Mungu amenibariki sana kwenye hilo”
 
“Ahaa wewe utalifaa jeshi ngoja kwanza twende nikakuone ufanisi wako wa leo”
Tukatoka nje na kuingia ndani ya gari na nikawa na kazi ya kumuelekeza ni wapi tunapaswa kufika na ndani ya dakika kadhaa tukawa tumefika nje ya jumba kuwa la kina Rahma.Mzee Ngoda akashuka na kuniacha mimi ndani ya gari na akaanza kulichunguza vizuri na akaingia ndani ya gari tukaondoka na gari tukaenda kuisimamisha kwa mbali kidogo na tukarudi hadi ilipo nyumba ya kina Rahma kisha akiitoa bastola yeke na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti kisha akaniomba nikae nyuma yeke nimfwate kila anapo pita.Cha kushangaza sikujua hata uogoa nimeutoa wapi kwani nikajikuta mwili mzima ukinitetemeka kiasi kwamba hata kutembea kwenyewe nikawa ninayumba nyumba.Tukafika kwenye ukuta mrefu kidogo na nikamshangaa mzee Ngoda akijirusha juu na kuishika sehemu ya juu japo ni mfupi ila mwenzangu ameweza kufanya hivyo
 
Kazi ikaanza kuwa kwangu kila nilipo karibu kujirusha kupafikia nikawa ninashindwa na kuishia kuburuzika ukurani
“Sikia wewe ukitaka kuruka hakikisha mguu wako wa kulia unakanyaga ukuta na kujirusha juu sawa”
“Sawa”
Nilijibu kama nimeelewa vile wakati sikujua hata nifanye nini,Nikajaribu kujirusha mara kadhaa hadi nikafanikiwa ila mikono yangu ikijaa michubuko mingi.Mzee Ngoda akawa wa kwanza kuingia ndani na mimi nikafwatia na sehemu tuliyo shuka ina maua mengi na taratibu tukajificha kwenye maua
 
“Mkango wa kuingilia upo wapi?”
“Kwa mbele”
“Kuwa makini na kuna walinzi wangapi?”
“Mmmm wala sifahamu”
Tukaanza kwenda kwa mwendo wa tahadhari huku mimi mara kwa mara nikitazama nyuma na tukafanikiwa kuingia hadi sebleni na kuwakuta watoto wadogo wakitazama filamu za kumi kwenye Tv kubwa humu sebleni.Tukapiga hatua za kimya kimya hadi sehemu waliyo kaa na walipo tuona mmoja akajaribu kupiga kelele ila Mzee Ngoda akamzaba kofi zito hadi mtoto wa watu akazimia na wengine walio ona hivyo hakuna aliye dhubutu kufungua kinywa chake
“Baba yenu yupo wapi?”
Mzee ngoda aliuliza kwa sauti ya ukali ila ni ya chini sana ambayo watu tuliopo kwenye eneo hili ndio tunaweza kuisikia.Mtoto mmoja wa kike akanyoosha mkono gorofani akimaanisha kwamba yupo chumbani kwake na hapo ndipo nikaamini kuwa pesa ina fanya kazi kwa maana askari walisikia juu ya mauaji yangu na kwa kawaida mtu akiwa amefanya kosa kama hili ni lazima kwanza ashikiliwe kwa muda kadhaa japo kuna kitu cha dhamana ila baba Rahma hakupaswa kupewa dhamana ya aina yoyote
 
“Hakikisha ngedere yoyote apanui domo lake”
Mzee ngoda alizungumza huku akianza kupanda ngazi akielekea juu gorofani na mimi nikawa nimewanyooshea watoto bastola yangu yenye risasi baridi ambazo hazina uwezo wa kumuua inadamu.Baada ya dakika kama tano nikaona baba Rahma akiwa na mke wake pamoja na ndugu wengine wakiwa wanashuka kwenye ngazi huku mikono yao wakiwa wameinyoosha juu kama mateka.Akawaamuru kupanga mstari mmoja huku wakiwa wamepiga magoti pamoja na mikono yao ikiwa juu.Macho ya baba Rahma pamoja na shangazi Rahma yakawa na kazi ya kunitazama kwa mshangao huku kila mmoja akiwa haamini kama ni mimi ndie nimesimama mbele yao tena nikiwa nimevalia nguo za jeshi
“Nenda kamtoa Rahma ndani kwake na umlete hapa”
Nikafanya kama mzee ngoda alivyo niagiza na kwa tahadhari kubwa na mimi nikazipandisha ngazi hadi chumbani kwa Rahma na kumkuta akiwa amelala pamoja na Hilda.Nikaigeuza kwa nyuma kofia yangu ya jeshi niliyo ivaa na nikamshika shavuni Rahma na akaanza kupepesa macho akihisi kama mdudu ndio anamtambalia
“Rahma”
Nikaita na akafumbua macho yake na kunitazama kwa muda na akastuka kidogo kuniona ila kabla hajazungumza kitu nikamziba mdomo
 
“Ni mimi Eddy nimekuja kukuchukua mpenzi wangu wa maisha”
“Kweli Eddy”   
“Ndio ninakuomba twende pamoja mbali na hapa mpenzi wangu”
Nikamuona Hilda akinyanyuka na kwa haraka nikamnyooshea bastola yangu na alipo niona ni mimi akawa kama anawewesekea kwa woga ulio changanyikana na uwoga
“Nyanyua mikono yako juu kabla sijakufyatua huo ubongo wako”
Akatii na kwaishara nikamuamuru kushuka kitandani na anyooshe mikono yeka juu na atangulie mbele,Rahma akashuka kitandani huku akiwa amevalia gauni jepesi linalo muonyesha nguo yake ya ndani.Kisha nikamshika kiuno kwa mkono mmoja huku mwengine ukiwa umeishika bastola nikimuelekezea Hilda ambaya gafla akachomoka haraka huka akupiga kelele za kuomba msaada na nikamaucha akimbie huku akishuka kwenye ngazi na kukutana na mzee ngoda akiwa ameshika bastola na kumnya kasi yote kumuishia kweye ngazi
“PITA HUKU KWA WAJINGA WEZAKO”
Hilda taratibu akapita kwa wezake na kufanya kama walivyo fanya huku akiwatazama watu waliopo kwenye adhabu hii.Rahma akaniendelea kunikumbatia huku akiwatazama wazazi wake kwa macho makali 
 
“Baba na Mama……najua siku zote kwamba mulifanya njama za kila namna ili nisiweze kuwa na Eddy…ila tambueni kuwa sijali kama yeye ni mtu mweusi au anapesa au hana pesa mimi nimemkubali jinsi alivyo…”
Rahma alizungumza kwa sauti ya kufoka na yenye uchungu na kwafanya wazazi na ndugu zake kubiki wakimtazama pasipo kujibu kitu cha aina yoyote.Kwa kuwadhiirishia wazazi wake na ndugu zeka akanishika midomo yangu na kuinyonya kama dakika mbili kisha akawageukia ndugu zake.
“Japo baba ulijaribu kumuua Eddy kwa kumpiga risasi ila ikanipata mimi nakuufanya ujauzito wangu kutoka ila ukweli ni kwamba ana uwezo wa kunizalisha tena na tena na tena na tukawa na watuto wafamilia kubwa “
Nikamuona baba Rahma akitemeka kwa hasira huku macho yake yakiwa mekundu kupita maekezo,kwa upande wa mama Rahma nikayashuhudia machozi yakimwagika huku akitetemeka kwa uchungu kwani hawakuamini kama mtoto wao ndio anaondoka mbele ya macho yao
 
“Eddy hembu fungua begi unitolee redio ndogo”
Nikafanya hivyo na kufungua na kukuta kijiredia kidogo kinacho tumia kanda na kimetengenezwa na kampuni ya Panasonic.Mzee Ngoda akakiwasha na kuminya kitufe cha rangi ya kijana kilicho andikwa ‘record’
“JE UMEKUBALI KUMUUOZA MWANAO RAHMA KWA BWANA EDDY?”
Mzee Ngoda alimuuliza baba Rahma huku bastola ikiwa juu yakichwa  cha baba Rahma ambaye bila ubishi akajikuta akijibu
“Ndio nimekubali”
“Je Rahma umekubali kuolewa na Eddy?”
“Ndio nimekubali tena sana”
“Na wewe Eddy umekubali kumuoa Rahma”
“Ndio nimekubali”
“Je mama Rahma umekubali binti yako aolewee na Eddy”
“Ndio nimekubali”
“Wanandugu wote wajomba mashangazi na mababu je mumekubali mtoto wenu Rahma kuolewa na Eddy?”
 
“Ndioo”
Walijibu kwa sauti za unyonge japo ndio hivyo wamekubali kwa kulazimisha.Akairudisha nyuma tepu iliyo kuwemo ndani ya redio hiyo kisha akaisikiliza na sauti zikawa zimeingia vizuri,akaizima redio na kuiingiza mfukoni mwake.
“Toa kamba na kisu ndani ya begi”
Nikatoa kamba ina ya manila pamoja na kishu kisha akawaamuru wote kulala chini na idadi yao wapo kumi na nne.Nikaanza kuwafunga kamba mmoja baada ya mwengine na mtu wa mwisho kummalizia kumfunga ni Baba Rahma ambaye akaanza kuleta ubishi nikatandika kofi moja la usogo akatulia,hasira ikaanza kunipanda na nikaikumuka siku alipokuwa akinitesa  ikanilazimu na mimi kumhindilia mateke mawili ya makalio baada ya kumaliza kumfunga kamba
“Jamani asanteni kwa ushirikiano wenu mulio tupa sawa”
“Samani jamani ngoja kuna kitu ninataka kwenda kuchukua ndani mara moja”
“Dakika mbili zinakutosha”
Rahma akapandisha ngazi na kurudi akiwa amevalia suruali ya jinzi pamoja na sweta lenye kofoa na akamfwata mdogo wake mmoja wa kike ambaye kwa makadirio ana miaka kama mitatu akambusu na wakazungumza kiarabu na tukaondoka.Tukamkuta mlinzi getini akiwa amesinzia na alipo stuka na kumuona Rahma akanywea
 
“Wewe una kazi ya kulala lala?”
“Ahaa ni ni samehe dada Rahma”
“Nyoo ingia ndani  ya kibanda chako”
Mlinzi akaingia na Rahma akamuomba funguo za geti kisha akamfungia mlizi kwa nje na kabana mlango kwa kufuli kisha tukaondoka.Tukaingia ndani ya gari huku saa yangu ikinionyesha ni saa saba usiku na tukaanza kuelekea katika njia ya Horohoro inayoelekea mpakani mwa Kenya na Tanzania.Mzee Ngoda akakunja kushoto na tukaingia kwenye barabara ya vumbi na safari ikaendelea na tukavipita vijiji kama vinne na katikati yam situ Mzee Ngoda akasimamisha gari na sote tukashuka
Mzee ngoda akanza kumtazama Rahma kwa macho ya kuiba kuanzia juu hadi chini na kwa jinsi Rahma anavyo nikumbatia kumbatia nikamuona kabisa mzee Ngoda akiumia moyoni mwake kwani ikafikia kipindi hadi sura yake ikawa inajikunja na kitu kinacho nikaanza kunipa wasiwasi.Gafla tukastukia akiichomoa bastola yake na kutonyooshe sisi na Rahma na kwastory nilizo wahi kuzisikia mtaani kweni ni kwamba huyu mzee anatabia ya kutembea na wasichana wadogo japo sikuwahi kumshuhudia na kwa story nyingine nilizo zipata mtaani ni kwamba alimuua mke wake kwa kumpiga rasasi baada ya kufumaniwa akiwa na binti mdogo

 ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts