Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 85 na 86 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 85 na 86 )

Written By Bigie on Saturday, April 14, 2018 | 3:34:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-                        
ILIPOISHIA    
Tulipo  hakikisha wanajeshi tumewadhibiti na kuwaua wote nata maderava wa magari haya tukaalisogelea gari moja na kulifungua kwenye moja ya kontena. Tukakuta shehena kubwa ya chakula ikiwa impengwa vizuri kwa mfumo wa vigunia.  Tukiwa katika kutazama chakula kilichopo kwenye makontena haya, kwa mbali tukasikia milio ya helicopter za jeshi.  Haikupita hata dakika mbili, helicopter mbili zikawa zimefika aneo la tukio na tukaanza kushambuliwa kutokea juu, jambo ambalo likaanza kutupa wakati mguu sana na kumchanganya kila mmoja aliyopo katika hili eneo hususani Hawa ambaye alisha anza kusherekea ushindi wa chakula hichi kingi kupita hata kilicho teketea kwenye ghala la chakula.

ENDELEA   
Sote tukajibanza kwenye magari haya kwa maana mtu usipo kuwa makini unaweza kujikuta unapoteza maisha. Hawa akatoa ishara nikamuona msichana mmoja akitambaa chini ya magari haya hadi kwenye moja yagari letu tulilo jia. Akachukua bomu moja la kutungulia helcopter, akapiga goti moja chini huku mwengine akiwa amelikunja, kisha akailiweka bomu hilo juu ya bega leke. Akaipima moja ya halcopter, kisha akaliachia bomu hilo ambalo, halikukosea kuelekea kwenye helcopter ambayo lilitumwa.
 
Helcopter hiyo ya wanajeshi wa umoja wa mataifa akalipuka, na kubaki moja. Msichana huo mwenye nguvu kama za kike akachukua bomu jengine na kukaa mkao kama alio kuwa amekaa hapo awali, akafyatua bomu hilo na kuipiga helcopter ya pili, iliyo anza kuzunguka kwa kasi hewani huku ikiwaka motona kuanguka chini.
Baada ya shambulizi hilo, sote tukatoka chini ya magari huku tukiwa tunashangilia. Tuakingia kwenye magari haya, na kuanza safari ya kuelekeea kwenye ngome yetu. Gari ninalo liendesha, lipo nyuma ya kabisa. Huku nyuma yangu kukiwa na gari ndogo moja tuliyo kuja nayo. Safari yetu ikachukua zaidi ya lisaa, tukaw tumesha fika katika ngome yetu. Tukayaingiaza magari hayo yote kwenye ngome yetu, na ulinzi ukazidi kuimarishwa.
“Mkuu kuna taarifa”
Kijana mmoja alizungumza kwa lugha ya kiarabu huku akimtazama Hawa machoni, na mimi nilipo jaribu kuyakutanisha macho yetu na kijana huyo akaonekana kuyakwepesha. Kutokana sikuwa na haja kufwatilia ni taarifa gani ambayo inayo endelea, ikanibidi kuondoka katika eneo hili kueleka katika chumba ambacho tunahifadhia silaha nzito.
Kabla sijatoka katika chumba hichi, wakaingia jamaa wawili wakasimama nyuma yangu.
“Dany upo chini ya ulinzi”
“Chini ya ulinzi!!?”
 
“Ndio”
“Kwa kosa gani?”
“Utakifahamu tu, ukiwa katika chumba cha ulinzi”
Kutokana walio agizwa kunikamata ni afiki zangu, sikuhitaji kufanya fujo yoyote. Nikakubali kuvishwa pingu ya mikononi na nikaongozana nao hadi kwenye chumba maalumu cha mahojiano, ambacho kimefungwa kameza kama sita na kina Tv kubwa inayo onyesha pembe zote za kila kamera ndani ya hichi chumba.
Akaingia moja ya kiongozi ambaye kwa siku zote ambazo huwa nina msalimia hakuwahi kuipokea salamu yangu. Akanitazama kwa macho makali huku akikuna kuna ndevu zake ndefu kama za Osama Bin Laden.
“Asalam alyakum”
Alinisalimia huku akikaa kwenye kiti kilichopo mbele yangu na tumetenganishwa na meza ya chuma katikati yetu.
“Salama”
“Wewe ni nani?”
Swali lake likaanza kunistua akilini mwangu, ila nikajifanya kama sio mtu ambaye ninajijua mimi ni nani.
 
“Mimi ni Dany”
“Ahaaaa nje ya Dany”
“Nje ya Dany mimi ni mwanajeshi wa AL-Shabab”
“Una uhakika?”
“Ndio”
“Nani alihusika na tukio la kuchoma chakula?”
“Siwezi kufahamu”
“Wewe ndio muhusikaaaa”
Alizungumza kwa hasira huku akinyanyuka na kuisogeza sura yake karibu yangu kabisa. Akanitazama kwa macho makali, nikaachia tabasamu pana usoni mwangu.
“Una ushahidi wakunionyesha kwamba mimi ndio muhusika?”
“Ndio”
“Nionyeshe”
Akapiga mluzi, mlango ukafunguliwa akaingia jamaa ambaye kwa mara ya mwisho kuonana naye, Hawa aliniambia kwamba akili zake hazipo vizuri na alitaka kunivamia. Pia kwa mara ya kwanza niliwahi kupambana naye nchini Tanzania, nikiwa kama mlinzi wa raisi. Alipo niona akanitazama kwa macho makali kisha akasimama pembeni ya huyu mkuu wangu.
 
“Huyu jana nilimuona usiku  akiwahsa moto kwenye chakula”
Hata alicho kizungumza, kinaonyesha huyu jamaa akilini mwake kuna hitilafu tena kubwa.
“Unasikia”
“Muheshimiwa ninahisi kwamba umepubazwa na huyo jamaa hadi kupelekea kunihisi kwamba nimehusika katika swala la kuchoma chakula. Ingekuwaje leo niende kuhusika katika kazi ya kutafuta chakula kingine na kukileta hapa kambini?”
Swali langu likamfanya jamaa na huyu mkuu wangu hapa kutazamana.
“Nilikuona jana”
“Mkuu kuna watu wa kuwahisi kwamba wanaweza kufanya hilo jambo  ila si mimi”
Mlango ukafunguliwa na Hawa akaingia, akatutazama wote tulivyo kaa. Akachomoa bastola yake na kumnyooshea huyu jamaa ambaye ni chizi.
 
“Kuishi duniani nahisi umechoka si ndioo?”
Hawa aliuliza kwa ukali hadi jamaa akaanza kutetemeka. Kwa haraka nikanyanyuka na kumshika hawa mkono wake alio shika bastola kwa maana sauti aliyo zungumza nayo ninaitambua vizuri na akizungumza kwa sauti hiyo ambayo haina masihara ndani yake, kwa kile alicho kizamiria basi ni lazima atakifanya kwa sekunde yoyote.
“Tafadhali mkuu nakuomba umsamehe”
Hawa akanitazama kwa macho makali, ila sikuhitaji kuyakwepesha macho yangu. Akainyoosha bastola kwa mkuu huyu mwenye mandevu.
“Na wewe unapelekeshwa na huyu mwanao chizi, kitu anacho kizungumza wewe unaona ni ukweli si ndio?”
Hawa akaendelea kufoka, mkuu huyu akaka kimya kabisa, pasipo kujibu kitu chochote.
 
“Kuanzia sasa huto  kuwa mkuu wa kitengo cha chakula na ninakuvua vyeo vyako vyote. Utabaki kuwa askari wa kawaida”
Hawa baada ya kuzungumza hivyo akamsogelea kiongozi huyu, akakivua kitambaa chenye nyota mbili. Kisha akatoka ndani ya hichi chumba, na kuniacha nikiwa nimeshangaa. Nikamtazama mzee huyu nikamuona jinsi anavyo gugumia kwa kulia moyoni mwake, japo sauti haitoki ila macho yanaonyesha mzee anamwaga chozi. Sikuwa na haja ya kuendelea kukaa ndani ya hichi chumba. Nikatoka huku pingu zangu zikiwa bado mikononi mwangu.
“Nifungueni”
Nikawambia rafiki zangu walio kuwa wamekuja kunikamata, kwa maana hawakuwa mbali na chumba hichi cha mahojiano kwa manaa kila mmoja alishangaa kukamatwa kwangu.
“Imekuwaje huko ndani?”
 
“Ahaa babu ni aibu”
“Aibu?”
“Ahaa mzee, kavuliwa cheo, sasa hivi hana tofauti na sisi tu”
“Weee”
“Ohoo analia na lile chizi lake humo ndani”
“Hahaaaa, kwani chanzo kilikuwa ni nini?”
“Mzee jinga sana, eti alikuwa akinihisi kwamba mimi ndio nimechoma ghala la chakula, shahidi eti anakuja yule chini”
“Haaaaaa, huyu mzee kweli kazi zilimshinda”
“Ohoo yupo ndani huko analia”
Galfa tukasikia mlio wa risasi ukitokea kwenye chumba cha mahojiano na kutufanya sote kustuka. Tukaanza kukimbilia kwenye chumba hicho, hata kabla hatujafika mlangoni tukasikia mlio mwengine wa risasi ulio tufanya tuzidi kuwa makini sana.
 
Nikawa wa kwanza kuingia ndani ya hichi chumba. Nilicho kutana nacho naamini ni kile ambacho kilidhibitishwa na milio ya risasi hizo. Jamaa ambaye akili zake hazipo vizuri, nikakuta akiwa amelala sakafuni huku damu nyingi zikimwagika kichwani mwake. Baba mtu naye, kichwa chake kimechanguka kwa nyuma, kwani alisokomeza bastola yake mdomoni na kujilipua.
“Ohoo Mungu wangu!!”
Rafiki yangu mmoja alizungumza baada ya kuziona hizi maiti mbili hapa. Baba kaamua kumuu mwanaye na yeye akajiua. Nikashusha pumzi nyingi huku nikitoka chumbani humu, nikakutana na Hawa akiwa ameongozana na walinzi wake wa kike, hakunisemesha chochote zaidi ya kuingia katika chumba hichi. Sikwenda mbali na hichi chumba ambacho kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo jinsi wanajeshi wanavyo zidi kufika katika hili eneo.
 
“Ilikuwaje?”
Niliisikia sauti ya hawa nyuma yangu.
“Hata mimi sielewi, ila nilimuacha mzee akilia. Naona ameamua kujiua mwenyewe”
“Jing asana”
Sikuzungumza chochote zaidi ya kukaa kimya.
“Leo usiku nitafanya kijisherehe kidogo, utapata muda?”
“Kinafanyika muda gani?”
“Kuanzia mbili, kule kwenye jumba la baba”
“Nitakuwepo, vipi mzee amrudi?”
“Hapana hajarudi, atarudi wiki ijayo”
“Sawa”
“Hakikisheni munawazika hao”
“Sawa”
Hawa akaondoka na walinzi wake, sikuhitaji kukaa hapa, na mimi nikaelekea chumbani kwangu. Kutokana na uchovu mwingi, nikapanda kitandani na kulala. Usingizi mzito ukanipitia na kulala fofofo.
                                                                                                     ***
    Taratibu nikafumbua macho yangu, nikaka kitako kitandani huku miguu yangu ikiwa imekanyaga chini. Nikatazama dirishani, mwanga hafifu wa jua linalo elekea kuzama, likanionyesha dhairi kwamba jioni inaanza kuingia. Nikanyanyuka kitandani na kuanza kujinyoosha viungo vyangu huku nikipiga miyayo ya usingizi iliyo jaa uchovu mwingi sana.
Nikavua nguo hizi za kazi na kujifunga taulo, nikaelekea bafuni ambapo ni nje kidogo ya chumba changu. Sikukuta watu kabisa katika hili bafu, jambo ambalo si la kawaida sana kwa maana mida ya jioni huwa watu ndio wanaoga. Nikataka kufungua bomba la maji, ila nikasita kidogo kwa manaa nimesha anaza kuhisi kuna jambo ambali si la kawaida katika eneo hili.
Nikachungulia nje, kila mwanajeshi anaendelea na shuhuli zake, nikarudi bafuni na kuanza kuoga, nikiwa katikati ya kupga wakaingia watu wawili walio valia nguo nyeusi huku nyuso zao wakiwa wamezifunga ninja na wamebakisha macho tu.
 
“Mumetumwa?”
Niliwauliza kwa lugha ya kiarabu, ila hapakuwa na aliye nijibu zaidi ya kuanza kunishambulia kwa kasi sana. Kutokana mimi mwenyewe ninajiweza kwa kila hali, nikaanza kurupushani nao. Piga teke, nipige ngumi. Ukichangia na mafunzo ambayo Livna alinipatia, basi jamaa hawa wawili nilianza kuwatembezea mkong’oto mzito ambao hawakutarajia kuupata kutoka kwangu. Wote wawili wakiwa chini wakijishauri kunyanyuka kutokana na kipigo nilicho wapa, nikasikia mlio wa makofi kutokea mlangoni. Akaingia mwalimu wangu wa mazoezi,
“Safi sana”
Alizungumza huku akwia amejawa na sura ya tabasamu, jamaa hawa wawili wakavua vitambaa vilivyo ficha sura zao, wote ninawafahamu, ni miongoni mwa wanafunzi bora wanao ongoza darasani kwa kujitahidi.
“Mtihani wangu umekwenda vizuri sana, juhudi yako kweli ninaiona Dany”
 
“Asante mwalimu kwa maana nilihisi labda ni wavamizi?”
“Yaa ni wavamizi unatakiwa ikitokea kama hivi uhakikishe kwamba unafanya kama unavyo fanya hapo”
“Sawa sawa mwalimu”
“Maliza kuoga, naona sherehe inakwenda kuanza”
“Sawa mwalimu”
Wakatoka huku jamaa hawa wawili wakiwa wanachechemea. Nikamaliza kuoga nikarudi chumbani kwangu. Nikavaa suruali yangu moja ambayo ni safi, nikavalia na tisheti. Nikazichana nywele zangu ndogo vizuri, nilipo hakikisha nimependeza vizuri. Nikavaa buti zangu na kuelekea kwenye jengo kuu lililopo humu kwenye hii ngome. Viongozi na wanajeshi wacheche ndio tumealikwa na Hawa, kufanya hii sherehe ya kufanikiwa kupata chakula ambacho ni mara mbili na chakula ambacho kimeteketea kwa moto. Sote tuliomo ndani ya huu ukumbi mdogo sura zetu tunaonana, ila Hawa hata iwe sherehe, hakuna mtu ambaye anaiona sura yake kutokana na kitambaa cheusi alicho kivaa usoni mwake.
 
Baada ya Hawa kuzungumza maneno mawili matatu, mziki ukafunguliwa na watu wakaanza kuserebuka. Mziki wenyewe sikuweza kuucheza kutokana siuelewi hata unavyo imbwa kwa maana umeibwa kiarabu. Ila viongozi na wanajeshi wengine wakaendelea kuucheza wakiwa wamejawa kwa furaha, ila ninacho kipenda kwenye huu mziki ni neno Golo golo, ambalo hata sielewi maana yake.
 
Hawa kwa mbali akanikonyeza, kisha akaondoka katika ukumbi pasipo watu wengine kuwaona zaidi ya mimi na walinzi wake wawili wa kike, nikanyanyuka kwenye kiti na kumfwata sehemu anapo elekea, nikamuona akipandisha katika ngazi za kuelekea gorofani, nikamfwata kwa nyuma. Akaingia kwenye chumba kimoja na mimi nikaingia chumbani humo. Akaufunga mlango kwa ndani, kisha akanivamia na kunikumbatia huku akivua kitambaa kilicho ificha sura yake. Alipo hakikisha kimeanguka chini, akaanza kuninyonya midomo yangu huku akitoa pumzi nyingi, kitendo kilicho nifanya na mimi kuanza kuipitisha mikono yangu kwenye kila kona ya mwili wake, nikimtomasa kisawa sawa.

AISIIIII……….U KILL ME 86

“Dany stop”
Hawa alizungumza huku akichomoka mwilini mwangu. Akapiga hatua hadi kwenye sofa na kujibwaga na kukaa. Nikatemeba kwa mwendo wa taratibu hadi kwenye sofa alilo kaa.
“Dany sijawahi kufanya kiu kama hichi”
Hawa alizungumza huku akihema sana.
“Kweli?”
“Ndio na sihitaji kufanya hichi kitu, hadi kufa kwangu”
Maneno ya Hawa yakanifanya nibaki nikiwa na kigugumizi. Kwa haraka haraka sina kitu cha kumuuliza kwa maana sielewi nianzie wapi kuuvunja msimamamo wake.
 
“Kwa nini huhitaji kufanya hichi kitu?”
“Dany, mimi ni binti wa kislam, baba yangu amenilea kwenye mazingira ya kidini sana. Nina msimamamo kuliko wasichana wote nahisi, japo msimamamo wa kitu changu kimoja ndio nimeweza kiyumba ila sinto weza kuyumba kwenye kitu kingine. Wewe ndio mwanaume uliye iona sura yangu tofauti na baba yangu, ila sinto weza kumuonyesha mwanaume yoyote hii sura. Pili kwenye swala la kuvunjwa bikra yangu, sinto kubaliana nalo hilo kabisa”
Hawa alizungumza kwa msisitizo kabisa, hata sauti yake imebadilika kwa kiasi kikubwa sana.
“Ahaa sio mbaya ukiwa na msimamo kama huo”
Ilinibidi kuunga mkono hivyo hivyo japo kimoyo moyo nina maumivu ya kukikosa kitumbua cha Hawa.
“Ila ninakuomba unisamehe katika hilo”
“Ahaha hakuna tatizo, mimi nipo sawa tu”
“Dany kwenye maisha yako ya nyuma umesha wahi kuwa na mpenzi?”
“Nilisha wahi kuwa naye, ila kwenye ile ajali ya ndege iliyo tokea, naamini nilimpoteza hapo”
 
“Pole sana”
“Asante”
“Ok fanya uurudi ukumbini isije watu wakatudhania vibaya”
“Pao”
Nikatoka chumbani humu huku nikiwa nimejawa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi isitoshe nina miaezi mingi sana sijawahi kukutana kimahusiano na mwanamke yoyote. Nikafika ukumbini, wala sikuona haja ya kuendelea kukaa ukumbini hapa. Nikaelekea kwenye jengo ambalo lina chumba changu. Nikajifungia ndani, na kuwasha taa, nikajitupa kitandani huku nikiwa na mawazo mengi sana kichwani mwangu. Nikiwa katikati ya dimbwi la mawazo, mlango wa chumbani kwangu ukagongwa, nikakurupuka kwa haraka kitandani, nikaichukua bastola yangu niliyo kuwa nimeiweka pembeni ya kitanda changu. Nikapiga hatua hadi mlangoni, nikaufungua na kukutana na rafiki yangu mmoja ambaye ni miongoni na watu walio kuja kunikamata. Ila cha kushangaza amevaa mavazi ya kawaida na si mavazi kama tuliyo zoea kuvaa wanajeshi wa hichi kikosi cha kigaidi cha Al-Shabab.
“Aisse nilivyo ona taa imewaka, nikaona bora nije kukucheki mwanangu”
“Kuna nini tena?”
“Twende zetu disko tukatembee”
“Disko?”
 
“Ndio, twende ukawaone watoto wazuri wa kisomali.”
“Muna ruhusa ya kwenda huko”
“Ahaa Dany hapa ishu ni kutoroka, niajua njia za kutokea humu kwenye kambi”
“Munakwenda wangapi?”
“Tupo mimi na jamaa, sasa tukaona tukupitie mchizi wetu”
“Sasa kama unavyo ona mimi sina pamba za kutokea”
“Twende sisi tutakupatia”
Kutokana tangu kuingia ndani ya hii ngome nimetoka mara moja na tena nimekwenda jangwani asubuhi hii kwa kazi ya kuteka magari ya chakula sikuona haja ya kuendelea kubaki humu ndani ikiwa nina hamu kubwa ya kukutana kimwili na msichana wa aina yoyote. Nikaongozana na Ruben, hadi kwenye chumba chao. Wakanichagulia jinzi pamoja na tisheti zilizo nitosha vizuri mwilini mwangu. Wakanipatia na kofia niliyo ivaa vizuri, kila mmoja akaiweka bastola yake sehemu anayo fahamu yeye kwenye mwili wake.
 
“Sasa huko nje tutatokaje?”
“Tulia kaka”
Ruben alizungumza huku akivuta kitanda pembeni na kukisukumiza hadi kwenye mlango. Wakafungua kapeti walilo litandaza chini, nikaona mfuniko wa mbao, wakaufungua nao, nikaona shimo kubwa.
“Dany hii ndio njia ambayo tunaweza kutokea ndani ya hii ngome”
“Weee mbona kunga giza”
“Chukua tochi hiyo hapo”
Kila mtu akachukua  tochi yake, tukazima taa za ndani ya chumba hichi. Tukaingia kwenye shimo hili ambalo hakina urefu sana kuelekea chini. Tukaziwasha tochi zetu na kuanza kutembea kueleka mbele. Hili ni bomba kubwa ambalo lina upana wa katosha unao muwezesha mtu kutembea pasipo kuinama wala kujibana.
 
“Tunatokezea wapi?”
“Tutatokezea kwenye fukwe moja hivi ya bahari.”
Kitu liacho kizungumza Ruben nikaanza kukifananisha na kitu ambacho kiliweza kutokea miezi kadhaa nyuma nilivyo kuwa ninatoroka na Vivian kwenye moja ya gereza kubwa. Jambo hili likaanza kunipa mashaka, ila sikutaka kuonyesha wasiwasi wangu upo wapi. Tukatembea zaidi ya dakika thelethini na kutokea kwenye fukwe moja ya bahari.
Mandhari ya hili eneo ni mazuri sana. Tukaanza kutemeba kwenye fukwe hizi kwa dakika kadhaa na tukaanza kukutana na watu  tofauti tofauti ambao wapo kwenye starehe zao, ambapo kuna ukumbi mmoja mkubwa wa starehe.
“Tuna msaa matatu, hadi  kurudi kambini. Pointi ya kukutena ni kwenye ile sehemu tuliyo tokea pale. Sawa Dany”
“Poa washkaji, sasa ninaingiaje humu sina mapene”
“Ohoo ngoja”
Ruben akatoa noti kumi za dola mia mia na kunikabidhi. Kisha kila mmoja akatawanyika na kuelekea anapo pajua yeye kwenye huu ukumbi mkubwa wa starehe. Nikaiweka kofia yangu vizuri, nikalipa kiingilio kwenye huu mlango na kuingia ndani. 
 
Wingi wa watu katika huu ukumbi kweli kulikuwa na haja ya kila mtu kuingia kwa namna yeka, kwa maana kama tungeongozana basi mtu ukimpoteza mwenzako basi unaweza kujikuta unachnganyikiwa, ila kwa jinsi tulivyo ingia basi kazi kubwa ni kwenda na masaa.
Nikatembea moja kwa moja hadi kwenye kaunta ya vijwaji, ambapo kuna viti viwili tu ambavyo havina watu, viti vingine vyote vimejaa watu wakipata vinjwaji. Nikajiweka vizuri tisheti yangu na kukaa kwenye hichi kiti kirefu, nikihakikisha kwamba hakuna mtu anaye iona bastola yangu mezani. Nikatazama tazama vinywaji vyote vilivyopo, nikaagiza kijwaji kinacho itwa Savana kwa maana ni kinywaji ambacho ndio ninakifahamu hata nchini Tanzania vipo, ila hivi vingine sihitaji kuagiza hata kimoja.
Taratibu nikaendelea kunywa huku macho yangu nikitapeleka huku na kule kutazama binti mzuri ambaye ninaweza kumchukua ili akanikate kiu iliyo nitawala kwa miezi mingi sana. 
 
“Hi handsome”
Binti mmoja mweusi na mrefu alizungumza huku tukiwa tumeyagonganisha macho yetu. Sikuhitaji kumjibu chochote kwa manaa simuelewi elewi hata muonekano wake, japo nina hamu kubwa ila si kwa binti huyu.
Nikaendelea kuwatazama wasichana wengine ambao nitaona wanaweza kunivutia. Nikampata msichana mmoja ambaye anacheza na mwenzake, nikampa muhudumu wa kaunta noti ya dola mia, nikamueleza ninarudi. Nikaanza kucheza ninavyo jua mimi huku nikiwa nimewakusudia kufika kwa wasichana hawa. Japo ninaminyana minyana na watu ila nikakutana nao. Nikaanza kucheza huku nikiwa nimememtazama msichana niliye mkusudia mimi kufika hapo, nikaanza kumkonyeza, huku nikimuonyesha ishara ya kumuomba tuzungumze pembeni. Msichana huyu ambaye ana uzuri ambao unavutia wanaume wengi humu ndani, akabaki akitabasamu tu huku akitingisha kichwa.
 
Sikujua ana maana gani ya yeye kutingisha kichwa, nikaendelea kumbembeleza hadi akakubali, akaanza kutangulia kutoka katika kundi hili kubwa la watu ila na mimi nikamfwata kwa nyuma.
Kitu kilicho nishangaza baada ya kumuona amesimama kwenye moja ya sehemu ambayo anaweza kuzungumza ni hili wanaume wanne walio simama pembeni yake huku wakiwa wamevalia suti nyeusi. Nikataka kusita kwenda eneo hilo, ila akaniita kwa ishara. Nikawatazama jamaa hawa ambao nao wamenikazia macho, nikatembea kwa kujiamini hadi katika eneo alipo.
“Mambo vipi?”
Nilimsalimia kwa Kiswahili, akatabasamu kidogo.
“Mimi sijui vizuri kiswali. Ila sana zungumza Engilish na Somalia lugha”
“Ohoo mwenyewe, kisomali ninakifahamu japo ni kidogo sana”
“Ok mimi naitwa Delfina Lameck ni President daughter wa hapa Somalia”
Kidogo nikapata nikastuka, mimi huyu msichana nilihisi labda ni malaya wa humu ndani ya huu ukumbi kumbe ni mtoto wa raisi. 
 
“Ok mimi ninaitwa Dany”
“Dany nani?”
“Dany John”
Ilibidi kuongopea jina la ukoo wangu kwa mana jina la baba yangu ni maarufu sana na inawezekana linafahamika karibia dunia nzima.
“Ohoo hiyo  imekaa vizuri. Ok elezea shida yako”
Nikawatazama hawa jamaa walio kaa karibu na binti wa raisi, nikakosa hata cha kuzungumza kwa maana nikajikuta nina aibu kubwa sana.
“Haloooo”
Delfina alizungumza huku akinitazama usoni mwangu kwa maana niliduwaa kwa sekunde nyingi sana. Gafla nikamuona mlinzi mmoja akianguka chini huku damu nyingi zikimwagika, sikukaa vizuri akafwatila mlinzi wa pili kuanguka chini. Jambo lililo nifanya nimuinamishe Delfina chinia na kumsogeza sehemu ambayo ina usalama mkubwa sana kwa manaa risasi ambazo zimewapiga hawa walinzi wawili zimetokea kwa mtu ambaye ni mdunguaji na bunduki yake haitoa mlio  wowote na imefungwa kiwambo cha kuzia sauti.  Walinzi wawiliw alio baki wakafyatua risasi juu nak uwafanya watu wote kuchanganyikiwa na kuanza kukimbia kimbia hovyo wakijitahidi kutoka ndani ya huu ukumbi ili kuyaokoa maisha yao.
 
“Tulia chini”
Nilimuambia Delifina huku nikichomoa bastola yangu kiunoni mwangu, nikatazama ni wapi alipo mdunguaji. Walinzi hawa wawili walio jibanza kwenye moja ya viti wakaendelea kufyatua risasi kwenye moja ya sehemu ya juu iliyopo gorofa ya kwanza na hapo ndipo alipo jificha mdunguaji huyo anaye jitokeza mara moja moja kufanya shambulizi kwa walinzi hawa walio jificha.
Walinzi  wakaendelea kujibu mashabulizi ya muuaji huyu anaye onekena ametumwa na amedhamiria kuja kufanya mauaji kisawa sawa kwa binti huyu wa raisi.
“Ni njia gani ambayo tunaweza kutokea?”
Nilimuuliza Delfina, ila hakunijibu chochote zaidi ya kuyaziba masiko yake huku mwili mzima ukiwa unamtetemeka kwa woga. Nikamshuhudia mlinzi wa kwanza akianguka chini naye akifa. Ikawa ni muda wa mimi kujibu mashambulizi kwa mshambuliaji huyo ambaye ana silaha zenye uwezo mkubwa kuliko bastola tunazo tumia.
 
“Hei broo ni linde nitoke na Delfina”
Nilimuambia mlinzi aliye salia akaninyooshea dole ngumba la mkono wa kulia. Akabadilsha magazine ya bastola yake kisha akaanza kufyatua risasi mfululizo zilizo mfanya mshambuliaji kujibanza kwenye nguzo aliyo kuwepo. Hii ndio nafasi ya pekee kutoka na Delfina katika hili eneo, nikamshika mkono Delifina na kuanza kukimbia naye kuelekea nje. Tukafanikiwa kutoka nje, huko nako, tukakuta watu wengi wakiwa wamepigwa risasi za wameanguka chini.
“Njia hii”
Delfina alizungumza huku akinishika mkono akikimbia akihakikisha anajitahidi kufika atika eneo  la maegesho ya magari. Watu si chini ya wanne wakiwa na bunduki mikononi mwao wanatukimbiza. Kazi yangu ni kujibu mashambulizi huku Delfina akijitahidi kukimbia kwa uwezo wake wote. Akafika kwenye maegesho ya magari, gari alilo kusudia kuingia, kwa bahati mbaya akakuta limefungwa.
“Funguo anazo mlinzi mmoja na amesha kufaa”
Delifina alizungumza huku akihema.
“Inama chini”
Nilitoa kauli hiyo baada ya watu hawa kutukaribi, tukajibanza kwenye moja ya gari huku sote tukigema. Akanitazama usoni mwangu, sote jasho jingi linatumwagika, uzuri kofia yangu haijaanguka, kwa jinsi nilivyo ivaa si rahisi kwa mtu kuweza kuiona sura yangu halisi.
 
Nikatoa magazine yangu, nikaikuta ina risasi mbili tu ndio zimesalia. Delfina akanitazama usoni mwangu pasipo kuzungumza kitu chochote. Pembeni ya haya maegesho ya magari kuna kiporomoko chenye miti mingi mirefu kwenda juu.
“Unawajua hawa watu wanao hitaji kukuua?”
Nilimuuliza Delfina kwa sauti ya chini.
“Ndio ninawaju……..”
Hata kabla hajamalizia sentensi yake, risasi ikapasua kioo cha gari hili tulilo jicha. Nikaingiza magazine kwenye bastola yangu. Nikaiweka sawa na kufyatua risasi moja iliyo mpata adui mmoja ambaye alikuwa karibu kabisa na hili gari. Wezake wote wakajibanza kwenye magari mengine, nikamshika mkono Delfina na kuanza kuingia naye kwenye huu msitu huku tunakimbia kwa kasi kubwa. Watu hawa wanao taka kumuu Delfina nao wakaanza kutukimbiza kwa kasi kubwa. 
 
Kitu ambacho nimekikubali kwa haraka kwa Delfina ni mwepesi sana kwenye kukimbia. Yeye ndio akawa ananiongoza wapi tupite. Risasi zinaendelea kutuandama nyuma yetu, ila sikukata tamaa zaidi ya kuendelea kukimbia kwa kasi sana. Hadi ikafikia hatua tukawapoteza hawa wauaji.
“Dany mimi nimesha fika nyumbani”
Delifina alizungumza huku akisimama, nikatazama kwa mbali nikaona uwanja  wenye nyasi nzuri na kwa mbele kuna majengo yanayo waka taa.
“Hapa ndio ikulu?”
“Ndio”
“Ni watu gani ambayo wanahitaji kukua?”
“Ni adui wa baba yangu, anaitwa Livna Livba na hii sio mara yake ya kwanza kuhitaji kuniua. Asante sana Dany na Mungu akubariki”
Delfina alizungumza akanibusu shavuni na kuondoka huku akikimbia. Taswira ya Livna amsaliti wangu ikaanza kunijia kichwani mwangu, nikajikuta nikitawaliwa na hasira kali na kwa haraka nikageuka na kuanza kurudi msituni huku nikikimbia, nikihitaji kumkamata mmoja wa watu wake nimpatie meseji atakayo ipeleka kwa bosi wake
                                                                            ITAENDELEA   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts