Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Sita ( 46 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Sita ( 46 )

Written By Bigie on Sunday, April 1, 2018 | 4:09:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

“Siipendi siasa, na sidhani kama ninaweza kuwa mbunge”
“Je kuna ukweli wowote kwamba wewe umepandikizwa roho ya nyoka?”
Swali la muandishi huyu wa habari likanifanya niiname chini ya meza kwani nilijikuta nikikasirika sana jambo ambalo taratibu nikanza kuhisi mabadiliko kwenye mwili wangu, ubaridi mkali ukaanza kunitawala, huku ukiambatana na mikono yangu kuanza kubadilika jambo lililo anza kuniogopesha

ENDELEA
Nikastukia nikifunikiwa na taulo mgongoni, kuangalia vizuri nikamkuta ni Rahma ndio amenifunika na taulo ambalo limelowana maji, kidogo nikaanza kujihisi vizuri hata ubaridi mkali na mabadiliko kwenye mikono yangu vikaanza kuputea taratibu hadi nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida
“Unajisikiaje mume wangu?”
Rahma aliniuliza kwa sauti ya chini ya kunong’oneza sana, ambayo sio rahisi kwa mtu yoyote kusikia
 
“Nipo powa”
“Twende basi ukapumzike ndani”
“Sawa”
“Jamani wapendwa Mr kidogo hali yake sio nzuri sana, ninawaomba mummpe muda kidogo, na mahojiano yataendelea jioni kwenye tafrija ndogo niliyo waandaliaa”
Rahma alizungumza na waandishi wa habari, taratibu akaninyanyua kwenye kiti, tarataibu tukaanza kuelekea ndani, Rahma kwa utaratibu akanilaza kitandani na kuniwashia feni lililopo pembeni ya kitanda changu
“Eddy vumilia, mume wangu”
“Mbona imekuwa hivi, sielewi?”
“Mume wangu pumzika kwanza nitakujibu baadaye”
Rahma alianza kunibembeleza taratibu, akaniacha na kwenda nje kuendelea na maandalizi ya tafrija fupi aliyo iandaa, nikaanza hihisi harufu ya tofauti ndani ya chumba changu, na taratibu nikaanza kunyanyuka kitandani mwangu, huku nikiongozwa na pua zangu, kunusa ni wapi harufu hiyo inapo tokea.Nikaanza kusikia vikopo vya kuwekea ,afuta vilivyopo bafuni vikianguka,
 
“Ni nini?”
Nilijiuliza kwa maana ndani kwat hakuna panya wala paka anayeweza kufanya uharibifu kama huo.Nikaendelea kutembea kwa umakini hadi bafuni na kukuta vikopo vyote vya mafuta na sabuni zikiwa chini, harufu nayo sikuihisi ndani mwangu tena.Nikaanza kuokota kimoja baada ya kingine, nikiwa nimeinama nikastukia kuiona miguu ya mwanake nyuma yangu, kupitia kioo kilichopo mbele yangu ikiwa inavuja damu nyingi, nikasimama na kugeuka na kukutana na binti wa miaka kama kumi na nane akiwa anavuja damu mwili mzima
Macho yake ameyatoa kiasi kwamba anaonekana kubanwa na kitu kwenye koo lake,
“Ni…nisa..idie”
Alizingumza kwa shida sana kiasi kwamba nikabaki nikiwa nimeshangaa kwani sikujua ameingiaje ingiaje ndani kwet na istoshe sikujua ni kitu gani kilicho mpata
“Wewe ni nani?”
“Ni…saaa iii..dieee”
Aliendelelea kuzungumza kwa shida sana, nikajaribu kuuinua mkono wangu ili nimpe, nikajihisi uzito mkubwa sana kutoka kwenye mkono wangu
 
“Ed….ddy nisai…diee”
Nikaanza kuulazimisha mkono wangu wa kulia kunyanyuka ila nikajikuta nikishindwa, kuunyanya na zaidi nikabaki nikiwa nimesimama kama namba moja, Gafla upepo mkali ukaanza kutawala ndani ya bafu na kunirusha na kuniangusha chini.Nikamuona Olvia Hitler akiwa amesimama katikati ya upepo unaozunguka mithili ya kimbunga kikali, gafla nikastukia Olvia Hitler akimvuta binti huyo na kumuingiza katikati ya upepo na kupotea mbele ya macho yangu
“Mmmmm”
Nilibaki nikiwa nimeguna tu kwani sikuelewa kitu kinacho endelea kati ya mtoto huyo na Olvia Hitler ambaye kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa katika hali mbaya sana kwenye mwili wake, ila ujio wake wa sasa upo tofauti sana.Nikajinyanyua kwa msaada wa kishika kuta za kioo zilizopo bafuni mwangu, kisha nikaelekea chumbani na kujitupa kitandani
 
Hadi unafika wakati wa tafrija sikuwa na furaha moyoni mwangu, japo usoni mwangu ninajikaza kutabasamu mbele ya wageni waalikwa, akili yangu yute inakazi ya kumfikiria binti niliye muona bafuni mwangu
“Habari yako kaka Eddy”
Msichana mmoja aliye valia suti nyeusi alizungumza huku akinipa mkono
“Salama tu mambo vipi?”
“Salama tu, Mimi ninaitwa Rejina, nimuandishi wa vitau vya story kama huto jali ninaomba kuzungumza mimi na wewe”
“Sawa, tunaweza kuzungumza”
“Ombi langu kubwa ambalo ninahitaji kukuomba kwako ni kwamba, ninaomba niiandike story ya maisha yako ninaimani kitabu chako kitauza sana”
“Kwa nini umeamua au umependela kuandika kitabu cha maisha yangu na sichawatu wengine?”
 
“Wewe, umepitia mambo mengi sana kwenye maisha yako japo sisi watu tunatambua machache ila kusema ukweli wewe kama wewe utakuwa na mambo mengi sana ya kuniadisia na mimi nikayaweka kwenye maandishi na kuwa kumbukumbu nzuri hata kwavizazi vijavyo”
“Nipe muda nilifikirie hilo”
“Ila kaka Eddy, kuna kitu nakuona kinakukosesha raha?”
“Hapana, nipo sawa tu”
“Sawa hii ni kadi yangu inanamba za simu ukiwa tayari ninaomba uwasiliane na mimi”
“Poa”
Nikapokea kadi ya mawasiliano ya Regina na akanikumbatia na kuondoka zake, na kuniacha nikiangalia jinsi watu wanavyo sakata mziki, nikaanza kukisoma kikadi alicho nipa Regina na kukuta maandishi ya jina lake na kampuni anayo ifanyia kazi, nikakuta namba zake mbili za simu za mitandao tofauti.Nikakiingiza mfukoni mwangu na kugeuka upende wa kushoto na kumkuta Rahma akiwa amenitazamakwa macho makali, baada ya macho yetu kukutana Rahma akaachia msunyo mkali nakuondoka kwa hasira
 
“Anataka nini naye huyu?”
Nilijiuliza swali mimi mwenyewe, sikutaka kumfwatilia sana Rahma zaidi ya kumuwazia msichana niliye muona akiniomba msaada bafuni.Nikatafuta kiti nakukaa, wakaja baadhi ya wageni waalikwa wakakaa na mimi na tukaanza kupiga stori za hapa na pale, wengine wakinipongeza kwa kazi niliyo ifanya
Gafla nikamuoma msichana aliye nitokea bafuni akiwa amesimama kwenye geti la kuingialia ndani kwangu,
“Samahani jamani, ninakuja sasa hivi”
“Sawa muheshimiwa”
Nikaanza kunyanyuka na kupita pembezoni mwa bwala la kuogelea walilo jaa baadhi ya wageni waalikwa wakiburudika, sikutaka kuyakwepesha macho yangu sehemu yoyote zaidi ya kumfwata binti aliyepo mbele yangu,huku akiwa katika muonekano wake ule ule wa kuvunjwa  na damu mwili mzima.Cha kustaajabisha nikaanza kumuona akiingia ndani, huku akipishana na watu wengine pasipo wao kumuona, nikazidi kuongeza mwendo wa kumfwatilia nikashangaa akielekea kweny vyumba vya chini akiacha kupanda vya ghorofani.
 
Akaingia kwenye moja ya chumba na mimi nikaingia pasipo kubisha hodi, gafla macho yangu yakakutana na Regina akiwa mtupu kama alivyo zaliwa huku mwili wake ukiwa umejaa maji, akionekana kutoka kuoga, nikatazama kila kona ya chumba na sikumuona binti ambaye nilikuwa ninamfatilia, Regina hakuonekana kushangaa wala hukuficha sehemu zake za siri, zaidi akabaki akiwa ametabamu na kuanza kupiga hatua za kunifwata, gafla nikastukia mlango ukifunguliwa nyuma yangu na nilipo geuka nikakutana na Rahma akiwa anatushangaa

 ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts