Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 73 na 74 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 73 na 74 )

Written By Bigie on Sunday, April 1, 2018 | 4:19:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
0657072588

ILIPOISHIA   
Livna aliendelea kuzungumza naneno ambayo yalizidi kukasirisha Mariam ambaye ninatambua kwamba ana nipenda. Taratibu Mariam akapiga hatua mbili mbele  na kuniacha mimi nyuma.
“Mari…..”
Kwa jicho alio nitazama nalo Mariam nilijikuta nikinyamaza kimya, Mariam akaachia msunyo mkalia na kumsogelea Livna sehemu alipo simama.
“Sipambani kwa ajili ya huyu mwanaume, ila ninapambana kwa ajili ya uhuru wangu”
Mariam baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, akamtandika Livna kichwa kizito cha pua, na kumfanya ainame chini huku akitoa mlio wa maumivu, kitendo kilicho pelekea wasichana wota hawa kuanza kutushambulia kwa hasira kali.

ENDELEA
Nikazidi kujitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha ninawahimili hawa wasichana wenye mafunzo makubwa ya kupambana, kila nilivyo jaribu kadri ya uwezo wangu, nilijikuta nikishindwa kabisa, kipigo ambacho ninakipata mfululizo kikanifanya taratibu kuanza kuishiwa nguvu na kuanguka chini, kwa macho yaliyo jaa ukungu wa damu inayo nimwagika kutoka kwenye baji la uso baada ya kuchanwa na kitu chenye makali, nikamuona jinsi Mariam naye akipokea kipigo kikali hadi akaanguka chini na kuulia kimya. Msichana moja pasipo kuwa na huruma, akanikanyaga kichwani mwangu kwa kiatu chake chenye ncha kali na kujikuta giza jingi likinitawala kwenye mfumo wa kuona, taratibu mawasiliano ya ubongo na mwili yakakatika.
                                                                                                          ***
    Mlio wa mashine ambayo sifahamu ni mashine ya nini, nikaanza kuisikia kwenye masikio yangu. Taratibu nikafumbua macho yangu, ukungu mzito uliopo kwenye macho yangu sikuweza kuona chochote katika chumba hichi, nikazidi kujitahidi kuyafumbua macho yangu, kwa sekunde kadhaa nikaanza kuona baadhi ya vitu ambavyo taratibu nikaanza kuvigundua kwani si mara yangu ya kwanza.
Taa mbili za mwanga mweupe zilizo juu ya chumba hichi, zikanifanya niweze kuyaona mandhari ya chumba hichi ambacho nimegundua ni hospitalini.
Mashine ya kugemea iliyopo pembeni yangu iliyo unganishwa na mtungi wa hewa ya oksijeni, vikazidi kunihakikishia kwamba eneo nililopo ni hospitalini. Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo macho yangu yalivyo weza kuona mandhari ya chumba hichi ambacho sijamuona mtu yoyote.
Nikiwa katika hali ya kufukiria ni kitu gani kilicho pelekea mimi kuwa katika hali hii, mlango wa hichi chumba ukafunguliwa na akaingia nesi wa kike aliye valia mavazi meupe ya kupendeza.
 
“Karibu duniani”
Nesi huyo alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Nipo wapi?”
“Upo sehemu moja isiyo na jina”
“Isiyo na jina?”
“Yaa ila mimi sio mzungumzaji mkubwa katika hilo, ila yupo ambaye atazungumza”
Nesi huyo akatoka chumba humu, huku kwa mara kadhaa akinitazama kitandani nilivyo laa. Nesi huyu mwenye asili ya kiafrika amenifanya nianze kuwaza mambo mengi sana akilini mwangu, na kitu kingine ambacho kinanichanganya ni yeye kuwa na uwezo wa kuzungumza Kiswahili. Nikaendelea kulala kwenye hichi kitanda huku nikitafakari mambo mengi sana kwenye maisha yangu. Baada ya lisaa moja akaingia mwana mama mrefu aliye valia gauni jeusi pamoja viatu virefu. Ana umbo lililo jengeka vizuri kwa mazoezi huku makalio yake ni makubwa kiasi. Akatembea kwa hatua za taratibu hadi pembeni ya kitanda changu, huku akinitazama usoni mwangu akiwa na tabasamu pana.
 
“Habari yako kijana”
Mama huyu alizungumza kwa Kiswahili fasaha kabisa hadi mimi mwenyewe nikabaki nimemkodolea macho tu.
“Habari yako kijana?”
“Ahaa salama tu”
“Kwanza nina furaha kukuona ukiwa upo hai”
Mama huyu alizungumza huku  akivuta kiti na kukiweka pembeni ya kitanda, kisha akakaa huku ananitazama usoni.
“Hapa ni wapi?”
“Upo Afrika kusini”
“Afrika kusini!!!!”
Nilijikuta nikishangaa, nikajaribu kukaa kitaki kitandani ila nikajikuta nikiwa nimeshindwa kutokana na maumivu makali ya kichwa.
 
“Tulia tu kijana huna haja ya kunyanyuka hapo ulipo”
“Afri…afrika kusini nimefikaje?”
“Mmmm ni kiji stori kirefu, ila hali yako  ikitengemaa nitakuambia umefikaje?”
“Samahani mama yangu naamini nimetengemaa na ninajielewa, hembu nieleze nimefikaje Afrika kusini, ukiniambie hilo tu, mambo mengine yanaweza kufwata”
Mama huyu akashusha pumzi taratibu huku akivua kofia lake alilo livaa, akaliweka pembeni juu ya meza kisha akanitazama kwa macho yake makubwa kiasi na malegevu.
“Naitwa Matilda, ni mfanya biashara mkubwa hapa Afrika kusini, nina makampuni yangu ma…”
“Mama yangu hilo sio jibu la swali  langu, wewe nieleze nimefikaje hapa Afrika kusini?”
Ilinibidi kumkatisha mama huyu ambaye anaonekana kujizungumzia yeye mwenyewe kuliko kulijibu swali langu.
“Nilikuokota kwenye moja ya mtaro kule maeneo ya Soweto, ulikuwa hujitambui, na ulikuwa katika nusu ya kifo kwani mwili wako ulisha anza kutoa harufu kali”
 
Maeno ya Matilda yakanifanya nizidi kushangaa na kujiuliza mimi mwenyewe, ni kitu gani kinacho endelea. Matilda, akatoa simu yake, akaminya minya na kuweka upande video na kunikabidhi niione video hii. Mwili ulio  lala kwenye mtaro unao onekena kwenye video hii iliyo rekodiwa na simu ni mimi mwenyewe, nimelala nikiwa na suti yangu ambayo imechafuka, kichwa changu kimelowana damu nyingi na kwa jinsi nilivyo lala kifudi fudi, hapakuwa na mtu wa kunigusa wala kunisaidia. 
 
“Nilipo fika katika eneo hilo, nilimuagiza kijana wangu kukugeuza na kukutazama kama upo hai, alipo kukuta upo hai, ikanibidi kuweza kukuwahisha hospitalini hapa, madaktari wakajitahidi kadri ya uwezo wako  na wakafanikiwa kuyaokoa maisha yako”
Nilihisi mwili mzima ukizizima, baada ya kumaliza kuitazama video hii, nikamkabidhi Matilda simu yake na kuanza kufikiria ni kitu gani kilitokea baada ya kupigwa na wale wasichana. Japo hapo katikatis ikumbuki kitu chochote ila swali jengine linalo niumiza akilinini inakuwaje tukio lifanyike Korea na mwisho wa siku nije kutupwa Afrika kusini.
 
“Nilifurahi sana kukusikia unazungumza kiswahili kwa maana mimi mwenyewe ni mswahili, japo asili yangu ni Kenya ila mama yangu ni Mtanzania”
Matilda alizungumza kuzidi kujitambulisha, kwangu hilo wala halikuwa swala la muhimu kwa wakati huu, maumivu ya kichwa na mawazo yakaanza kupelekea hadi damu za puani zikaanza kutoka. Matilda kwa haraka akawaita madaktari, walio ingia kwa kasi katika chumba hichi na kuanza kunihudumia kwa kunichoma sindano za kupunguza maumivu na sindano ya pili waliyo nichoma ikanifanya ukungu ulio kuwa umetawala awali machoni mwangu kurudi tena na usingizi mzito ukanipitia.
                                                                                                          ***
    Nikazinduka kutoka usingizini, nikamkuta Matilda akiwa amelaza kichwa kwenye kitanda changu huku akiwa amekalia kiti alicho kuwa amekali. Nikamchunguza vizuri, mavali  aliyo kuwa ameyavaa kwa mara ya kwanza ni tofauti na haya aliyo yavaa hivi sasa. Nikausogeza mkono wangu wa kulia hadi kwenye mashavu yake, sikusita kuyashika na kuanza kuyapapasa, jambo lililo mfanya Matilda kuyafumbua macho yake.
 
“Umeamka?”
Alinniuliza kwa sauti ya upole iliyo jaa wenge la usingizi.
“Ndio habari yako?”
“Salama”
Matilda alizungumza huku akikaa vizuri, akakaushika mkono wangu wa kulia nilio kuwa nimempapasa shavuni mwake.
“Ni siku yangapi  tangu nilale?”
“Ni masaa kama ishirini hivi, siku haijakamilika”
“Madkatari wamesema ninasumbuliwa na nini?”
“Watatupa majibu baada ya hali yako  kuwa vizuri, kwa sasa hivi hata mimi hawaja niambia”
“Ahaa sawa”
Katika kuichunguza mikono ya Matilda, katika kidole cha kiganja cha mkono wa kushoto nikaona pete ya ndoa. Jambo hilo Matilda akaligundua kwa haraka sana baada ya kuyaona macho yangu yameganda kwenye hiyo pete.
“Nimeolewa”
Matilda alizungumza huku akitabasamu, ikanibini na mimi kutabasamu. 
 
“Hongera”
“Asante, ila nd…….”
Matilda hakumalizia sentensi yake mlango ukafunguliwa kwa nguvu, akaingia mwanaume mwenye upara alite jazia misuli, paji la uso wake limejaa mistari ya hasira, kwa haraka Matilda akaniachia kiganja changu. Mwanaume huyo akanitazama kwa macho makali yaliyo jaa hasira. Akaanza kutembea kwa haraka akihitaji  kunifwata kitandani, ila Matilda kwa haraka akasimama na kumzuia mwanaume huyu huku wakizungumza lugja ya Kizulu. 

Mwanaume huyu kwa hasira akamtandika kofi zito Matilda lililo mfanya kuangukia kwenye miguu yangu kitandani. Kabla mwanaume huyu mwenye hasira hajanifikia, Matilda akamzuia tena huku akizungumza akionekana kumuomba asinifanye chochote huku machozi yakimwagika. Mwanaume huyu akamkaba koo Matilda huku akiwa amemgandamiza kwenye ukuta, cha kumshukuru Mungu, askari wanne wenye vifaa vya shoti ya umeme mikononi mwao wakaingia na kuanza kumkandamiza navyo mwanaume huyo vya mgongo na kumfanya amuachie Matilda aliye jikuta akikaa chini pasipo kupenda, na wakafanikiwa kufunga pingu mikononi mwake.
 
Wakamtoa mwanaume huyo aliye endelea kuzungumza maneno ya hasira huku kwa mara kadhaa akinitazama kwa ukali sana.
“Dany pole sana”
Matilada alizungumza hukua kinyanyuka kwa hasira, akanifwata nilipo lala na kuanza kunitazama kwenye miguu yangu kama kuna sehemu nimeumia au laa.
“Sijaumia ila pole na wewe”
“Ohoo Mungu wangu nimechoka sasa na hii ndoaa”
Matilda alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, hapo ndipo nilipo gundua kwamba mwanaume huyu ni mume wake wa ndoa.
 
“Imekuwaje kwani?”
“Sifahamu Dany, ila huyu mwanaume ataniua sasa jamani, huu sio wivu ni ukatili”
Matilda alizungumza huku machozi yakimwagika. Nikatamani kumfuta machozi Matilda ila nina hofia mumewe anaweza kurudi muda wowote na kama akitukuta kwenye hali hiyo basi nitambue kinacho fwata hapo nitauliwa kwa maana sina uwezo wa kufanya kitu chochote hapa kitandani kutokana bado sijapona vizuri.
“Tena inabidi nikuhamishe hospitali araka iwezekanavyo”
“Kwa nini?”
“Dany nisikilize mimi, huyu mwanaume ni katili sana, ana pesa nyingi, anaweza kukufanya chochote hata kukuua kwa mikono yake mwenyewe. Hapendi mke wake mimi nisaidie watu hususani wanaume”
 
Matilda alizungumza huku akisimama, akapiga hatua hadi mlangoni, akachungulia nje akatazama nje kwa sekunde kadhaa, kisha akaufunga mlango na kupiga hatua hadi dirishani, akachungulia nje, kisha akatoa simu yake akaminya minya namba kadhaa na kuiweka simu sikioni. Akazungumza lugha ya Kizulu, alipo maliza akakata simu.
“Nimempigia dereva wangu wa siri, ambaye atafika hapa na gari la wagonjwa, nitakuhamisha hospitali”
“Kwa nini unanifanyia yote haya wakati unafahamu mume wako haitaji ufanye vitu kama hivi?”
“Dany hilo swali kwa sasa kwangu sio muhimu, nahitaji tufanye hichi nilicho kisema.”
Matilda akatoka chumbani huku na kuniacha nikiwa katika maswali mengi huku nikiwa nimejawa na woga wa kujiuliza endapo mumewe atafika wakati huu nikiwa peke yangu hivi itakuwaje.
 
Baada ya dakika tano Matilda akarudi akiwa ameongozana na madaktari wawili, akazungumza nao lugha ya kizulu ambayo siielewei kitu chochote. Madkatari wakawa wanatingisha vichwa kuonekana wanakubaliana na kile ambacho Matilda anakizungumza. Walipo maliza kuzungumza Madaktari wakaanza kuniweka vizuri kwenye kitanda, dribu la maji wakalichomoa kwenye sehemu waliyo kuwa wamelining’iniza, daktari mmoja akalishika huku akiwa amelinyoosha juu kwa kutumia mkono wake wa kulia.
“Wanakupeleka kwenye gari la wagonjwa limeshafika, kuna hospitali inaitwa St Maria, ndipo wanapo kupelekea, mimi ngoja nikamalizane naye huyu mwanaume kisha nitakuja kuuangalia muda wowote”
“Asante sana Matilda kwa msaada wako”
“Usijali Dany, nilicho kifanya kwako ni  kidogo sana”
“Hapana kuyaokoa maisha yangu, wakati nilikuwa nusu mfu, ni jambo  la kukushukuru sana dada yangu”
 
“Asante Dany ila mwenyezi Mungu ndio msaada wa kila kitu. Kule yupo sister mmoja anaitwa Matlda naye ndio atakupokea na kila kitu atakuafanyia”
“Shukrani”
Matilda akanipa mkono wa kulia kama ishara ya kuniaga, na mimi nikampa mkono wangu wa kulia, tukatazamana machoni kwa sekunde kadha, na kumfanya Matilda kumwangikwa tena na machozi, akanichia mkono wangu na kuelekea dirishani na kuangalia nje na kuniachia mkono. Kwa ishara akawaomba madaktari hawa kunitoa ndani ya hichi chumba na ndivyo madaktari walivyo anza kufanya. 
 
Kwenye kordo hii ndefu, ninapishana na watu wengi, wengine wakiwa na afya mgogoro, wengine wakiwa wamekuja kuwatazama wagonjwa. Tukaingia kwenye lifti huku nikiwa nimelala kwenye kitanda changu. Hapo ndipo nilipo gundua kwamba nilikuwa gorofa namba kumi. 

Taratibu tukaanza kushuka chini huku sote tukiwa kimya kwenye hii lifti. Ilipo fika chini, ikajifungua na madaktari wakaanza kukisukuama kitanda changu chenye matairi hadi kwenye maegesho  ya magari, wakaninyanya na kuniingiza kwenye gari la wagonjwa ambalo lina kitanda chake, humo ndani ninakuta madaktari wawili mmoja akiwa wa kiume na mwengine wa kike. Wakanipokea na kuufunga mlango, tukaondoka eneo hili la hospitalini, huku madaktari hawa wakinihudumia huduma ndogo ndogo.
 
    Ukimya ukaendelea kutawala hapakuwa na mtu aliye zungumza na mwenzake. Ila katika  kuchunguza hawa madaktari, huyu nesi wa kike nikamuona ana tattoo kama ya mume wa Matilda kwenye mkono wake wa kushoto jambo lililo anza kunipa wasiwasi, nikamgeukia daktari huyu wa kiume wala sikuona kama ana tattoo yoyote kwenye mkono  wake. Gafla daktari huyu wa kike akatoa bastola yake iliyo fungwa kiwambo cha kuzuia sauti akampiga daktari wa kiume ya kichwa na kumfanya afariki hapo hapo. 

Daktari huyu wa kike akavua wigi la nyele nyeusi alizo kuwa amezivaa na kubakiwa na mwele za rangi ya dhahabu. Nikajaribu kujiokoa misha yangu kwa kumshika japo mkono wenye bastola, ila sikuwa na guvu ya kupambana naye kwani alinitandika ngumi moja ya kifua iliyo nifanya nijisikie maumivu makali sana, akachukua sindano iliyo jaa dawa kwenye bomba lake na kunichoma shingoni na hapo hapo nikazidi kulegea na kupitiwa na usingizi mtizo tena.
                                                                           
AISIIIII……….U KILL ME 74                                                                                                   

Gafla daktari huyu wa kike akatoa bastola yake iliyo fungwa kiwambo cha kuzuia sauti akampiga daktari wa kiume ya kichwa na kumfanya afariki hapo hapo. Daktari huyu wa kike akavua wigi la nyele nyeusi alizo kuwa amezivaa na kubakiwa na mwele za rangi ya dhahabu. Nikajaribu kujiokoa misha yangu kwa kumshika japo mkono wenye bastola, ila sikuwa na guvu ya kupambana naye kwani alinitandika ngumi moja ya kifua iliyo nifanya nijisikie maumivu makali sana, akachukua sindano iliyo jaa dawa kwenye bomba lake na kunichoma shingoni na hapo hapo nikazidi kulegea na kupitiwa na usingizi mtizo tena.
       
ENDELEA       
    Kama ilivyo kuwa awali nilivyo kumbwa na ukungu mwingi katika macho yangu ndivyo jinsi ilivyo hivi sasa kila kitu kilichopo mbele yangu ninajionea mauza uza, hata watu walio simama mbele yangu siwezi kuziona sura zao vizuri. Masikio yangu yanasikia kile wanacho kizungumza ila kukielewa ndio shida kwani lugha wanayo itumia ni Kizulu ambacho niliwahi kukisikia katika tamthjilia moja ya kiafrika Kusini inayo itwa Isidingo.
 
Maji mengi na ya baridi niliyo mwagiwa mwilini mwangu yakanifanya nitetemeke kwa baridi hata ukungu uliopo machoni mwangu wote ukatoweka. Wasichana wanne wamesimama mbele yangu wakiwa wamevalia mavazi ya kijeshi huku kila mmoja kiunoni mwake akiwa amechomeka bastola yake, kusema kweli haya mazingira yanaogopesha sana kwa maana yana taa moja kubwa inayo toa mwanga mkali ndani ya chumba hichi ambacho kuta zake zimechakaa kupita maelezo. Binti mmoja aliye simama pembeni ya ndoo ambayo ninaamini ndio iliyo kuwa na maji aliyo nimwagia mimi mwilini mwangu, akanisogelea karibu yangu katika kiti nilicho kikalia huku nikiwa nimefungwa kamba ngumu katika hichi kiti na sina uwezo wa kufanya kitu chochote hata kuusogeza mguu wangu mbele siwezi.
 
Akanishika kidevu changu kwa kiganja cha mkono wake wa kushoto, akanitazama uso wangu vizuri huku akiwa ameusogeza uso wake karibu kabisa na uso wangu, Macho yake makubwa kiasi ambayo anajua kuyatoa kwa kumuogopesha mtu hata mimi yakaniogopesa kuyatazama.

    Wakazungumza maneno ambayo sikuyaelewa kabisa kisha akarudi kusimama pembeni ya kindoo chake. Mlango wa chuma ndani ya hiki chumba ukafunguliwa, akaingia mzee mmoja wa kizungu mwenye ndevu nyingi nyeupe pamoja na nywele zilizo nyonyoka katika kichwa chake nazo pia zina rangi nyeupe kutokana na uzee wake. Koti jeupe na miwani kubwa aliyo ivaa pamoja na kipima mapigo ya moyo alicho kining’iniza shingoni mwake, anaonekana kabisa kwamba huyyu mzee ni daktari. 

Akaweka kabegi kake kadogo mezani, akakifungua na kutoa gloves mbili nyeupe na kuzivaa. Kisha akachukua kijitochi kidogo sana na kunisogelea sehemu nilipo. Akanifumbua jicho la upende wa kulia akanimulika mulika na kijitochi chake kisha akanifumbua jicho la upende wa kushoto na kunimulika mulika na kijitochi hicho, alipo ridhika akarudi kwenye meza yake.
   
Mambo yote hayo yanayo fanyika hadi sasa hivi sielewi wana maana gani kunifanyia uchunguzi kwenye mwili wangu, sisitoshe sifahamu ni sehemu gani ambayo nipo. Daktari huyu akanisogelea akiwa na kipima mapigo ya moyo, akaniwekea kifuani na kusikilizia kwa muda, kisha akatingisha kichwa chake na kuwafanya wasichana hao kutazama kwenye nyuso zao kisha wakanitazama na mimi. 

Mzee huyu akarudi tene kwenye meza yake alipo kiweka kijibegi chake, akatoa mashine moja amnayo ndio mara yangu ya kwanza kuiona kwenye masisha yangu, akanisogelea sehemu nilipo kaa wasichana wawili wakanishika mkono wa kushoto huku mzee huyo akiiwasha sindano hii ambayo kwa mbele ina ncha ndogo kiasi. Jasho jingi lijanimwagika mwilini mwangu, sikukuja dhamira yao ya kunishika mkono tena kwa nguvu ni nini.

Mzee huyo akanyanyua mashine hiyo taratibu na kuniwekea kwenye mkono wangu wa kushoto kisha akanichoma kitu kilicho ingia kwenye mwili wangu na kunisababishia maumivu makali sana. Mzee huyo akarudi mezani mwake huku wasichana hawa wakiendelea kunishika mkono wangu kwa nguvu zao zote. 

Mzee huyo akarudi na sindano maalumu za kushona ngozi za binadamu ikiwa na uzi wake. Akaanza kunishota taratibu kisha akaninifunga bandeji ambalo ndani ya muda mchache likawa gumu sana. Wasichana hawa wakaniachia mkono wangu, mzee huyu ambaye ni daktari akaanza kurudisha vitu vyake kwenye kabegi kake, akakafunga na kuondoka zake na kuniacha na wasichana hawa wa kiafrika kusini. 

Msichana mmoja akatoka akaniacha na wezake ambao wanaendelea kuzungumza mazungumzo yao ambayo hadi muda huu sijaelewa chochote. Msichana huyo akarudi akiwa ameshika nguo za rangi ya chungwa pamoja na tisheti.  Akanirushia mbele yangu pasipo kuzungumza chochote, kwa ishara akamuamuru mwenzake kujifungua kamba walinzo nifunga. Kwa umakini mkubwa mwenzake huyo akanifungua kamba zote na nikabaki huru.

Wakanilazimisha kuvua nguo zangu, na kuniamuru kuvaa nguo walizo niletea, kutokana ni eneo ambalo silifahamu, ikanilazimu kuwa mpole na kukubali kuvua nguo zangu mbele yao na kuvaa nguo walizo niletea japo wote hakuna hata mmoja aliye pepesa jicho lake pembeni, walinitazama maungo yangu kwa kunikazia macho. Nilipo maliza, wakaniamuru kunyoosha mikono yangu mbele, nikafanya hivyo, msichana mmoja akanifunga pingu, kisha mwengine akanifunga nyororo ndefu kwenye miguu yangu ambayo ipo peku  peku. 

Wasichan wawili wakatangulia mbele na wengine wawili wakafwata nyuma na mimi nipo katikati. Tukaanza kutembea kuelekea mlangoni, lango hili la chumba likafunguliwa na sote tukatoka na kuanza kutembea kwenye kordo ndefu ambayo ina taa zenye mwanga hafifu pamoja na kamera za ulinzi. Kila sehemu ambayo ninapita nikajaribu kuhakikisha kwamba ninaitazama vizuri hata hapo mbeleni nitaamua kutoroka basi iniwie urahisi katika kuikamilisha dhamira yangu hiyo.

Mlamgo mkubwa ulipo mbele yetu ukafunguliwa. Masikio yangu yakakumbana na makelel ya watu wengi sana, jambo lililo nistua zaidi ni jinsi nilivo ona watu hawa ambao ni wafungwa wakishangilia wapiganaji wawili waliopo uliongoni wanao mwagikwa damu nyingi kutokana na kujeruihana.
 
Gereza hili, ni kubwa sana na sehemu tuliyopo nimeanza kuigundua kwani ni kwenye mapango tena yaliyopo chini ya ardhi. Hii ni kutokana kila sehemu ya hili pango kumewekwa taa zenye mwanga mkali ambazo zinalifanya eneo zima kuonekana mchana. Wafungwa baadhi ambao wapo kwenye makukwaa yaliyo uzunguka uwanja huu wa mapambano ulio zungushiwa nyavu ngumu na za kuchoma choma. Wakaanza kunishangilia kwa shangwe kubwa, kusema kweli omba kusikia tu kwamba kuna mageraza ila usiombe kuingia magerezani. Kwani ndani ya gereza hili kuna wanaume wenye miili mikubwa sana, tena ya kujazia iliyo gawanyika gawanyika kutokana na mazoezi makali ya kunyanyua vyuma wanayo yafanya kwenye gereza hili.

Wengi wao wamejichora kwenye miili yao wengine wamejichora michoro ya kutisha hadi kwenye vchwa vyao ambavyo wamevinyoo nywele zote na kuvipaka mafuta mengi ya kumeremeta. Katika kulichunguza gereza hili sijaona askari wa kiume hata mmoja, askari wote ni wakike tena ni wanajeshi. Msichana aliye nifunga pingu za mikononi akanifungulia kisha mwazake naye aliye nifunga pingu za miguuni akanifungulia. Wakaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama eneo ambalo nikishuka ngazi nne kwenda nchini ninaingia kwenye viti vya wafungwa washangiliaji wa pambano hili.
Kushuka nikawa ninatamani sana, ila kila mfungwa ninaye gonganisha naye macho, alinifanyia kituko chake kwa ishara, wapo walio nionyeshea ishara ya kunichinja shingo yangu, wapo walio nionyeshea ishara ya vidole vya kati, wapo walio nionyeshea ishara za kunizomea, ili mradi kila mtu amefanya vitisho vyake.
   
Ni kijana mmoja tu wa kiarabu ambaye amekaa peke yake kwenye na kiti cha pembeni hakina mtu, akatabasamu na kuniita kwa ishara, ila kuna jamaa mmoja mwenye mwili mkubwa na ulio jaa michoro alipo mtazama kijana huyo tu, tabasamu lake alilo kuwa akinitazama nalo kikapotea usoni mwake na akajikausha kimya. Kwa ishara hiyo nikagundua kijana huyu anamuogopa jamaa huyu. Taratibu nikashuka kwenye ngazi hizi huku nikiwa makini sana kumtazama kila mfungwa aliye simama pembeni yangu. Nikafika katika sehemu alipo kaa kijana huyu wa kiarabu ambaye ni mnyonge na ana mwili mdogo mdogo na anavyo onekana ndio mnyonge kwa wote hapa.
Wafungwa baadhi nilio kaa nao karibu wakabaki wakiwa wananishangaa, jambo ambalo kwa haraka haraka nikahisi ni kutokana na ugeni wangu ndani ya gereza hili
“Do you know to speak Swahili language?”(Je unafahamu kuzungumza lugha ya Kiswahili?)
 
Nilimuuliza jamaa huyu huku nikimtazama usoni mwake.
“Ndio ninafahamu  japo sio sana”
“Ila unafahamu?”
“Ndio”
Sote tukabaki kimya baada ya kumuona mpambanaji mmoja kwenye ulingo kichwa cheke kikielea hewani baada ya kukatwa na jambia kali na mpinzania wake na kupelekea mauti hayo. Kilicho nishangaza zaidi ni jinsi watu walivyo nyanyuka katika viti vyao na kuanza kushangilia kwa shangwe nyingi sana, huku wengine wakitukana. Hata kijana huyu wa kiarabu naye akanyanyuka na kushangilia, ila ni mimi pekee tu ndio nimekaa kwenye kiti changu huku nikiuutazama mwili wa mpambanaji ambye dakika chake nilizo ingia hapa nilimuona akiwa anajitahidi kardi ya uwezo wake kumkabili mpiganaji mwenzake.
 
Kijana huyu akanikanyaga mguuni na kwa ishara akaniomba ninyanyuke nishangilie. Ila sikuhitaji kufanya kitu kama hicho, gafla nikatukia mtu akinisukuma mgongoni mwangu, laiti kama si mazoezi ninayo yafanyabasi ningeanguka na kuwakumba wafungwa wengine. Nikanyanyuka kwa haraka na kugeuka nyuma, nikakutana na mijamaa miwili iliyo jazia miili yao huku ikiwa imenikazia macho yaliyo anandamana na sura zilizo jaa mikonjo. Sikutaka kuwa mnyonge kivile, na mimi nikakaza macho yangu pamoja na sura, kama ubabe ni ubabe tu.

Jamaa moja likanisukuma, nikarudi nyuma hatua chache kidogo na mimi nikajivuta na kumsukuma na yeye kifuani, japo ni jitu lenye uzito mkubwa, ila likajikuta likianguka chini kama mzigo na kuwafanya mwenzake kunivamia kwa kunirukia. Wafungwa ambao walikuwepo mbele yangu, tukawakumba na kuanza kubingirika kuelekea chini, huku nikijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kumpiga jamaa huyu visukusuku  vya kichwa, naye akanishindilia ngumi za mbavu ila nikajitahidi kuzuia ngumi zake kwa mikono yangu niliyo ikunja kila pale alipo jaribu kurusha ngumi. Tukafika karibu kabisa na uwanja wa mapambano, hata watu walio kuwa wakishangilia wakakaa kimya wakitutazama. Kitu ninacho jivunia ni kufahamu jinsi ya kuwadhibiti mijitu yenye miili kama hii. Nikashika vidole vya mkono wake wa kushoto, na kuanza kuvunja kimoja baada ya kingine.
 
Maumivu yake yakamfanya apige ukunga mkubwa wa kuomba msaada, wafungwa wengine wakaanza kuingilia ili kuja kumuokoa mwenzao. Hapo ndipo kikapigwa king’ora cha hatari, nikawaona wafungwa wote wakilala chini, kasoro mimi niliye simama na kutazama jinsi wanavyo lala chini. Kitu nilicho kifanya ni kuinyoosha mikono yangu juu na kuiiweka kichwani mwangu na taratibu nikapiga magoti baada ya kuana wanajeshi wakike wanye bunduki zao wakija katika eneo ambalo vurugu zimetokea.

Msichana mmoja akanipiga teke la kifua lililo nifanya nianguke chini, wakanigeuza na kunilaza kifudi fusi na mikono yangu wakaizungusha kwa nyuma na kuipiga pingu. Wakaninyanyua na moja kwa moja wakaniondoa eneo la uwanja. Japo baadhi ya sehemu za mwili wangu zinatoka damu kutokana na kubingirika sana kwenye viti pamoja na kuwakumba wafungwa wengine, sikulijali sana hilo. Wanajeshi hawa ambao ndio walinzi wa hili gereza wakaniingiza kwenye moja ya chumba kisicho na kitu hata komoja. 

Wakaingia wasichana wengine wanne wakiwa wameshika mipira ya maji kama wanayo itumia jeshi la kuzima moto. Wakanitazama kwa macho yasiyo na huruma, maji yaliyo funguliwa kwenye mipira hiyo inayo toa maji kwa kasi ya ajabu tena yakiwa yananguvu sana, wakaanza kunimwagia mwilini mwangu. Kusema kweli nilijikuta nikipata maumivu makali sana huku maji yahoo yakiniyumbisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Nilipo hisi ninaweza kufa kwa kumwagiwa maji haya yenye nguvu, nikajigeuza na tumbu langu nikalielekezea kwenye ukuta, nikawaachia mgongo ambao wakaendelea kuushambulia kwa maji hayo nyenye nguvu hadi nikaishia wanguvu kabisa na kujikuta nikilala chini. Walipo niona nimelegea kabisa, wakanicha na kuufunga mlango wa chumba hichi cheye maji mengi na kunifanya nilale hapa chini huku machozi yakinimwagika na kujiuliza ni kitu gani kinacho endelea kwneye maisha yangu ya hivi sasa.
 
 ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts