Home » , » “Tuolewe na Wazee Watufie?” - Riyama na Uwoya Kuhusu Kuolewa na Viben- 10

“Tuolewe na Wazee Watufie?” - Riyama na Uwoya Kuhusu Kuolewa na Viben- 10

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 11:27:00 AM

Muigizaji wa Bongo movie Riyama Ally amefunguka kuhusu kuolewa na mwanaume ambaye ni mdogo kwake kiumri ambapo amesema haoni tatizo na pia kuhusu Irene Uwoya kuolewa na Dogo Janja amesema ndio vizuri waolewe na wazee wawafie?.

Riyama Ally ameolewa na Mwanamuziki wa Bongo fleva anayejulikana kama Leo Mysterio ambaye kiukweli kabisa ni kiben10 kwake kwani ana umri mdogo kuliko yeye jambo ambalo Riyama amesema ndio anapenda hapendi wazee.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Millard Ayo Tv, Riyama amefunguka na kusema kwamba haoni tatizo kuwa na mwanaume mdogo na hata alipoulizwa kuhusu rafiki yake Irene Uwoya kuolewa na kiben-10 Dogo Janja amedai ndio vizuri kutafuta kijana.

Kwenye mahojiano hayo Riyama alisema mambo haya:
"Mimi nimempa ushauri Irene kama dada yake na rafiki yake nikamwambia kaza hapo hapo kwenye ndoa yako usilegeze maneno yatasemwa sana kama mimi ninavyosemwa kuolewa na Mume wangu niliyemzidi umri kwa sababu mapenzi furaha bwana kama furaha yako ipo hapo basi inatosha kwanini tukatafute wazee waje watufie ndani?”.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts